Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Sawa, LAKINI fikiria yafuatayo:-

1. Nyama ya kuku na ng'ombe huliwa sana kwenye sherehe; wafugaji na wauzaji pamoja na familia zao wanafaidika.
2. Wali, ndizi, mbogamboga n.k havikosekani kwenye sherehe; wakulima, wafanyabiashara sokoni pamoja na familia zao wanafaidika.
3. Wapiga picha, MCs, Video shooters, watengeneza kadi pamoja na familia zao wanafaidika.
4. Wenye kumbi pamoja na familia zao wanafaidika.
5. N.k

MUHIMU:
Ni vema tukajenga utamaduni wa kuchangia kulingana na uwezo ulio nao.

Ukishaangalia hivyo angalia pia na upande wa mchangiaji kwa jinsi anavyoumia
 
Olesaidimu mh, hivi unafikiri waomba michango lazima wakupe card mkononi! si unaikuta tu nyumbani au ofisini kama anafahamu hom or ofc iko wapi! culture an kuoneana aibu ndio imetufikisha hapa, tena kuna mwingine hata hajakuzoea kivile, anaanza kujichekesha akijua kesho anakuzukia na card. Sema cha muhimu sasa tuamue kubadilika wote, kuanzia waoaji na waolewaji hadi wachangaji, hii kitu tuikatae tu, kwenye ukoo ukikataa wenzio wakitoa unajua kutengwa? halafu hawakutengi wakikungojea kuoa/olewa au mtoto wako akioa/olewa, wanakutenga hadi kwenye ishu zingine kwamba huna ushirikiano.
Halafu eti budget za siku hizi umeziona 30 to 100m ni sawa kweli? walao kwa usawa huu kama mchango ni 10,000 kwenda mbele kadri ya uwezo poa, watu wanaweka limit utafikiri wamekutafutia kazi au wamekusomesha! its high time we Tanzanians to change.
Hata misiba nayo haihitaji ufahari, tumepoteza ndugu,rafiki, wafanyakazi wenzetu ni huzuni, mbwembwe za nini? wengine wanashona nguo, sare, watu full demonstration na mapose why? sasa mwingine afe mwingine afanye marketing ya sura jamani? Mabadiliko yaanze kangu kwako na kwa wote


Kuchangiana na kusaidiana ni mila zetu hatuwezi kuziepuka bila kuacha madhara tupo kwenye mtibwiliko wa maisha kuanzia kiuchumi mpaka tamaduni zetu sasa la muhimu ni kujua ni vipi na kiasi gani tunasaidiana!!!

Nashukuru lile jibu langu la kwanza limefanya kazi,nilikusudia kuamsha hisia juu ya tamaduni zetu kuwa sis ni wamoja tusiharibu hii ila tujadili jinsi ya kuendelea nayo bila ya kuumia
 
Waliooa na kuchangiwa ndo wanajua umuhimu wa kuchangia wengine.
 
Hii michango imekuwa mingi sana. Kibaya zaidi ni pale mtu anakutafuta hata kama hamjaongea miaka 5. Na hizi sms za kukumbushia michango zinaudhi sana. Mtu alikuwa hakujulii hali hata siku noma, leo hii unapata sms ya good morning everyday. Unafiki mtupu. Mimi nikioa nitafanya harusi kwa uwezo wangu. Watakaonichangia nitashukuru lakini sitaki ufahari wa kusababisha kero kwa wenzangu.

nna watu tangu tuachane miaka 5 sasa,ila walipotaka kuoa wamesumbuaaaaaa,na baada ya ndoa wamepotea tena,,,,,
harus nzuri na ya heshima ni ile isiyohitaj michango toka kwa watu
 
Kuchangiana na kusaidiana ni mila zetu hatuwezi kuziepuka bila kuacha madhara tupo kwenye mtibwiliko wa maisha kuanzia kiuchumi mpaka tamaduni zetu sasa la muhimu ni kujua ni vipi na kiasi gani tunasaidiana!!!

Nashukuru lile jibu langu la kwanza limefanya kazi,nilikusudia kuamsha hisia juu ya tamaduni zetu kuwa sis ni wamoja tusiharibu hii ila tujadili jinsi ya kuendelea nayo bila ya kuumia

Mawazo ya kijinga kabisa haya, hizi mila za kijiga kawashauri wamasai wenzako.
 
Mawazo ya kijinga kabisa haya, hizi mila za kijiga kawashauri wamasai wenzako.

We ni kabila gani ambalo kaburi mnachimba wafiwa wenyewe? ????????

Give and take haiishii harusini tu.

Jaribu kufikiria uhalisia wa maisha mjinga wa ukubwani wewe..say sisi wamasai wajinga kama unavyodhani wewe ni kabila gani ambaye mwenzetu kabila na mila zenu zinawasisitiza juu ya kutokusaidiana????

Mjinga kama wewe bila ya authority huwa hamulewi sasa mimi najitolea kukupa distance learning,kasome theory hizi halafu na wewe unipe nikasome ili mjadala uende

1. Structural functionalism
2. Symbolic interactionism
3. Social construtionism of reality

Ujinga ni sehemu ya kujifunza kwa anayekubali mapungufu na kwa nayegomea mapungufu hakika upumbavu hauko mbali naye..will be back kama utaleta nadharia na vitendo sio kubisha tu
 
Wadau hii michango imekuwakero sasa,

binafsi mpaka sasa hivi nina kadi 6 za michango,simu kila mda inapigwa kukumbushwa michango,sms

ndo usiseme.


Inatubidi kubadilika kabisa na hii michango isiyokuwa na tija zaidi ya kuacha madeni na lawama.

Unapigiwa simu kila mara kama unadaiwa vile.


Kama na wewe umekutana na kero yoyote embu tujuze hapa na nini suluhisho?
 
Wadau hii michango imekuwakero sasa, binafsi mpaka sasa hivi nina kadi 6 za michango,simu kila mda inapigwa kukumbushwa michango,sms ndo usiseme. Inatubidi kubadilika kabisa na hii michango isiyokuwa na tija zaidi ya kuacha madeni na lawama. Unapigiwa simu kila mara kama unadaiwa vile. Kama na wewe umekutana na kero yoyote embu tujuze hapa na nini suluhisho?

1)Unapokea zanini hizo kadi?
2)Hata ukipokea umeambiwa usipochangia unapewa adhabu?
3)wape makavu laiv kwamba hautaki wakupigie sim au wakutext' au unawaogopa?
 
Mkuu wala usihofu, mchango wa harusi siyo lazima. ukiwa na nafasi unachangia usipokuwa na nafasi unamwambia ukweli mhusika ili ajue uko under tight budget.
 
Duh..kadi 6..ukisema kila moja utoe elfu 50..ni laki 3 iyo ahaha pole.

kati ya hizo mkuu kuna kadi mbili wameandika kabisa mchango sio chini ya laki moja,kuna raia wengine sijui huwa wanafikiria kwa kutumia ma------?
 
Back
Top Bottom