MJADALA: Je, unapendekeza Serikali na Sekta Binafsi zifanye nini cha tofauti ili kuondoa tatizo la ajira nchini?



Hakuna
 
Mada kama hizi huwezi kukuta wana jf wanachangia sana, inaonyesha kabisa watz wana vipaumbele gani

Mzee mzima Dr Restart yupo uzi wa kula tunda kimasihara huu anafanya hajauona
Acha ubogus.

Nilikuwa live X. Na nilipata nafasi ya kuchangia. Baadae space ikashuka.

Sikujoin tena.

Tatizo unadhani wote marue rue kama wewe.
 
Kilimo biashara, kwa maoni yangu na ujuzi mdogo nilioupata katika biashara ya mazao, nimetambua kuwa kilimo kinalipa isipokuwa miundombinu ya kilimo ndiyo siyo rafiki. Wakulima wetu hawathaminiwi ili hali ndiyo wanaolisha taifa, sababu ya kutokuthaminiwa kwa wakulima kunafanya hata vijana wasio na ajira waone ukulima ni sawa na kazi ya kimaskini.

Hali hii imejenga dhana kiasi kwamba hata mkulima mwenyewe haoni sababu yoyote ya kumridhisha mwanae kazi ya kilimo. Hii pia imechangiwa na ukosefu wa elimu juu ya kilimo.

Ukosefu wa mtaji katika kilimo pia ni tatizo. Linalofanya vijana wengi washindwe kuingia katika kilimo (kilimo kinahitaji mtu ambaye tayari yupo stable kiuchumi, ama ana biashara nyingine inayomuingizia kipato)
Tanzania tumezungukwa na mataifa ambayo kama tungewekeza katika kilimo, nina uhakika vijana wengi kusingekuwa tunalalamika juu ya ukosefu wa ajira.

Malawi ukame, Zambia hawana ndizi tamu kama za Tukuyu, kiasi kwamba ukipeleka ndizi uhakika wa soko upo changamoto nyingine ni mlolongo wa vibali, rushwa na kodi pamoja na utitiri wa ushuru. Hizi changamoto zinakatisha tamaa.
 
Nendeni Kilindi Tanga mkawekeze viwanda vya kusindika mazao mengi kule ikiwemo matunda.
 
Masoko ya uhakika yanayotoa thamani halisi ya jasho la mzalishaji husika.

Na pia muangalie watu wasipate togauti na thamani wanayoileta kwa Taifa. Mfano kumpatia mtu fulani (mwanasiasa/muajiriwa whatever) posho iliyozidi thamani anayoitoa kwa jamii nao ni UTAKATISHAJI FEDHA na UHUJUMU.

Kila mtu alipwe kwa haki thamani halisi ya kazi yake, hapo ndio uchumi utatengemaa
 
Nasikitika hii kitu nimeikosa kwanini JF hamkuiweka hewani mapema watu tushiriki!
 
Tubadili mfumo wetu wa Elimu, uendana na dunia ilipo, hii ndilo jambo la kwanza ili Kwanza tuzarishe skilled work force, tuhakikishe kila taaluma inaendana na wakati tuliopo.

Elimu ya form five na six ifutwe na baadala yake vijana wetu akimaliza form four waende college moja kwa moja miaka 3, kama mwanasheria akapate diploma ya Sheria, kama mhasibu akapate diploma ya uhasibu, kama ni engineer akapate diploma ya engineering, kama mwalimu basi akapate diploma ya ualimu nk.
Watakaofaulu hapo ndio waendelee na Elimu ya juu Kwa maana ya degree.

Hapo kwenye diploma, engineering and technology iwe ni special case, na wanaohitimu kwenye ufaulu wa kawaida kwenye engineering and technology wapewe scholarship wakasome short courses za mwaka mmoja mmoja kwenye area ambazo tutazifocus kwenye nchi kama China, Korea, Ujerumani na USA, tujitahidi walau kila mwaka waende vijana kama 300 kwenye program ya miaka hata 20.

Hii skilled workforce ikishakuwa kubwa maana yake vijana watajikita kwenye production zaidi na sio uchuuzi, maana yake pia watatoa ajira nyingi Kwa wenzao mitaani na kuongeza exportation ya bidhaa za mikono na kuacha kutegemea China, India, Pakistani nk.

Skilled workforce inayoendana na technolojia ya kisasa ikishakuwa kubwa maana yake pia wengi watakuwa na uwezo wa kwenda kujitafutia kazi huku na kule duniani.

JWTZ lianzishe production industries kwa ajili ya kutengeneza silaha kama bunduki, tanks, simple military vehicles, artillery, patrol boats, matractors, power tillers nk, kupitia hii program yakudevoloped skilled workforce kubwa maana yake JWTZ itabidi iajili vijana wengi Kwa ajili ya kurun hivi viwanda na kuexport silaha na nyingine zibaki kwa matumizi ya ndani.

