Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Nlichokiona wengi walioandika hawana hii gari xtrail ni ushabiki maandazi tu ndo inawasumbua....
 
Sio kweli kuna rafiki zangu 3 wote wana hizo hari na zinawatesa, waliagiza moja kwa moja japani, hakuna formula kua gari fulani ni nzuri/gari ile ni mbaya, sensor za harrier bei yake ipo juu kama gari nyingine tu, mimi namiliki nissan xtrail, jinsi ilivyonitendea haki nina mpango wa kuagiza new model nissan xtrail ni gari nzuri unless umeuziwa magumashi ambapo ni kawaida kwa gari yyte ukiingia/ukibambikiwa
Kama kutunza Harrier kuna kushinda basi achana na kukimbilia kununua gari.

Rudi kwenye bajaj au pikipiki.

Hakuna gari nyepesi kuitunza kama Harrier, kuanzia ulaji wa mafuta, spares na maintanance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kutunza Harrier kuna kushinda basi achana na kukimbilia kununua gari.

Rudi kwenye bajaj au pikipiki.

Hakuna gari nyepesi kuitunza kama Harrier, kuanzia ulaji wa mafuta, spares na maintanance.

Sent using Jamii Forums mobile app

Harrier nayo ni gari au ni mkebe wa kuuzia sura? Ungesema Rav 4 au Kluger ana VanGuard ningekuelewa.
 
Hakuna kampuni inayotengeneza gari isiyofaa na ikaendelea kuuza miaka yote.

Changamoto unayokutana nayo wewe sio wote.
 
kwa jinsi ilivyonitesa Nissan pressea , niliyachukia magari yote ya Nissan, drive shaft unatafuta mji mzima ukija kupata bei mara karibu nne ya toyota na bado kwenye kufunga spea inataka modification,

Nissan waachiwe wenye pesa zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kampuni inayotengeneza gari isiyofaa na ikaendelea kuuza miaka yote.

Changamoto unayokutana nayo wewe sio wote.
Majority ya gari za nissan zinasumbua , Angalia Navara saa hii ziko wapi halafu linaganisha na hilux, ya mwaka sawa na hiyo Navara , jiulize hata serikalini Nissan patrol hazitumiki sana ukilinganisha na land cruiser ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majority ya gari za nissan zinasumbua , Angalia Navara saa hii ziko wapi halafu linaganisha na hilux, ya mwaka sawa na hiyo Navara , jiulize hata serikalini Nissan patrol hazitumiki sana ukilinganisha na land cruiser ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mmh kwenye Nissan Patrol, naweza kukataa kidogo. Hazisumbui kabisa hizi gari. Naongelea experience.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu za Brand za magari kama NISSAN, MITSUBISHI na Zinginezo kuonekana ni tatizo.

Utalamu wa mafundi wetu na kujua mahitaji ya magari husika upo chini. Haya magari hayataki mafundi ambao ukimpelekea gari anaanza kupiga ramli kujua tatizo linaanzia wapi.

Anaanza kusearch kichwani mwake kwa kutumia akili yake binafsi na sio utaalamu wa kujua mfumo wa gari husika. Hizi gari kwa miaka mingi zimetibiwa magonjwa yake kwa kufanyiwa modification na sio kuadress shida kuu.

Mfano kama mimi niliwahi kuhangaika na Mitsubishi Pajero IO zile ndogo. Kila unapokwenda gereji kila fundi anakuja na ugonjwa wake, ikafikia m'moja akasema kwa gari hiyo nitoe hiyo engine niweke ya Noah, of which ni modification inayowezekana but sikuwa comfortable. So nikapunguza nayo matumizi nikisubiria suluhu hadi nilipowasiliana na jamaa kutoka Japan na akanieleza why hizo gari zikifika nchi za dunia ya tatu kama india na African zinakuwa zinazingua.....

Akasema gari ni system.... Na system huwa inakuwa na standard requirements. Na zisipokuwa met basi hiyo gari itaanza leta shida. Akanishauri gari nipate fundi mwenye diagnosis machine, ambayo itaelezea shida gani kwenye mfumo automatically kupitia computer chip iliyo katika gari.

