Hivi kuamua kuacha kuchangia harusi mpaka utambie nasi, si uamue mwenyewe! Serikali itatoza vipi kodi mara mbili wakati kila supplier amekwisha lipa kodi kwa bidhaa anayopeleka kwenye sherehe?
Lazima kwanza uelewe maana ya hizo sherehe hasa send off na reception. Hivi umelazimishwa?
Yakwangu sikuhitaji mchango wa mtu, hii naisema sababu ya uzoefu, Mwanamayu, unataka kusema ndugu zako wako katika hali nzuri sana, mpaka uwe sehemu ya kushuhudia matumizi mabaya ya pesa kwa siku moja tuu?
huna ndugu wanaolia kwa kukosa mkopo wewe, saidia na changia mambo ya lazima, kataa huu ujima wa kuchangishana mambo ya anasa.
Kubali kuonekana mbinafsi, ishi bila stress, na ishi maisha yako kwa furaha bila bugudha ya wataka michango, fikiria kupita pale jeshi la wokovu na kusaidia wale watoto pale ama sehemu nyingine zenye watu wenye uhitaji.
Amini Mungu atakubariki utakapowasaidia wenye shida kuliko haya matumizi ya kufuru.
Mawazo Mengine bwana! Sasa wewe mbona hukuacha kufunga harusi yako, hizo pesa ukawapa watu wanaotaka mikopo.. Au ukulijua hilo. THINK TWICE BEFORE YOU DO ANYTHNG