Okay kwa haya maelezo yako kuna uwezekano mkubwa Throttle position sensor ikawa ina shida, kwa sababu hii ndio sensor inayopeleka taarifa kwenye ECU kuwa throttle imeopen kwa nafasi kubwa kiasi gani wakati unaendesha gari.
Kwa hiyo unapokuwa unakanyaga ukifika hapo kwenye 3 badala ya kuendelea kupeleka taarifa kwamba throttle inazidi kuopen yenyewe itakuwa inapeleka taarifa kwamba throttle imeopen kidogo na hivyo kupelekea hewa nyingi kuendelea kuingia kwenye engine wakati ECU inallow mafuta kidogo yaende, na hapo ndio linayokea hilo tatizo la kukosa nguvu...