Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

kwan lazma kuchangia?au ucpochanga unanyimwa kad?na ukinyimwa kad unapungukiwa na nini?...i think kama kipato hakitosh ucji4c kuchanga ili kwenye ndoa yako wakuchangie....wapo wengine watakaOKUCHANGIA NDG....LOH!MICHANGO ICKUMALIZIE MSHAHARA BABU WE...HAD UKOSE CHAKULA...
 
...ha ha ha, changia biblia au msahafu. Waambie huo ndio uwezo wako!
Issshhh....eti utanufaika na mkewe, he he he!

Mkuu mwenye harusi yake amekuomba umchangia halafu unampelekea msahafu au biblia na kumwambia huu ndio mchangu wangu atakuelewa kweli!? "Yule jamaa hovyo sana ni bora hata angeniambia hana uwezo wa kuchangia kuliko kuniletea msahafu/biblia na kuniambia eti ndio mchango wake." Hizi ndizo zitakuwa story za kumuumbua mchangiaji huyo.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mkuu mwenye harusi yake amekuomba umchangia halafu unampelekea msahafu au biblia na kumwambia huu ndio mchangu wangu atakuelewa kweli!? "Yule jamaa hovyo sana ni bora hata angeniambia hana uwezo wa kuchangia kuliko kuniletea msahafu/biblia na kuniambia eti ndio mchango wake." Hizi ndizo zitakuwa story za kumuumbua mchangiaji huyo.
Lakini maisha ni ndoa na si harusi.

...naam, ndio maana 'ukiwatunuku' kitabu cha ibada kiwe ni mwongozo wa maisha yao itakuwa ni heri kuliko kuwapa pesa.
 
mimi napenda sana kuchangia ila sina ndugu wengi na marafiki wanaooa. kwa nini hapa JF hilo kapu huwa halipitagi?
 
hizi ni dalili za UBINAFSI,
hawa hawa ndo tukiwapa madaraka yanajilimbikizia mali,
na kuiba bila haibu!
ndani ya jamii watu husaidiana kadri ya uwezo!
unaliona hilo tu, kesho mfano unafiwa watu tukasema,
tumechoka kuudhuria misiba, itakuaje: michango ya harusi ni sehemu moja tu
ya kusaidiana ndani ya jamii! siyo lazima umfahidi mke wa mwenzio!
siyo vema wakati wewe tukikuchangia, au unafikiri tumesahau??:madgrin::madgrin:
 
He hata wewe KIRANJA MKUU. kumbuka mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba. :shut-mouth:
 
Mkuu kwakweli hili limekua ni tatizo sasa manake kadi haziishi kila kukicha.minafikiri dawa ni kuwa wazi tu kuliko kutoa huku unaumia.Kama budget yako ya kuchangia haipo its better kuwa wazi kuna mambo mengine ya msingi ya kusaidia kuliko just harusi.Kuna watu wamesha starabika siku hizi anaandaa kila kitu then anawaita tu kuja kusheherekea pamoja na inakua na maana zaidi sio sherehe kwake huku anaacha msiba
 
Hakuna michango inayonikera kama ya mtu ambae anataka kumuoa mke wake na wana watoto wawili tayari, kisingizio utasikia nataka kubaliki ndoa upumbavu mtupu.
Mimi siku hizi nachangia elimu na maendeleo, mfano kuna dimbwi lilikuwa linatusumbuwa hapa mtaani nimechangia shillingi 50,000/= za kununulia kifusi leo magari yanapita bila shida.
 
tubadilike, tuanze kuchangia elimu na maendele.
Pia tuchangie wenzetu wenye mahitaji ya tiba na afya, tuachane na ujinga wa harusi za kifahari
 
tubadilike, tuanze kuchangia elimu na maendele.
Pia tuchangie wenzetu wenye mahitaji ya tiba na afya, tuachane na ujinga wa harusi za kifahari

Nina balance ya 200,000/= nadaiwa ni school fees ya mtoto wangu kwenye moja ya hizi shule zenye majina ya watakatifu, sasa atokee mpuuzi tu na proposal za harusi unadhani nitamuelewa? mimi nashauri kwa wale ambao home town zao sio mbali na Dr es salaam ni bora wakafungie hizi ndoa zao kwenye vijiji vya asili zao.
 
Hawa waoaji na wanaoolewa hata ukiwaambia huna hela wanaendelea kukusumbua.
Urafiki unageuka kuwa uadui, kipato changu chenyewe ni kidogo hakinitoshelezi, halafu jitu linatoka huko linaniambia nilichangie, as if na mimi ntakuwa nanufaika usiku na huyo mkewe.
Nimechoka na maombi yenu ya michango ya fedha kwa ajili ya harusi.
mkuu mm ndo kabisa yaani urafiki unataka kufa kabisa
 
Hata sielewi,,

Nlipenda ya jamaa mmoja alioa juzi, yeye aliita marafiki zake zaid kama 9, akawaeleza ili waweze kumsaidia majukumu mengine. Lakin marafiki wale wakataka japo nao wamchangie hata kidogo wakatoa michango yao, mwisho jamaa kamalizia na wengine wakaalikwa ukumbini.

Ss wengine budget 8-10m, akiulizwa bwana harusi unakiasi gani umeandaa 1m, yaani hizo 7 zote ndo wachangiaj mhhhhhh.

Ndo maana ndoa cku hizi fashion..

bora huyo, rafiki yangu alituita kwenye kikao cha kaka yake anaoa, mkaka akaulizwa una shs ngapi akasema laki 5 lakini wanapenda harusi iwe ya 10 mil, mkaka mwenyewe anapasha kiporo, wanaishi pa1 na wana mtoto wa 8yrs, hiyo 9.5 mil ni nguvu ya kamati,halafu mnapangiwa kabisa mchango wa mwana kamati mr/mrs 200, cngle 150....nilikomea hapo michango, cku hizi nikiambiwa hayo mambo nawazungusha mpaka wanakata tamaa.
 
Back
Top Bottom