Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Hivi kuamua kuacha kuchangia harusi mpaka utambie nasi, si uamue mwenyewe! Serikali itatoza vipi kodi mara mbili wakati kila supplier amekwisha lipa kodi kwa bidhaa anayopeleka kwenye sherehe?

Lazima kwanza uelewe maana ya hizo sherehe hasa send off na reception. Hivi umelazimishwa?
 
Yakwangu sikuhitaji mchango wa mtu, hii naisema sababu ya uzoefu, Mwanamayu, unataka kusema ndugu zako wako katika hali nzuri sana, mpaka uwe sehemu ya kushuhudia matumizi mabaya ya pesa kwa siku moja tuu?
huna ndugu wanaolia kwa kukosa mkopo wewe, saidia na changia mambo ya lazima, kataa huu ujima wa kuchangishana mambo ya anasa.
 
Hiyo ni njia mojawapo ya kushirikiana na jamii inayokuzunguka.
 
Michango ya harusi ni unyonyaji na uzembe tu wetu Watanzania.Najua wengi waliopitia katika 'utamaduni' huu wa kuchangiana fedha za kunywa na kula kwa siku moja watapinga sana lakini ni wazi michango ya harusi imepitwa na wakati na wapende wasipende taratibu híi kitu inakufa.
 
Tusidanganyane eti kuwa kutoa ni moyo...michango ya harusi imekuwa kama obligation,kwamba ni lazima nikuchangie otherwise mara nyingi inakuwa 'silent beef'.Ni scratch my back,I scratch yours too policy...hapa suala la kusaidiana linakufa na kuzaa silently forced contract.
 
Kubali kuonekana mbinafsi, ishi bila stress, na ishi maisha yako kwa furaha bila bugudha ya wataka michango, fikiria kupita pale jeshi la wokovu na kusaidia wale watoto pale ama sehemu nyingine zenye watu wenye uhitaji.
Amini Mungu atakubariki utakapowasaidia wenye shida kuliko haya matumizi ya kufuru.
 
Yakwangu sikuhitaji mchango wa mtu, hii naisema sababu ya uzoefu, Mwanamayu, unataka kusema ndugu zako wako katika hali nzuri sana, mpaka uwe sehemu ya kushuhudia matumizi mabaya ya pesa kwa siku moja tuu?
huna ndugu wanaolia kwa kukosa mkopo wewe, saidia na changia mambo ya lazima, kataa huu ujima wa kuchangishana mambo ya anasa.

Mawazo Mengine bwana! Sasa wewe mbona hukuacha kufunga harusi yako, hizo pesa ukawapa watu wanaotaka mikopo.. Au ukulijua hilo. THINK TWICE BEFORE YOU DO ANYTHNG
 
Kubali kuonekana mbinafsi, ishi bila stress, na ishi maisha yako kwa furaha bila bugudha ya wataka michango, fikiria kupita pale jeshi la wokovu na kusaidia wale watoto pale ama sehemu nyingine zenye watu wenye uhitaji.
Amini Mungu atakubariki utakapowasaidia wenye shida kuliko haya matumizi ya kufuru.

Ooooooookay! Si tatizo kubwa sana! jambo ni moja tu hapa. Wewe umesikiliza/umeona au umesoma maandiko matakatif,sasa yamekuingia na Unaona kila kitu sasa kinaenda kinyume na maandiko.. Kijana jua kuwa unapotoa mchang pia umemsaidia mtu, na umebarikiwa. Hata kama we hukutoa,usikurupuke ukaanza kufuata kila kilichosemwa kweny maandiko bila kukaa chini na kukifikiria,unawez kupotoka na ukatafsir vibaya maandiko.
 
Mawazo Mengine bwana! Sasa wewe mbona hukuacha kufunga harusi yako, hizo pesa ukawapa watu wanaotaka mikopo.. Au ukulijua hilo. THINK TWICE BEFORE YOU DO ANYTHNG

Sijakwambia usifunge harusi! nachokuasa acha kutegemea michango toka kwa wengine kwani utagharamika mpaka unakufa! michango ya harusi ni deni la kudumu ambalo utalilipa siku zote, sasa kwanini usifikirie kutememea mfuko wako then uwaalike hao unaowataka, ili shughuli itakapokwisha usiwe na deni nao!
Usione sifa kuchangiwa kwani utazilipa mkuu,na usipolipa utakuwa adui yao waliochanga ya kwako
 
Huo ni mtazamo wako hivyo bac usilazimishe na wengine waishi kibinafsi kama unavyotaka wewe, nini maana ya jumuia na jamii kwa ujumla unamchango gani katika jamii iliyo kuzunguka?je ni salam tu? kama unacho unatoa kama huna bac unatulia,don't stress your self
 