JWTZ ianzishe mashamba makubwa ya kilimo cha kisasa, hapa vijana wengi skilled kwenye kilimo na mitambo watapata ajira na Taifa litazarisha chakula kingi ambacho tutauza nje na kingine kubaki kwenye akiba yetu.

Kupitia zana za kilimo zitakazozalishwa na JWTZ kama nilivyoonyesha juu hapo maana yake wakulima wetu nao watanufaika na kuachana na kilimo cha kizamani na uzarishaji wa chakula utakuwa mkubwa sana.

Serikali sasa, itoe kipaumbele hata Kwa kuweka hela kwenye madini ya chuma pale Liganga, tukichimba chuma na kuwa na chuma maana yake sasa hii skilled workforce tutakayokuwa nayo mitaani itajikita kwenye uzarishaji rahisi wa bidhaa za vyuma, maana yake gharama za uzarishaji zitakuwa chini maana chuma kipo hapa, bidhaa nyingi zitazarishwa na hawa vijana na kuuza nje, ajira nyingi zitatengenezwa na serikali itaingiza pesa nyingi kupitia exportation ya hizi bidhaa za chuma.

Ukishakuwa na Chuma na Gharama za umeme ukashusha Kwasababu tutakuwa automatically na Stieggler maana yake hawa vijana wengi tutakaokua nao ambao ni skilled watakuwa na uwezo wa kucompete kwenye world market Kwa kuzarisha cheap products.

Mwisho kabisa serikali iachane na mentality ya kukusanya kodi tu kwenye uchuuzi unaofanywa na watu wake, ijikite kutumia population ya vijana na watu wengi wenye nguvu kufanya uzarishaji (kuzarisha bidhaa) kupitia viwanda vidogovidogo, hili linawezekana kwa kuweka miundombinu sahihi kama kuwa na mfumo mzuri wa elimu utakaozarisha skilled workforce, kulifanya jeshi JWTZ kuwa more productive na kuajili hawa skilled workforce, kuhakikisha gharama za usarishaji zinakuwa chini Kwa kuweka nguvu kwenye uzarishaji wa chuma, umeme na maji vya kutosha.
 
Kilimo na masoko ya uhakika,kila mara wakulima wakiweka nguvu kwenye zao flani mwaka huo bei inakuwa mbovu. Parachichi zinaoza hovyo wakati soko halijulikani. Uchumi wa uvuvi uzinagtiwe na ulete tija.

Vijengwe vitaru vya kuzalisha sato ndani ya mazingira ya asili kama kule Lamadi na kwingineko.
Kilimo cha mbao ngumu kiimarishwe na kuboresha muda wa uvunaji

Gesi ichakatwe ili iuzwe kwa bei nafuu na lolipelekwe kwenye uzalishaji wa mbolea kuepusha uagizaji nje
Fitna zipungue na husda kwa wenye nia ya kuimarisha uchumi.

Tuwekeza kwenye zao la mahindi kwa wingi nchi jirani zote ni soko mpaka sudani kusini na visiwani shelisheli
Natamani kuona tunazalisha Michele supa na kuupeleka Canada

Ngano izalishwe kwa wingi na bidhaa zake ziwe za kutosha kuepusha kuagiza nje,pia mapato ya makaa ya mawe tujue tija yake.Serikali isijenge Barabara kwa Kasi kuliko kuwekeza kwa watu.

Tuangalie.pia kupunguza ugonjwa wa kamati na afya ya akili.watu wanacheza sana kamali.
 
1. Kuondoa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kwny ofisin za umma!
Kuna viongozi wengine ambao wamefunga Fursa za vijana kwny ofisi za UMMA mfano mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa idara muhimu Kwa mfano NSSF ,PSSSF, Wakuu wa Vyuo vikuu nchini,idara ya Sensa na Makazi.Itungwe sheria ambayo itawapa vijana Fursa ya kutoa mchango wao Kwa taifa lao na pia Fursa ya kugawana keki ya taifa Kwa usawa. Ikumbukwe Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere amekuwa Waziri wa Tanganyika na Baadae Rais wa Tanganyika akiwa na miaka 39 na 40 mtawalia Kwa hivyo msiseme vijana hawana uwezo Wala uzoefu.

2. Benki na Taasisi za fedha ziwekewe mazingira wezeshi ya kufanya kazi na vijana.
Ukweli ni kwamba vijana ndio kundi kubwa ndani ya jamii na nchi Kwa hivyo tunapopanga maswala ya fedha lazima kipaumbele Cha kwanza ni kuwafikia walio wengi na kundi Hilo ni vijana! Nini kifanyike?! Sheria,Kanuni, Taratibu,Sera na miongozo itolewe Kwa Benki na Taasisi za fedha nchini kabla ya kupewa fedha za mikopo inayolenga kukuza uchumi na uwekezaji nchini.

