jockey emmanuel
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 330
- 50
...ha ha ha, changia biblia au msahafu. Waambie huo ndio uwezo wako!
Issshhh....eti utanufaika na mkewe, he he he!
Badili namba ya simu.
Jamani maisha kusaidiana acheni kuponda michango ya harusi
Mkuu mwenye harusi yake amekuomba umchangia halafu unampelekea msahafu au biblia na kumwambia huu ndio mchangu wangu atakuelewa kweli!? "Yule jamaa hovyo sana ni bora hata angeniambia hana uwezo wa kuchangia kuliko kuniletea msahafu/biblia na kuniambia eti ndio mchango wake." Hizi ndizo zitakuwa story za kumuumbua mchangiaji huyo.Lakini maisha ni ndoa na si harusi.
asiyekubali achana naye mapema. Baadaye atakuwa matatizoHivi wadada wakiambiwa tufanye harusi ndogo tu watakubali?
ndoa zisizo usumbufu wa kulazimisha michango ndio zenye baraka!
mijitu haielewi
tubadilike, tuanze kuchangia elimu na maendele.
Pia tuchangie wenzetu wenye mahitaji ya tiba na afya, tuachane na ujinga wa harusi za kifahari
mkuu mm ndo kabisa yaani urafiki unataka kufa kabisaHawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.
Hata sielewi,,
Nlipenda ya jamaa mmoja alioa juzi, yeye aliita marafiki zake zaid kama 9, akawaeleza ili waweze kumsaidia majukumu mengine. Lakin marafiki wale wakataka japo nao wamchangie hata kidogo wakatoa michango yao, mwisho jamaa kamalizia na wengine wakaalikwa ukumbini.
Ss wengine budget 8-10m, akiulizwa bwana harusi unakiasi gani umeandaa 1m, yaani hizo 7 zote ndo wachangiaj mhhhhhh.
Ndo maana ndoa cku hizi fashion..