Habari za asubuhi wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge' yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha chini cha kunichangia ni laki moja.
Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu ambaye humfahamu.
Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.
NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.
Hii mara kadhaa, nimeiona..tena 'maofisini' ndio kwenyewe.
Yaani, ndugu yeyote wa mfanyakazi mwenzio akitaka kuoa/kuolewa michango(hata kama humjui, au hamna ukaribu). Halafu michango ya sherehe hizo zimekuwa nyingi utasikia sijui kitchen party, send off, harusi yenyewe!
Habari za asubuhi wakuu? Hii wiki tu nimepokea sms na kupigiwa simu zaidi ya 5 watu wanakudai mchango uchangie harusi yake. Namaanisha kudai mchango nawala sio kuomba uchangie. Mtu anakupigia simu alafu anakwambia taja "pledge' yako kwenye harusi yangu. Unamjibu kistaarabu tu ondoa shaka muda ukifika nitakuchangia tu. Yeye anakulazimisha usiwe na wasi ahidi kiasi chochote kile haina tatizo. Baada ya kukubana sana unamweleza kiasi fulani, huyo anayedai anakujibu samahani kaka/dada kiwango changu cha chini cha kunichangia ni laki moja.
Samahani lakini sijui kwa vile mimi ni mgeni na haya maswala au ndio kawaida kwa wote.
Maana ndani ya mwezi mmoja natakiwa niwachangie watu zaidi ya 5.
Swali hiyo hela anayodai mtu aliiweka mfukoni mwako? Maana kwa mimi ninavyojua mtu unapoguswa na swala hili na ukaribu na mhusika ndivyo utakavyotoa kiasi kikubwa.
Chakushangaza kingine unapigiwa simu na marafiki nao utoe pledge kwa mtu ambaye humfahamu.
Mimi binafsi sitamkwaza mtu wakati wa kuomba kuchangiwa.
NIMEMALIZA, NAWAKILISHA.
sisi watanzania hatupendi kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii, unakuta jamaa lofa tu wa kijiweni anatengeneza kamati nzuri ya harusi na kukusanya Mil. 6 au zaidi, then anafanya harusi ya kifahari, that is irresponsible and corrupt behavior!
mimi na my wife wangu tulibariki ndoa bila sherehe mapema alfajiri, na niliwahi kazini saa moja na nusu asubuhi.Total cost haikuzidi Sh. ELFU HAMSINI!
Hivi dunia ya leo mtu unafanya harusi hujajiandaa uba kazi ya kutuma sms kla dakika kuuliza michango?? Hebu tubadilike,fanya jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wakoacha kusumbua watu.nakumbuka wakati wa harusi yetu,tulijipanga,tukakusanya pesa zilipofika 7 mill,tukatangaza harusi,watu 70 tu ndio tuliwaalika,hatukumchangisha mtu,ila ilikua harusi nzuri sana,kila kitu kilienda kama tulivyopanga,na mpaka leo tuanaishi kwa upendo na furaha
Mkuu hippocratessocrates nina kadi nitakuletea jioni ya Send off na Harusi ya dada yangu! Tafadhali usizime simu!
Nafikri katika hili serekali ya dhaifu inatakiwa iweke masharto magumu ya kodi labda watu wakiona fedha yao yote inaishia kwenye kodi tutaacha huu upuuzi! Watu wanalazimisha kukuita kwenye kamati kuu, halafu wanapanga elfu 50 yaani uchimung'unye wala uchicheme!! Hapo hapo unakuta una harusi kama 4 kwa mwezi, sasa hiyo si laki 2 jamani?
Aiseee mimi kuna baadhi ya watu au makabila sichangii mpaka nijui viwango vyao vya uchangiaji. Yaliwahi kunikuta, nimemchangia mtu fulani 80,000 mtaani halafu sikupewa kadi. Baada ya sherehe jamaa mtaani wakaniuliza mbona sikuonekana kwenye send off party ya jirani, nikawajibu nilichangia lakini sikupata kadi, ndiyo nikafahamishwa kwamba wote waliochangia chini ya 100,000 hawakupewa kadi hata ya single....