Sawa, LAKINI fikiria yafuatayo:-
1. Nyama ya kuku na ng'ombe huliwa sana kwenye sherehe; wafugaji na wauzaji pamoja na familia zao wanafaidika.
2. Wali, ndizi, mbogamboga n.k havikosekani kwenye sherehe; wakulima, wafanyabiashara sokoni pamoja na familia zao wanafaidika.
3. Wapiga picha, MCs, Video shooters, watengeneza kadi pamoja na familia zao wanafaidika.
4. Wenye kumbi pamoja na familia zao wanafaidika.
5. N.k
MUHIMU:
Ni vema tukajenga utamaduni wa kuchangia kulingana na uwezo ulio nao.
Hakuna upuuzi ambao siupendi kama huo,na source ya yote ni umaskini wa nchi zetu za Africa but wenzetu developed countries scenario kama hii ni chache sana,kuna mwana ananifanyia followup za ajabu dhidi ya mchango hadi kero......
Hii mada nadhani ni mara ya 10 kama si zaidi kuwekwa humu!!!!. Mkuu kama mtu anakukera mpe laivu, kuja kulalamika lalamika hapa hakusaidii kitu. Kama hutaki kuchanga acha PERIOD.
Olesaidimu mh, hivi unafikiri waomba michango lazima wakupe card mkononi! si unaikuta tu nyumbani au ofisini kama anafahamu hom or ofc iko wapi! culture an kuoneana aibu ndio imetufikisha hapa, tena kuna mwingine hata hajakuzoea kivile, anaanza kujichekesha akijua kesho anakuzukia na card. Sema cha muhimu sasa tuamue kubadilika wote, kuanzia waoaji na waolewaji hadi wachangaji, hii kitu tuikatae tu, kwenye ukoo ukikataa wenzio wakitoa unajua kutengwa? halafu hawakutengi wakikungojea kuoa/olewa au mtoto wako akioa/olewa, wanakutenga hadi kwenye ishu zingine kwamba huna ushirikiano.
Halafu eti budget za siku hizi umeziona 30 to 100m ni sawa kweli? walao kwa usawa huu kama mchango ni 10,000 kwenda mbele kadri ya uwezo poa, watu wanaweka limit utafikiri wamekutafutia kazi au wamekusomesha! its high time we Tanzanians to change.
Hata misiba nayo haihitaji ufahari, tumepoteza ndugu,rafiki, wafanyakazi wenzetu ni huzuni, mbwembwe za nini? wengine wanashona nguo, sare, watu full demonstration na mapose why? sasa mwingine afe mwingine afanye marketing ya sura jamani? Mabadiliko yaanze kangu kwako na kwa wote
Hii michango imekuwa mingi sana. Kibaya zaidi ni pale mtu anakutafuta hata kama hamjaongea miaka 5. Na hizi sms za kukumbushia michango zinaudhi sana. Mtu alikuwa hakujulii hali hata siku noma, leo hii unapata sms ya good morning everyday. Unafiki mtupu. Mimi nikioa nitafanya harusi kwa uwezo wangu. Watakaonichangia nitashukuru lakini sitaki ufahari wa kusababisha kero kwa wenzangu.
Kuchangiana na kusaidiana ni mila zetu hatuwezi kuziepuka bila kuacha madhara tupo kwenye mtibwiliko wa maisha kuanzia kiuchumi mpaka tamaduni zetu sasa la muhimu ni kujua ni vipi na kiasi gani tunasaidiana!!!
Nashukuru lile jibu langu la kwanza limefanya kazi,nilikusudia kuamsha hisia juu ya tamaduni zetu kuwa sis ni wamoja tusiharibu hii ila tujadili jinsi ya kuendelea nayo bila ya kuumia
Mawazo ya kijinga kabisa haya, hizi mila za kijiga kawashauri wamasai wenzako.
Wa kulaumu ni huyu aliyeanzisha huu utaratibu
Wadau hii michango imekuwakero sasa, binafsi mpaka sasa hivi nina kadi 6 za michango,simu kila mda inapigwa kukumbushwa michango,sms ndo usiseme. Inatubidi kubadilika kabisa na hii michango isiyokuwa na tija zaidi ya kuacha madeni na lawama. Unapigiwa simu kila mara kama unadaiwa vile. Kama na wewe umekutana na kero yoyote embu tujuze hapa na nini suluhisho?
wewe ni mmoja kati ya waliompa kadiKwani umelazimishwa? Kama hutaki kulipa potezea waachie wanataka
1)Unapokea zanini hizo kadi?
2)Hata ukipokea umeambiwa usipochangia unapewa adhabu?
3)wape makavu laiv kwamba hautaki wakupigie sim au wakutext' au unawaogopa?
Duh..kadi 6..ukisema kila moja utoe elfu 50..ni laki 3 iyo ahaha pole.
Mkuu wala usihofu, mchango wa harusi siyo lazima. ukiwa na nafasi unachangia usipokuwa na nafasi unamwambia ukweli mhusika ili ajue uko under tight budget.
Kwani umelazimishwa? Kama hutaki kulipa potezea waachie wanataka