Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Uko wapi? Taja mkoa uelekezwe kuna vizee bado vipo tangu enzi hizo samurai zinaingia uelekezwe warekebishe usipeleke kwa mafundi hawa vijana wengi ni bangi na tamaa
 
Khaa hebu google kitu kinaitwa bathtub kwenye reliability engineering unaweza kupata mawazo mapya kabisa
 
Mkuu hiyo gari ni ya zamani sana, wewe unategemea gari inaishi milele au?

Kama kila mtu akitumia gari mpaka liyeyuke kama wewe si viwanda vitakufa???
 
kuna jamaa alikuwa ana tatizi hilohilo,ishu ilikuwa ni throtle
 
nenda kacheck kwa watalaam wanaotumia computer,you will know the fault straight
 
Richman,
samurai yko inatumia magneto au point....engine yke I mean....cheki hyo kwanza....
 
pole mkuu,unaweza tu kurudi nayo mpaka dsm utakapoipeleka kwa fundi. Inawezekana inapoteza nguvu na hii inatokana na hydrolic nyingi tunazoweka hazina kiwango. Muhimu iwe haivuji na inasukuma hapo unatembea by the way ukiwa speed itakua laini na utafika
Mkuu ushauri wako niliuzingatia nimefika Dar siku ya leo mchana.
Na kama ulivyosema ukiwa speed stiffness inapungua na sasa naona kama imeisha baada ya kufika
 
Dogo. bado hujapata tu mnyalu wa kumuuzia hilo gari ? usitafute hapo kwa Msigwa. hapo town ni wajanja. sogea kule kwa Mhe. Luku vi
 
Najaribu kumwelewesha ni hivi kwenye tairi za mbele kuna vitu vinaitwa BALL JOINT sasa hizo zikichoka zinafanya usukani wa gari unakuwa mgumu, ni uzoefu maana nishakutana na hali hiyo.

Nashukuru kwa ushauri mkuu.
Nimefika Dar nitawaona mafundi waangalie ball joints
 
Richman,
Kwa suala la kuishiwa ngivu na kuzimila halafu haiwaki mpaka ikae muda, hiyo gari itakua ina overheat na chanzo kinaweza kuwa ubovu wa cooling system, yaani radiator na fan au inaweza kuwa cylinder head.

I had the same issue kwenye gari yangu baadae nikaja kugundua tatizo ilikua cylinder head (expensive to buy)

Kukurahisishia kujua kama ni cylinder head rejea historia ya hiyo gari, kama imewahi kuwa na tatizo la kukausha maji (radiator kuvuja or something) na ukaendelea kuitumia kwa mtindo wa kuongeza ongeza maji basi hiyo ni rahisi sana kuharibu cylinder head

Nipe mrejesho and will try my best to help you discovering the acrtual problem
 
nenda kacheck kwa watalaam wanaotumia computer,you will know the fault straight

Hivi Samurai nayo ina sehemu ya kuunganisha kwa computer? Nilidhani ni kwa gari za mwaka 2000+ tu.
 
Back
Top Bottom