Naunga mkono hoja
mimi harusi yangu sikuchangisha watu. Marafiki wachache waliniletea hela bila kuwaomba. Sikufanya vikao, ndugu walikuja juu nikakomaa sikubadili msimamo. Hiyo ilikua 2008.
Tangu 98 sijawai kuhudhuria vikao vya harusi baada ya wenyeviti wa "kamati" kuharibu harusi fulani kwa kutowajibika kwa walichopangiwa. Mwaka huo huo rafiki yangu akaoa harusi kubwa ilifanyikia diamond jubilee, baada ya mwezi akaja kwa mshikaji kuomba mkopo wa laki 2. Nikaona mambo ya maharusi makubwa ni ujinga tu
halafu hii kitu ni kama unakopa. Utakaowachangisha baada ya mwaka wote watakua wamekuletea kadi na wewe uwachangie hata harusi za watu usiowajua. Utatumia fedha nyingi kuliko ulizochangiwa.
bora ufanye harusi ndogo unayoimudu wewe na familia yako, usiache madeni
inasikitisha kuona vijana wengi wanaishi kwenye dhambi kisa hawana pesa ya kufanya harusi. Huu ni upungufu wa mawazo. Harusi ni kitu cha kwenda kanisani au kwa shehe au bomani, yanayofuata si ya lazima.
 
Nimechangia harusi wee mpaka sasa niko hoi na hivi niandiapo post hii nina kadi tatu za november eti kiwango cha chini laki.Sasa nimeamua hizi ni harusi za mwisho kuchangia pamoja na kwamba nimepanga kufunga ndoa mwakani na sihitaji mchango wa mtu na hakutakuwa na kamati wala big bash,just me,my bride and our parents in church and later we reserve a table at one of 5stars hotel in town for dinner and honeymooning in some beach resort kigamboni au bagamoyo.How about this guys? Quite stunning ah!
Just live yr life guys and stop begging,ni kujidharirisha tu kutwa kujipendekeza kwa watu na ili wakuchangie.Haya mambo haya yanafanya wengine wanachangiwa hadi watoto,ujinga mtupu!
 
Dah, hii michango ya harusi sasa imekuwa kero nimetafakari hapa nilipo niko na kadi za michango sita, mbili za watu wa ofisini harusi zao ni mwezi dec, nina ya rafiki wawili, mdogo wa mwenyenyumba na mwingine ni rafiki wa braza nikifikiria hapa naona nikitoa michango Dec itakuwa ngumu kwangu.
Ila kwa marafiki zangu ambao hamjaoa wala kuolewa mtanisamehe mwakani sitachangia harusi na kama nikichangia basi ni zile za kupewa ahsante na sio mwaliko
 
Nachukia sana hiyo michango. Sijui kwa nini watu hulazimisha harusi za gharama kubwa.
 
umeonaeee kumbe ni kero kwa wengi, mie cn hamu jamani ni kero mie nina kadi kama 16 tena wasivyo na haya eti unatiliwa kadi mbili bahasha moja ya kitchen party na sendoff! halafu uliza relationship? eti jirani yako wa tegeta anaozesha binamu yake anaeishi mbagala!!! mie choka kabisa
 
Wewe umeshaoa au kuolewa? Kama umevuta au kuvutwa tu ndani ok,ila kama uliwachangisha watu wakati wa harusi yako,usi-mind! Na pia kama utasema eti ukija kuoa utawaalika watu wachache tu kwa kuwa pesa unayo,nalo heri.Lakini kumbukeni jamii yetu,utashangaa siku unasusiwa shughuli ambayo ungewahitaji watu hasa msiba.
 
halafu haka kamtindo kamekomaa si mijini tu hadi vijijini. Ajabu ni kwamba huyo huyo uliyemchangia kwa arusi yake kesho ukimwomba akuchangie hata kwa kukukopesha hela kwa ajili ya kumpeleka mtoto shule atakwambia, "dah! kwa sasa niko vibaya sana aisee". kwa nini hatuchangiani kwa mambo ya kimaendeleo bali katika anasa?
 
kinachonikera zaidi ni hii
utakuta watu wameshakaa pamoja wana watoto tena wawili wana umri miaka mitano eti utasikia tuna funga ndoa na kadi za michango kuanzia kitchen party, Send off na harusi
sasa wewe mama mzima na kuzaa mmemaliza unataka kitchen party ya nini, Send off uagwe uende wapi wakati uko kwa mwanaume zaidi ya miaka 6.
si bora mbariki ndoa yaishe

Ndio yale mtu anamuoa mke wake
 
Back
Top Bottom