Suala la ground nililisema nikiwa najaribu kuonesha adhari ya electrical resistance kwenye flow ya umeme. .
Hilo suala unalozungumzia ww kuhusu kuchubuka nalifahamu. Kwamba kama hiyo cable haiko well insulated basi huwa kunakuwa na sparks ambazo zinajump kuja kwenye sehemu ya juu ya engine ukiwa umewasha gari.
Nilichokuwa najaribu kueleza ni kwamba hizo nyaya huwa zinakuwa na resistance, tena ni resistance kubwa tu, Mfano ukiukuta waya ambao ni Carbon resistance yake huwa inakuwa around 12k Ohms. Sasa kutokana na kwamba hizo nyaya zinafanya kazi katika mazingira ambayo zinakutana na chemicals( mfano fuels), electrical stress na high temperature. Haya mazingira huwa yanafanya hiyo resistance inaongezeka na kuvuka ile ambayo inatakiwa na hivyo kupelekea umeme unaoflow kuwa mdogo kuliko ule unaohitajika.
Kwa hiyo kuna waya unaweza kuwa uko well insulated lakini una resistance kubwa kuliko inayohitajika, Hapo mtabadili kila kitu kwenye gari ila kama huo waya upo gari itamiss tu.
Halafu kinachovuja kwenye waya wenye bad insulation siyo umeme ila ni sparks. Ndio maana moja ya test ya kujua kama huo waya uko well insulated ni kuumwagia maji wakati engine inarun. Kama ungekuwa ni umeme basi watu wanaofanya hizo test wangekuwa wanapigwa shoti mbaya sana maana umeme unaopita kwenye hizo coil huwa unafika mpaka 45kV.