Hii michango imekuwa mingi sana. Kibaya zaidi ni pale mtu anakutafuta hata kama hamjaongea miaka 5. Na hizi sms za kukumbushia michango zinaudhi sana. Mtu alikuwa hakujulii hali hata siku noma, leo hii unapata sms ya good morning everyday. Unafiki mtupu. Mimi nikioa nitafanya harusi kwa uwezo wangu. Watakaonichangia nitashukuru lakini sitaki ufahari wa kusababisha kero kwa wenzangu.