Kwa mfano, kwa hii gari, kwenye mfumo wake wa engine inataka sana mafuta ya premium level. Yaani mafuta ya zile Petrol stations kama Puma, Victoria, Engine, Total na wengineo ambayo hayo mafuta huwa yanasaidia katika uchomaji kwenye engine na kuipa nguvu inayotaka.... Badala ya kuweka haya ya ordinary kama ya Camel, oilcom, na kwengineko.

Kimsingi gari kupitia mfumo wake ikiditect kuna shida kwenye mfumo wake automatically inatengeneza fault ili kuzuia madhara yasisambae..... Sasa kwa mbongo wa kawaida akiona gari limejizima tu anasema hizi gari ni mbovu, anapeleka kwa fundi ambaye hazijui anafanya kuotea tu tatizo na mwisho wa siku akiifungua kuna vitu harudishii sawa au anavidisturb kwakusema hiki tukitoe maana ndicho kinazuia gari isirespond kuwaka. Kumbe unatoa kitu ambacho ni muhimu katika kutoa taarifa fulani kwenye sytem ya gari. Sometimes unakuta ni sensors tu zimefeli na inatakiwa kipatikane kile kifaa cha diagnostic kitoe jibu la fasta bila kuhangaika kupiga ramli.

So kwa ushauri wangu ukiwa na magari kama, Nissan Xtrail, Nissan Navara, Pajero zote ndogo na kubwa, Ford, Descovery, BMW, Mercedes, Volkswagen, na kadhalika wewe nenda kwa fundi ambae atafanya diagnosis kupitia kifaa na sio ramli ya kichwa watakuharibia gari na kukuaminisha gari ni mbovu kumbe ni wabovu kwenye kudeal na technology ya magari ya kisasa ambayo mifumo yao inakuwa inarespond pale ikiharibiwa.....


Kuna magari ukishaanza kuyaweka mafuta ambayo sio premium utaona linaanza kusumbua kuwaka kumbe system imeshadetect mafuta ya kuchakachua na hivyo inatuma warning signal gari isiendelee kutumika itauwa fuel pump..... So kuweni makini sana na maswala ya modification....

Na kuhusu spear.... Spear zilikuwa ni shida kupata zamani before internet haijawa kila kitu..... Ila kwasasa hiyo shida hakuna tena.... Internet imerahisisha mambo, kwasasa unaweza kufanya manunuzi ya spare kwa kuweka to Serial namba ya spear ya gari yako mzigo ukaletwa ukakufikia na unapata kitu genuine.... Shida ni kwamba wabongo ni waoga wa maisha na tunaishi kwa mazoea.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo BIAFRA hao mafundi wanastahili TUZO aisee mm maji ya rejeta yanaisha haraka yaani ukitoka hom mwenge kufika posta mjini hamna maji. nikapeleka kwa makanjanja mwenge chini ya mwembe/karibu na tamal hotel full sanaa wanakula pesa gari haiponi, nilienda kuchukua RB nikamuweka ndani kisha nikaenda pale biafra jamaa katumia 30 mins. shida kwisha. *****.... Biafra noma...
Boss nisaidie namba ya huyo fundi, maana na mimi nina suzuki yangu ina shida hiyo hiyo yanii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uongo umezidisha khaaa

Mbona spare za kumwaga tu, ww kama umenogewa na hiyo miyeboyebo ya toyota endelea tu ila usianzishe story za uongo
We rafiki yako anatumia mimi ninayo hapa nimeagiza Nagoya Japan mwaka Jana nimeshafanya service mara mbili huo ndio ukweli huwezi fananisha hiyo Nissan yako na Toyota Harrier spea zimejaa kariakoo gerezani na Machinga Karume we mpaka ukope pesa uagize spea Nairobi au DubaiView attachment 1445003

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mimi natumia X trail 2010 na haina shida mpaka sasa, nadhani ni utunzaji wako binafsi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaezekana unatumia nguvu na pesa nyingi sana kuitunza hiyo x trail., Tunaposema gari flani ni mbovu sio kwamba hazitengenezeki , Bali Kuna kiwango flani kikipita kwa ajili ya maintenance ,gari inakuwa declared Kama Ni sumbufu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikiliza sana Watanzania hutanunua hata baiskeli...

