Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Je inajipandiaha na kujishusha tu wakati unaendesha? Au hata ukiiwasha tu ukaiacha idle?
Wakati unaendesha ukikanyaga inaenda mpaka labda kwenye tatu then inashuka na gari kukosa nguvu, lakini ikiwa silence haivuki kwenye mbili inakuwa katikati ya moja na mbili
 
Okay kwa haya maelezo yako kuna uwezekano mkubwa Throttle position sensor ikawa ina shida, kwa sababu hii ndio sensor inayopeleka taarifa kwenye ECU kuwa throttle imeopen kwa nafasi kubwa kiasi gani wakati unaendesha gari.

Kwa hiyo unapokuwa unakanyaga ukifika hapo kwenye 3 badala ya kuendelea kupeleka taarifa kwamba throttle inazidi kuopen yenyewe itakuwa inapeleka taarifa kwamba throttle imeopen kidogo na hivyo kupelekea hewa nyingi kuendelea kuingia kwenye engine wakati ECU inallow mafuta kidogo yaende, na hapo ndio linayokea hilo tatizo la kukosa nguvu.

Kama gari yako ina Accelerator pedal sensor nayo ingeweza kupelekea hilo tatizo.

Anyway kama ungekuwa Morogoro ningekupimia hiyo sensor before ubadili nyingine ili kama tatizo siyo hiyo sensor usingeingia gharama ya kununua sensor nyingine Ila lingetafutwa tatizo exact lipo sehemu gani.

Kama gari yako ina OBD2 port unaweza kupita kwa mtu mwenye OBD2 scanner akakufanyia scanning. Inaweza kukupa picha shida ipo wapi.

Kila la heri mkuu.
 
Okay kwa haya maelezo yako kuna uwezekano mkubwa Throttle position sensor ikawa ina shida, kwa sababu hii ndio sensor inayopeleka taarifa kwenye ECU kuwa throttle imeopen kwa nafasi kubwa kiasi gani wakati unaendesha gari.

Kwa hiyo unapokuwa unakanyaga ukifika hapo kwenye 3 badala ya kuendelea kupeleka taarifa kwamba throttle inazidi kuopen yenyewe itakuwa inapeleka taarifa kwamba throttle imeopen kidogo na hivyo kupelekea hewa nyingi kuendelea kuingia kwenye engine wakati ECU inallow mafuta kidogo yaende, na hapo ndio linayokea hilo tatizo la kukosa nguvu...
Wewe jamaa ungekuwa DAR tungekuja wengi Sana Kwenye garage yako. Ila yote Kwa yote asante Kwa ushauri
 
Wewe jamaa ungekuwa DAR tungekuja wengi Sana Kwenye garage yako.....
Ila yote Kwa yote asante Kwa ushauri

Shukrani sana mkuu. In fact Dar ntafungua tu kijiwe siku moja... Hata kama itakuwa ni chini ya mti. Maana kazi zangu ni za kufanya masaa machache tu. So mtu anakuja namuhudumia anaondoka na gari lake. Simple.
 
Okay kwa haya maelezo yako kuna uwezekano mkubwa Throttle position sensor ikawa ina shida, kwa sababu hii ndio sensor inayopeleka taarifa kwenye ECU kuwa throttle imeopen kwa nafasi kubwa kiasi gani wakati unaendesha gari.

Kwa hiyo unapokuwa unakanyaga ukifika hapo kwenye 3 badala ya kuendelea kupeleka taarifa kwamba throttle inazidi kuopen yenyewe itakuwa inapeleka taarifa kwamba throttle imeopen kidogo na hivyo kupelekea hewa nyingi kuendelea kuingia kwenye engine wakati ECU inallow mafuta kidogo yaende, na hapo ndio linayokea hilo tatizo la kukosa nguvu...
Mkuu nashukuru sana mimi nipo mafinga Iringa kuna jamaa alifanya diagnosis akaniambia kuwa ni hiyo throttle position sensor! Wakati anafanya sikuwepo ndo maana nikaona nifanye verification huku kwenu wataalamu.
Asante mkuu
 
Basi mkuu wewe funga tu throtle position sensor mpya then enjoy your car.
 