Hapa lazima tuwatungie sheria ngumu na zenye adhabu Kali Kwa kukiuka masharti Kwa mfano mkopo maalumu utolewe Kwa vijana(watu) wenye umri kati ya miaka 18-45 na ambao sio watumishi wa UMMA na mkopo huo uwe na riba ndogo na kuwe na taasi maalumu ya kufatilia wanufaika ikiwemo kuwapa ushauri,elimu na uzoefu katika uwekezaji waliopanga.Mikopo yote iwe na bima na pia biashara za hao vijana ziwekewe bima ili kuwasaidia wanapopata misukosuko.Hii itafanya Benki nyingi zifanye kazi na vijana wasiokuwa na ajira rasmi kama watumishi wa UMMA ambao Kwa idadi Yao hawaongezi Pato jipya Kwa taifa zaidi ya kunufaisha mabenki tu.

3. Tuwekeze kwenye ujuzi na sio taaluma tu Kwa vijana wetu wakiwa bado wadogo kabisa.
Hapa maana yangu ni kwamba vijana waandaliwe kuwajibika au kuingia kwenye soko la ajira na kujiajiri wakiwa bado wadogo Kwa mfano kila wilaya na ikiwezekana kila kata iwe na Centre za Serikali Kwa ajili ya kuwapa vijana ujuzi mara tu wanapohitimu hatua Fulani ya elimu kuanzia darasa la saba Hadi chuo kikuu na elimu hii iwe na mwendelezo Yani tuwe na mhitimu wa darasa la saba anaeweza kushona nguo kwny chereani na tuwe na mhitimu wa degree anaeweza kujenga nyumba na sio mhandisi wa ujenzi! Ule mwaka mmoja anaposubiri matokeo ndio mahala pake kijana asikae kizembe nyumbani baada ya kuhitimu. Na elimu hii itolewe Kwa lazima na bila malipo.

Hii itasaidia sana vijana wa kitanzania kujiajiri wenyewe wakiwa bado wadogo na kuzalisha bidhaa nyingi ambazo tutazitumia ndani na nje ya nchi na kudhibiti uagizaji holela wa bidhaa za nje ambazo tunaweza kuzalisha nchini! Kwa hapa Serikali Kwa kushirikiana wadau wa maendeleo Wana wajibu wa kutekeleza.

4. Kufuta nafasi za viti maalum bungeni hii fedha ipelekwe Kwenye mfuko maalumu wa kushughulikia matatizo ya ajira Kwa vijana.

Hapa najua nitagusa wenye mamlaka na hawapendi lakini ukweli ni kwamba mtoto wa kike anachopaswa kupewa Kwa sasa ni Fursa ya pekee kwenye elimu na sio mpaka kuingizwa bungeni kama ilivyo Sasa.Hivi ni nani Sasa hivi atamchagua mbunge mjinga sio kielimu ila Kwa utambuzi wa matatizo ya jamii na suluhisho mbadala Kwa kigezo tu eti ni mwanaume na amwache nwanamke shupavu labda iwe ni Kwa njia ya rushwa tuu. Kwa hivyo pesa hizi zitafungua Fursa nyingi kwa vijana kuliko hizo nafasi mia na kadhaa zinazotumia pesa nyingi bila mafinikio sawia. Ni ukweli mchungu lakini lazima tukubaliane nao.Dada zangu wabunge mlioingia Kwa njia hii naomba mnisamehe lakini na nyie muwe na huruma Kwa vijana wenzenu.

5. Kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani na kuteka soko la nje.
Hapa Waziri wa fedha, Waziri wa kilimo na Uvuvi,Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Waziri wa Biashara, Waziri wa Ajira, kazi na maendeleo ya vijana,Waziri wa Elimu na Ufundi na Elimu ya juu,Waheshimiwa mabalozi,Vyuo vya Ufundi,Taasisi za fedha, lazima muwe na dirisha la pamoja shirikishi Kwa ajili ya uanzishwaji wa Viwanda vipya,ufufuaji wa Viwanda vya zamani ili kuzalisha bidhaa nyingi ndani ya nchi na zenye ubora wa kitaifa na kimataifa huku mabalozi wakitutafutia masoko nje ya nchi.Hatua hii inapaswa ifuatwe baada ya kufanikisha hoja yangu ya Tatu hapo juu.

HITIMISHO
Hizo ni hatua chache tuu ambazo nimezianisha lakini zipo nyingi sana na Kwa uwezo wa Mungu nitaandaa andiko maalumu ambalo nikikamilisha ntakabidhi mamlaka za juu za Serikali ili wazichambue waone wapi pa kuanzia na Ikiwa dira ya maendeleo haijagusa haya mambo bado tunaendelea na tatizo hili Kwa kiwango Cha juu zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…