Ninashindwa kuelewa kabisa watu wanaegemea wapi..

Watakuambia X trail ni mbovu,

Ukija kwenye Toyota utasikia injini D4 kimeo,

Nilichogundua sisi watanzania hatupendi kubadilika...tunapenda kuwa conservative, kutishana na kuigana.....kwa mfano angalia GX 100 zilivyoingia, watu waliigana wakakimbilia huko karibu wote, Angalia ujio wa IST ,Sasa hivi ni Athletes Crown ndiyo watu wamekimbilia huko...

Point yangu ni nini..?
Hakuna gari bovu (in general conclusion)
Kwa sababu gari linapotengenezwa kiwandani linapitia standards nyingi sana za kimataifa ili kuku balike kuendesheka popote duniani...

Cha ajabu hawa Watanzania wanaosema Nissan X trail na Toyota za D4 engine ni mbovu, watanzania hawa hawa hawana hata technolojia ya kuyengeneza bulbu tu ya gari....kiwanda cha matairi kule Arusha kimewashinda kimekufa....Sijaelewa wanatoa wapi ubavu wa kuikosoa technology ya mjapan...

Ingelikuwa X trail ni mbovu kama madai ya watanzania yanavyodai, nadhani Nissan Motor Cop wangesitisha uzalishaji wa haya magari...

Lakini leo hii X trail ipo generation ya tatu...Ina maana generation ya kwanza ilifanya vizuri, wakaja na generation ya pili ikafanya vizuri, na sasa wapo generation ya tatu....

Watanzania tuna kile kitu cha sizitaki mbichi hizi...

Why x trail na Toyota D4 ni mbovu kwa wabongo tu na siyo huko duniani..?

Majibu..
1. Umasikini

hali zetu za umasikini hazikidhi sisi kumiliki hayo magari na kuyafurahia...Kipato cha kuunga unga unataka ukae ndani ya x trail au Toyota yenye d4, lazima tu utasingizia hizi gari hazifai kwa sababu huna hela za kufanya service inayokidhi viwango na spea genuine.....Mtu wa namna hii kaa kimya ndani ya starlet, carina, vitz, funcargo, corrola na nyinginezo za jamii hizo.

2. Ufundi
Nchi yetu bado ina majanga makubwa sana kwa upande wa mafundi waliobobea kwenye brands nje ya Toyota....hawa mafundi ndiyo wamekuwa wapotoshaji wakubwa kuwa Nissan, Mitsubish,Mazda,Subaru, BMW,Aud,Benzi B na Toyota zenye injini ya D4 azitengenezeki, hazina spea, spea ni ghali(hili nakubaliana nalo lakini ukifunga unasahau)
Unakuta fundi hajui kuandika jina lake vizuri anaikosoa technology ya mjapani. Watanzania wengi wamekuwa wakiishi kwa ushauri wa mafundi wa chini ya mwembe mwisho wanapotea.

3. Baadhi ya watu wanapenda kushikiwa akili zao na mafundi wao
Kwa mfano Nina Nissan ambayo ina bush flan ya wishbone...hii bush inaingiliana na kwenye Nissan March....kuna jamaa nilimkuta kwa fundi kachongesha hii bush, nikamuuliza WHy, akanijibu fundi wangu kasema spea za Nissan hazipatikani na ukipata ni ghali sana....nikambishia kwa sababu huwa ninanunua hizo bush kwa 15000/ kwa moja na zimajaa tele...jamaa yeye alishikilia msimamo wa fundi wake..The hell with him...[emoji84][emoji83][emoji48][emoji48][emoji49][emoji84][emoji84]

Kwa hiyo, tunapojadili magari fulani fulani, kagua mfuko wako, mafundi wako na aina ya service unayofanya...

Usije ukataka kuleta Service ya starlet kwenye X trail, halafu ufikiri X Trail itakuchekea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom