Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Mkuu Leads ni kifaa gani?
Au unamaanisha Coil za plugs?
Zinahusiana na ignition coil kwa ajili ya kuchoma plugs....Zikichakaa zinakuwa na tabia ya kuvujisha umeme, hivyo umeme kidogo ndiyo unakwenda kwenye spark plugs, hapo utakosa nguvu ya gari na utapata miss zisizoisha..
 
Leads ndyo nini?
Hizi hapa....zipo tofauti tofauti kulingana na aina ya gari
Ignition-Leads.jpg
 
Ufumbuzi kuhusu gari yangu kukosa nguvu mlimani jibu nimelipata leo baada ya kulipeleka Gereji na likakaguliwa na Fundi kila kona na ikabainika Leads kukosa ubora(kutorosha moto pembeni)

Ishu hiii imenifanya nishant sana kuwa katitu kadogo tu kanaweza kunikwamisha safari yangu....aiaeee kweli mzungu mchawi sanaa daaaaaah ....basi nikaomba nibadilishiwe na kupewa zingineee ingawa gari yangu inaonekana kuwa selective sana kwenye hizi leads aiseee basi nimeungaunga hivyo hivyo nikabahatika kupata 3 nzima na moja kimeo.

Now mlimani napanda kama nashuka vilee kitu mnato yani nafidiaaa mateso yote[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ulipeleka gereji gani?
 
Zinahusiana na ignition coil kwa ajili ya kuchoma plugs....Zikichakaa zinakuwa na tabia ya kuvujisha umeme, hivyo umeme kidogo ndiyo unakwenda kwenye spark plugs, hapo utakosa nguvu ya gari na utapata miss zisizoisha..

Actually siyo kuvujisha umeme. Hizi cable huwa zinakuwa na resistance. Sasa hiyo resistance ikizidi utahitaji umeme mwingi zaidi ili kuweza kupata spark inayohitajika. Ndio maana gari inamiss.

Ni kama tu zilivo components zingine kwenye gari. Component yoyote ya umeme ikiwa na poor grounding inaweza basi lazima itafanya kazi chini ya kiwango sababu poor grounding inaongeza resistance. Na ndio maana engine ikiwa na poor grounding inaweza isiwake kabisa au ikawaka kwa shida.
 
Poor ground kivipi Mkuu, hizo cable kazi yake ni kupitisha moto wa coil/ spark kwenda kwenye plug ili kuwasha mvuke kwenye piston chamber hazihitaji earth au ground
zikichoka hata moto haupiti (labda mm ushamba wangu nijaribu kufunga nyaya nipitishie na ground / ndipo napokwamia uelewa wangu)
High tension leads - Wikipedia
High tension - Wikipedialeads

High tension leads or high tension cables or spark plug wires or spark plug cables are the wires that connect a distributor, ignition coil, or magneto to each of the ...
 
Actually siyo kuvujisha umeme. Hizi cable huwa zinakuwa na resistance. Sasa hiyo resistance ikizidi utahitaji umeme mwingi zaidi ili kuweza kupata spark inayohitajika. Ndio maana gari inamiss.

Ni kama tu zilivo components zingine kwenye gari. Component yoyote ya umeme ikiwa na poor grounding inaweza basi lazima itafanya kazi chini ya kiwango sababu poor grounding inaongeza resistance. Na ndio maana engine ikiwa na poor grounding inaweza isiwake kabisa au ikawaka kwa shida.
Hapo ulipozungumzia mambo ya ground ndiyo sijaelewa vizuri...

Ninachojua body zima la gari ni ground, block engime, cylinder head vyote hivi huungwa na grounding wire...

Kwa hiyo hizo leads kazi yake ni kupeleka umeme (High voltage ) kwenye plugs na voltage hii huwa ni positive(+)...

Leads huunganishwa kwenye positive (+) electrode ya plug na grounding/negative (-) electeode ya plug huwa ni ile sehemu yenye threads ambayo hujifunga kwwnye cylinder head...

Hizi leads zinapitisha HV...High voltage kiasi kwamba ikiwa na mchubuko mahali umeme unaruka nje na kutafuta grounding iliyopo karibu...hapo ndiyo unakuta cylinder husika inamiss na gari kukosa nguvu..

Imeshanitokea kwenye gari ndiyo maana naeleza hivi..

Sasa kuna yale magari ambayo coil zake zipo pale pale juu ya plugs, hata hizi zile rubber boots zake au tuziite leads kuna wakati zinachoka zinatoka katundu kadogo tu, basi hapo umeme wa positive unaruka na kwenda kwenye block engine ambayo ina act kama ground...hapo utapata miss isiyoisha mpaka ubadilishe hiyo rubber/lead au ufunge na insulate tape ili ikutoe porini ufike mjini..

Nipo tayari kukosolewa.
 
Hapo ulipozungumzia mambo ya ground ndiyo sijaelewa vizuri...

Ninachojua body zima la gari ni ground, block engime, cylinder head vyote hivi huungwa na grounding wire..

Suala la ground nililisema nikiwa najaribu kuonesha adhari ya electrical resistance kwenye flow ya umeme. .

Hilo suala unalozungumzia ww kuhusu kuchubuka nalifahamu. Kwamba kama hiyo cable haiko well insulated basi huwa kunakuwa na sparks ambazo zinajump kuja kwenye sehemu ya juu ya engine ukiwa umewasha gari.

