Kwa upande wa Yamaha crux ni pikipiki nzuri sana.
1. Inakula wese vizuri tu lt1 unaenda mpka 55km hadi 60km kutegemea na uendeshaji wako.
2. Ina kamlio flani amazing kama kamluzi hivi, kapo kwenye yamaha nyingi (huwa nakafurahia).
3. Sio yeboyebo kama mchina, zipo chache.
4. Service ni kawaida tu, mie natumiaga total oil 8000/= na 500/= au 1000/= ya fundi kumwaga oil. Service huwa nafanya kila mwezi, pikipiki ni binafsi halafu haina mizunguko zaidi ya mishe zangu na nyumbani tu.
Changamoto nlizokuwa napata ni pamoja na;
1. Upatikanaji wa vifaa (sio kila duka waweza pata spea).
2. Brake zake sio strong kivile sababu ni drum especially ya mbele halafu utaudjust sana hizo break ili zibaki na ile grip unayoitaka.
3. Tairi zake ni nyembamba zinataka lami tu kwa hiyo ukipita sehemu yenye kamchanga kuwa makini sana sana sana sanaaa..... yaani kwa lugha nyingine ukiona mchanga punguzu mwendo mapema sana kabla hujawa maarufu mbele ya umati wa watu kwa mfano anapopita SanlG,Fekon n.k kama kuna mchanga unaopitika vizuri tu, ukiwa na yamaha crux unaweza kukutupa chini.
Vilevile tairi zake ni za tube kwa hiyo ukipiga msumari haina cha kusubiri ndani ya dk moja upepo kushnei, sali sana sehemu ya mafundi iwe karibu.
4. Kana gia 4 tu kwa hiyo kanadai sana gia.
5. Ngoma ni kick to start only.
Mbali na hizo changamoto naikubali sana.