Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania


Ndoa nn harusi nn changanua
 
huu mchezo uliozuka sasa wa watu kupeana mimba kwanza kisha ndiyo kuanza kutukaba tuwape michango ya harusi mi sikikubali hata kidogo. Huu siyo utaratibu mzuri kabisa ambao sisi watanzania inabidi tuufuate.
yaani tatizo lako wewe ni mimba umesahau kuwa mimba ni matokeo ya sex, mtu akibort je achangiwe? au wanao sex bila mimba je wachangiwe? Nazani kama unataka kuisaidia jamii ni kuuangalia mzizi wa tatizo sio matokeo ya tatizo. Sishabikii watu waolewe na mimba ila sioni kwa nini iwe ni tatizo kama kuna aliyeolewa na kaabort. Kama unamchangia mtu, mchangie tu na kama hutaki usitoe tu, mimba isiwe sababu.
 
Hiyo ndio shida ya umasikini,ukiwa na pesa vyote unafanya Wenyewe halafu unakaribisha watu kunywa tu.
 
kweli mkuu kijiji watu wanakula hadi wanabeba na hawajachangia hata cent! Sasa ndg office ina staff 12 waliopo kwenye ndoa may b 4, utachakaa kwa kuchangia
 
Kweli cybertech,vitoto haviendi shule ada 60,000 majirani wanajua ila wanacheka. Ila ukiwa bachelor utasikia oa umri unaenda,m#***%t@ unafiki mtupu
 
Hapa juu ya meza nina kadi nane za michango ya harusi na sendoff, nikijumulisha zote ni sh laki 480. nina kadi mbili za kuitwa kuwa mwanakamati, najua huko sio chini ya laki tatu. nikijumlisha yote hiyo napata mifuko 39 ya cement, sijapiga lipu kajumba kangu jamani! Mnaooa na kuolewa hebu andae harusi ndogo zisizo na gharama kubwa lol! Mwezi wa tisa huo hapo wengine tunatakiwa kulipa ada za watoto wanarudi shule
 
Kama watu wanagegedana, tegemea mimba. Labda tuseme watu waoane wakiwa mabikra.
 

 
Watanzania wengi tunapenda kutatua tatizo linapotokea. We are reactive rather than proactive. Watu wanachezea pesa kwenye sherehe alafu wakikwama kwenye mambo ya msingi baadae inakuwa surprise na mahangaiko. Hatuweki mipango thabiti na ya muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…