Niko tayari kuchangia endapo nitapewe mwaliko kushiriki zoezi la kuijaza dunia
Kuna sehemu mmeambiwa ni lazima kuchangia?????!!!!
Umewahi kumjibu mtu kuwa hutaki kumchangia na akaendelea kukukumbusha???!!!
Michango sio taabu mnafiki ni wewe uliyepokea kadi ya kwanza mpaka ya tisa halafu unakuja kulalama huku
Tatizo mtu anakupigia simu halafu anakuuliza hivi siku hizi unafanya kazi wapi??
Ukimtajia tu anakukadiria na kiwango cha mshahara unachopata halafu anakukandamizia na mchango hapo hapo.......
Ndiyo majukumu yenyewe hayo. Mbona mkialikwa kwenye kikao mnapleji mahela kibaao, huku jukwaani mnalalamikia kadi.....
yaani me jamani niliachaga kuchangia harusi atakae nichukia poa tu. Sababu mimi mwenyewe nafight kupata maendeleo kamshahara kadogo bado hakohako nianze kugawa eti kufanikisha kuona kwa watu wengine nimejuana nao miezi michache tu. Lo! Sifikirii kumchangisha mtu kwenye harusi yangu nitakaoweza kuwaalika ndo haohao. Harusi zenyewe tunupoteza pesa na muda mwingi alafu zinadumu kwa muda mfupi. Aaaagh! Sitoka nichange.. tubadilike jamani,hii nchi.....This is stupidity of africans, kutwa kucha ni kuwaza harusi n sherehe, hamna kingine cha maana, msimu mzima ni vikao vya kamati tu,
UJINGA!!, say NO to michango ya harusi.
Si wewe tu utakuja jamaa na tumbo kubwa linakuletea kadi tena na kiwango wamekiweka,baadae kila siku linakuja kudai! Mimi hadi nimevunja urafki na rafki yangu baada ya kumwambia kwa sasa sina. Hivi nauliza unaponidai kama nimekopa FINCA utaniazima mke wako japo usiku mmoja?Jamani hivi kuchangia harusi sasa imekuwa lazima?
Nahisi sasa harusi zinatuletea umasikini, yani mtanzania wa kawaida nina kadi tisa mpaka sasa.
Bado natafutwa na jamaa yangu mwingine, yani simu imejaa meseji za watu wanakumbushia michango.
Jamani hatuwezi kuwa na utaratibu mbadala kwenye hili swala? Tupungiziane stress!
Halafu na hii tabia ya mtu anakutumia tu ujumbe uje siku fulani mahala fulani kuna kikao cha harusi, kumbe kesha kuweka kwenye kamati ya harusi we bila kujua afu ukifika wanaweka kiwango cha kila mwanakamati kutoa.
Nadhani tuhitaji mbadala wa hili.
Unasapoti tuchangie sawa, shemu na yeye tuchangie? Au ndo methali isemayo mzigo wa chizi huishia kichwani?Sawa, LAKINI fikiria yafuatayo:-
1. Nyama ya kuku na ng'ombe huliwa sana kwenye sherehe; wafugaji na wauzaji pamoja na familia zao wanafaidika.
2. Wali, ndizi, mbogamboga n.k havikosekani kwenye sherehe; wakulima, wafanyabiashara sokoni pamoja na familia zao wanafaidika.
3. Wapiga picha, MCs, Video shooters, watengeneza kadi pamoja na familia zao wanafaidika.
4. Wenye kumbi pamoja na familia zao wanafaidika.
5. N.k
MUHIMU:
Ni vema tukajenga utamaduni wa kuchangia kulingana na uwezo ulio nao.
Na wewe KJ tu huna lolote. Sikiliza kibao "majanga" labda utaelimikaHii mada nadhani ni mara ya 10 kama si zaidi kuwekwa humu!!!!. Mkuu kama mtu anakukera mpe laivu, kuja kulalamika lalamika hapa hakusaidii kitu. Kama hutaki kuchanga acha PERIOD.
Chukua hatua acha kuchangia harusi na wewe ukiwa na harusi alika watu waje kusherekhekea na sio kutoa mchango. Hii kitu inaweza kabisa kufa iwapo tutaanza nasisi wenyewe tusisubiri mtu mwingine atuamulie . Tuwe mbele ktk kuisaidia jamii hasa kwenye maradhi. Ukiwa na 50000 nenda pale muhimbili angalia ni nani amekosa pesa ya dawa au vipimo msaidie huyo au nenda mashuleni utapewa majina ya watoto walio na hali ngumu then wasaidie ada au uniform.
Michango go ya harusi ni majangaaaaaa, cha MSINGI ni kuacha Kabisa kuchangia