Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Nissan zinahitaji discipline ya matumizi sana....hii ikijumuisha uendeshaje wako na mengineyo. ikiwemo na spea..! nina Nissan Note, ila service yake na shughuli....gear box oil..NS2 ni laki tatu na upuuuzi....heheeeee
 
Nakubaliana na wewe mkuu haziko vizuri,hata nje wameshusha sana bei ili zitoke ndiyo maana watu wengi wananunua pasipo kujua kuwa ni bei promo..

Ni kweli, xtrail haziko reliable kabisa kama Toyota. Inaweza kukuharibikia ghafla ukashindwa kujua cha kufanya, na spea zake ni chache sababu nyingi haziingiliani na gari nyingine.

Kimeo kingine ni Nissan Murano. Kama umeshafanya utafiti kidogo wa bei zake kwenye used, zimeshuka saana, sasa hivi ni affordable kwa watu wengi. Ila haziko reliable hasa kwa barabara zetu na mafundi wetu
 
In general, Nissan zote hazitaki pesa za mawazo, whether iwe Nissan Diesel (UD), Civilian, March, X Trail au Condor. Ni kama ilivyo Benz ama BMW.
 
Kwa ujumla gari isiyo manual ni tatizo. Ni kweli vipuli vya Nissan ni vya ghari sana but kama ni manual utaendesha hadi uchoke. Mimi ninayo double cabin ( Nissan YD) tena ya under licence kutoka SA , huu ni mwaka wa Tatu haijawahi haribika hata kidogo.
 
nissan zinahitaji discipline ya matumizi sana....hii ikijumuisha uendeshaje wako na mengineyo...ikiwemo na spea..! nina nissan note, ila service yake nia shughuli....gear box oil..NS2 ni laki tatu na upuuuzi....heheeeee

Si mchezo dah
 
Xtrail haichelewi kukuzimikia mazima barabarani
 
Kwa ujumla gari isiyo manual ni tatizo. Ni kweli vipuli vya Nissan ni vya ghari sana but kama ni manual utaendesha hadi uchoke. Mimi ninayo double cabin ( Nissan YD) tena ya under licence kutoka SA , huu ni mwaka wa Tatu haijawahi haribika hata kidogo.

Unaweza kutupa sababu za msingi??
 
Nimesoma huu Uzi naona kila mmoja anatoa story asieijua. Kwa taarifa yenu hakuna Gari nzuri kama Nissan xtrail. Nimekaa nayo five years, Nina ndugu zangu wanne hazijasumbua.

Kuhusu AC zipo vzr sana kama gx 110 spear so ghali kama watu wanavyotaka kutuaminisha no za kawaida sana. Engine complete used 700 laki sijui kwa mini watu wanapotosha. Kwa safari nni Gari nzuri sana.

Ulaji was Mafuta in mzuri ukilinganishana na SUV nyingine ambazo ni 4WD. Ukitaka detail ya kila spear na being uliza sio kukurupuka na kudanganya umma. Ukiwa na RAV4 kwa mwaka garana za service na Mafuta no kubwa kuliko Xtrail, ninao ushahidi kwa hili

Kuagiza extrail no cheap kuliko RAV4 lakini ushuru was Xtrail no mkubwa kuliko rav4 n.k
 
kuna work mate wangu, alipata nayo ajali, hapo ndipo nilijua kuwa xtrail siyo gari ni jini la kuleta umaskini. yaani taa moja kubwa 350,000 ndogo 150,000 kwa taa 4 ni 2,000,000. yaani jumla ya cost ilikuwa milion 7 na point.
 
Back
Top Bottom