Ukisikiliza sana Watanzania hutanunua hata baiskeli...
Ninashindwa kuelewa kabisa watu wanaegemea wapi..
Watakuambia X trail ni mbovu,
Ukija kwenye Toyota utasikia injini D4 kimeo,
Nilichogundua sisi watanzania hatupendi kubadilika...tunapenda kuwa conservative, kutishana na kuigana.....kwa mfano angalia GX 100 zilivyoingia, watu waliigana wakakimbilia huko karibu wote, Angalia ujio wa IST ,Sasa hivi ni Athletes Crown ndiyo watu wamekimbilia huko...
Point yangu ni nini..?
Hakuna gari bovu (in general conclusion)
Kwa sababu gari linapotengenezwa kiwandani linapitia standards nyingi sana za kimataifa ili kuku balike kuendesheka popote duniani...
Cha ajabu hawa Watanzania wanaosema Nissan X trail na Toyota za D4 engine ni mbovu, watanzania hawa hawa hawana hata technolojia ya kuyengeneza bulbu tu ya gari....kiwanda cha matairi kule Arusha kimewashinda kimekufa....Sijaelewa wanatoa wapi ubavu wa kuikosoa technology ya mjapan...
Ingelikuwa X trail ni mbovu kama madai ya watanzania yanavyodai, nadhani Nissan Motor Cop wangesitisha uzalishaji wa haya magari...
Lakini leo hii X trail ipo generation ya tatu...Ina maana generation ya kwanza ilifanya vizuri, wakaja na generation ya pili ikafanya vizuri, na sasa wapo generation ya tatu....
Watanzania tuna kile kitu cha sizitaki mbichi hizi...
Why x trail na Toyota D4 ni mbovu kwa wabongo tu na siyo huko duniani..?
Majibu..
1. Umasikini
hali zetu za umasikini hazikidhi sisi kumiliki hayo magari na kuyafurahia...Kipato cha kuunga unga unataka ukae ndani ya x trail au Toyota yenye d4, lazima tu utasingizia hizi gari hazifai kwa sababu huna hela za kufanya service inayokidhi viwango na spea genuine.....Mtu wa namna hii kaa kimya ndani ya starlet, carina, vitz, funcargo, corrola na nyinginezo za jamii hizo.
2. Ufundi
Nchi yetu bado ina majanga makubwa sana kwa upande wa mafundi waliobobea kwenye brands nje ya Toyota....hawa mafundi ndiyo wamekuwa wapotoshaji wakubwa kuwa Nissan, Mitsubish,Mazda,Subaru, BMW,Aud,Benzi B na Toyota zenye injini ya D4 azitengenezeki, hazina spea, spea ni ghali(hili nakubaliana nalo lakini ukifunga unasahau)
Unakuta fundi hajui kuandika jina lake vizuri anaikosoa technology ya mjapani. Watanzania wengi wamekuwa wakiishi kwa ushauri wa mafundi wa chini ya mwembe mwisho wanapotea.
3. Baadhi ya watu wanapenda kushikiwa akili zao na mafundi wao
Kwa mfano Nina Nissan ambayo ina bush flan ya wishbone...hii bush inaingiliana na kwenye Nissan March....kuna jamaa nilimkuta kwa fundi kachongesha hii bush, nikamuuliza WHy, akanijibu fundi wangu kasema spea za Nissan hazipatikani na ukipata ni ghali sana....nikambishia kwa sababu huwa ninanunua hizo bush kwa 15000/ kwa moja na zimajaa tele...jamaa yeye alishikilia msimamo wa fundi wake..The hell with him...[emoji84][emoji83][emoji48][emoji48][emoji49][emoji84][emoji84]
Kwa hiyo, tunapojadili magari fulani fulani, kagua mfuko wako, mafundi wako na aina ya service unayofanya...
Usije ukataka kuleta Service ya starlet kwenye X trail, halafu ufikiri X Trail itakuchekea...
Sent using
Jamii Forums mobile app