Fanya utembee Dar mkuu hayo mambo ya gar kukosa nguvu ni mengi sana, ndo maana watu wengi sana wanatamani uje dar, maana kwa ule uzi wako ulitia moyo watu wengi sana. Pia ulionesha uwezo mkubwa sana aiseee...ila watu walichoka pale tuu uliposema unapatiaka Moro. Fanya ukaribie huku hata kwa wiki moja tu mkuu.

Hizi gari za kisasa hayo ndo magonjwa yake makuu ya kukosa nguvu.
 
Fanya utembee Dar mkuu hayo mambo ya gar kukosa nguvu ni mengi sana, ndo maana watu wengi sana wanatamani uje dar, maana kwa ule uzi wako ulitia moyo watu wengi sana...pia ulionesha uwezo mkubwa sana aiseee...ila watu walichoka pale tuu uliposema unapatiaka Moro. Fanya ukaribie huku hata kwa wiki moja tu mkuu....

Hizi gar za kisasa hayo ndo magonjwa yake makuu ya kukosa nguvu.

Mkuu si magari tuu hata vijana wa sasa nguvu ni tatizo sana
 
Okay kwa haya maelezo yako kuna uwezekano mkubwa Throttle position sensor ikawa ina shida, kwa sababu hii ndio sensor inayopeleka taarifa kwenye ECU kuwa throttle imeopen kwa nafasi kubwa kiasi gani wakati unaendesha gari.

Kwa hiyo unapokuwa unakanyaga ukifika hapo kwenye 3 badala ya kuendelea kupeleka taarifa kwamba throttle inazidi kuopen yenyewe itakuwa inapeleka taarifa kwamba throttle imeopen kidogo na hivyo kupelekea hewa nyingi kuendelea kuingia kwenye engine wakati ECU inallow mafuta kidogo yaende, na hapo ndio linayokea hilo tatizo la kukosa nguvu...

We jamaa ni noma sana ubarikiwe mkuu
 
Fanya utembee Dar mkuu hayo mambo ya gar kukosa nguvu ni mengi sana, ndo maana watu wengi sana wanatamani uje dar, maana kwa ule uzi wako ulitia moyo watu wengi sana...pia ulionesha uwezo mkubwa sana aiseee...ila watu walichoka pale tuu uliposema unapatiaka Moro. Fanya ukaribie huku hata kwa wiki moja tu mkuu....

Hizi gar za kisasa hayo ndo magonjwa yake makuu ya kukosa nguvu.

Mkuu Dar ntakuja tu... Ni mambo yangu tu hayajakaa sawa. Hapa napanga mambo yangu nataka atleast kila weekend niwe nakuwa dar. Ila mambo yakikaa poa nitahamishia mishemishe dar.
 
Cheki alternator boss. Yangu pia shida ndo ilikua hyo. Ikafika mahali ikazima kabisa, haiwaki
 
Naombeni kujua shida nini, gari kama hiyo inapoteza nguvu. ukiwa kwenye mwendo ghafla unakutana na hali ya gari kukosa nguvu mfano wa kuzibwa pumzi au wewe unakanyaga mafuta na mwingine anakanyaga break.

naomba kujua inasababishwa na nini na utatuzi wake ni nini?

Gari ni Nissan HardBody
Engine ZD30 Turbo.
 
Matatizo ya kukosa nguvu kwa sehemu kubwa yanaweza kusababishwa na:-

1. Mechanical probles kama compression ndogo, air filter kuziba, fuel filter kuziba, Au kuziba kwa exhaust manfold.

2. Matatizo kwenye sensors hasa zile zinazoweza kuwa na uhusiano na fuel injection. Kama upo Dar es salaam hizi naweza kukupimia na kujua kama kuna shida.

3. Matatizo kwenye actuators kama fuel injectors kuwa na shida au fuel pump kuwa na shida. Hili pia naweza kukupimia.

Karibu.
 
Matatizo ya kukosa nguvu kwa sehemu kubwa yanaweza kusababishwa na:-

1. Mechanical probles kama compression ndogo, air filter kuziba, fuel filter kuziba, Au kuziba kwa exhaust manfold..
Unapatikana wapi mkuu nikuibukie. Huwezi pitwa na bajaji halafu ukasema nami gari yangu inakimbia!!
 
Back
Top Bottom