Nilichokuwa najaribu kueleza ni kwamba hizo nyaya huwa zinakuwa na resistance, tena ni resistance kubwa tu, Mfano ukiukuta waya ambao ni Carbon resistance yake huwa inakuwa around 12k Ohms. Sasa kutokana na kwamba hizo nyaya zinafanya kazi katika mazingira ambayo zinakutana na chemicals( mfano fuels), electrical stress na high temperature. Haya mazingira huwa yanafanya hiyo resistance inaongezeka na kuvuka ile ambayo inatakiwa na hivyo kupelekea umeme unaoflow kuwa mdogo kuliko ule unaohitajika.

Kwa hiyo kuna waya unaweza kuwa uko well insulated lakini una resistance kubwa kuliko inayohitajika, Hapo mtabadili kila kitu kwenye gari ila kama huo waya upo gari itamiss tu.

Halafu kinachovuja kwenye waya wenye bad insulation siyo umeme ila ni sparks. Ndio maana moja ya test ya kujua kama huo waya uko well insulated ni kuumwagia maji wakati engine inarun. Kama ungekuwa ni umeme basi watu wanaofanya hizo test wangekuwa wanapigwa shoti mbaya sana maana umeme unaopita kwenye hizo coil huwa unafika mpaka 45kV.
 
Hapo ulipozungumzia mambo ya ground ndiyo sijaelewa vizuri...

Ninachojua body zima la gari ni ground, block engime, cylinder head vyote hivi huungwa na grounding wire...

Kwa hiyo hizo leads kazi yake ni kupeleka umeme (High voltage ) kwenye plugs na voltage hii huwa ni positive(+)...
Mkuu haya ndio Majibu halisi ya hizo nyaya
na namna ya kuzitest ni kuichomoa kwa kuishika na gloves au rubber yoyote uitoe kwenye Plug wakati gari ikiwa ina run bila kuweka gear, utaona tu engine inapunguza mzunguko wa idadi ya piston
ukiichomoa na gari kuelekea kuzima unacheki Plug km ni nzima basi wire una mushkeli
tusimwagie maji
siwezi kukukosoa wewe ni fundi hasa wa muda mrefu
 
Unaangalia vipi kama spark plug ni nzima?
 
Poor ground kivipi Mkuu, hizo cable kazi yake ni kupitisha moto wa coil/ spark kwenda kwenye plug ili kuwasha mvuke kwenye piston chamber hazihitaji earth au ground
zikichoka hata moto haupiti (labda mm ushamba wangu nijaribu kufunga nyaya nipitishie na ground / ndipo napokwamia uelewa wangu)

Hiyo poor ground ni paragraph tofauti. Na nilikuwa najaribu kuonesha athari ya resistance kwenye operation ya hizo electrical components...

Point yangu ilikuea kwenye resistance na siyo hivyo vitu vingine.
 
umeeleweka
 
Ok nimekusoma vyema..
Suala la ground nililisema nikiwa najaribu kuonesha adhari ya electrical resistance kwenye flow ya umeme. .

Hilo suala unalozungumzia ww kuhusu kuchubuka nalifahamu. Kwamba kama hiyo cable haiko well insulated basi huwa kunakuwa na sparks ambazo zinajump kuja kwenye sehemu ya juu ya engine ukiwa umewasha gari.

Nilichokuwa najaribu kueleza ni kwamba hizo nyaya huwa zinakuwa na resistance, tena ni resistance kubwa tu, Mfano ukiukuta waya ambao ni Carbon resistance yake huwa inakuwa around 12k Ohms. Sasa kutokana na kwamba hizo nyaya zinafanya kazi katika mazingira ambayo zinakutana na chemicals( mfano fuels), electrical stress na high temperature. Haya mazingira huwa yanafanya hiyo resistance inaongezeka na kuvuka ile ambayo inatakiwa na hivyo kupelekea umeme unaoflow kuwa mdogo kuliko ule unaohitajika.

Kwa hiyo kuna waya unaweza kuwa uko well insulated lakini una resistance kubwa kuliko inayohitajika, Hapo mtabadili kila kitu kwenye gari ila kama huo waya upo gari itamiss tu.

Halafu kinachovuja kwenye waya wenye bad insulation siyo umeme ila ni sparks. Ndio maana moja ya test ya kujua kama huo waya uko well insulated ni kuumwagia maji wakati engine inarun. Kama ungekuwa ni umeme basi watu wanaofanya hizo test wangekuwa wanapigwa shoti mbaya sana maana umeme unaopita kwenye hizo coil huwa unafika mpaka 45kV.
 
Wakuu naomba msaada wenu natumia gari aina ya Toyota Raum.

Siku hizi mbili gari yangu imekua ikikosa nguvu haswa mlimani pamoja na kuchelewa kubadili gia pia imeandamwa na miss nyingi.

Injini 4E.

Naomba msaada wa ushauri nn cha kufanya.
Badili Spark plugs, Weka Denso (Iridium) kisha uje kunishukuru!
 
mm huwa napigwa shot au nauelekeza kwenye Body ambayo imeunganishwa na (-) ya betri
Du..umetisha..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji23][emoji23][emoji23]

Usijaribu tena kujijaribishia kwenye mwili wako....Dunia bado inakuhitaji..
 
nashukuru mkuu lkn boysperner ndivyo tulivyoanza
lkn kuniambia nizimwagie maji hiyo test siiamini labda wewe mkuu ujaribu na ndoo
 
Back
Top Bottom