Hilo nalo neno ViolSometimes michango inaleta uhusiano mzuri baina ya ndugu na marafiki,wengine fahari yao ni kuchangiana,kwani michango lazima bhana kama hutaki unaacha,kwanza michango mingi si ya kushtukiza unaambiwa kabla,sasa kama mchango tu kumsaidia ndugu yako au rafiki hutaki je utaishije na majirani katika kusaidiana.
Nadhani umekosea; suala la NDOA halina gharama kabisa, iwe ni ya kiserikali,kikristu au kiislam.... Kinacholeta tofautini SHEREHE baada ya ndoa kufungwa kanisani/msikitini/kwa mkuu wa wilaya.Pili bila shaka wewe ni muslim,mana nyie ndoa hata ukiwaambia watu kuanzia asubuhi kwamba unaoa saa mbili usiku nyie ni poa,ila kristos ndoa zao ni process,then naomba umuulize baba yako,alivyofunga ndoa alichangisha au? Labda ndoa iwe ya mkeka
Hata mimi huo ujinga sifanyi,sitoi michango ya harusi na wala sitaomba ya mtu. Ukiendekeza huu ujinga wa kuchangia harusi mwisho wa mwaka utajikuta umetumia pesa nyingi sana. Kuoa ni kwa faida yako haina maana kusumbua wengine.
Kushrikiana kwenye furaha na hudhuni ni utamaduni wetu bahati mbaya hawa waliogeuza biashara sherehe za wenzao ndio wanao tuharibia mkuu. Unajua hata hiyo mil 1 inatosha kabisa kwa sherehe ya harusi tatizo huwa lipo kwa wanakamati.
mm nashindwa kuelewa kwan harusi n kiapo au kula na kunywa jamn....
kwann watu wasioane tu bila ya sherehe!!padre akisema u are now husband na wife c ndo tayar ndoa.....sherehe za mapesa mengi tena ya michango za nn!!
Julsa..... Ujinga ni kutaka kwenda kinyume na mila na desturi zilizozoeleka ktk jamii iliyokulea hadi kukua na kupata akili
sion mantiki ya kukwepa sherehe baada ya ndoa...
Unafanya sherehe ya mahafali sembuse ndoa????
Msiba tu unakuwa na kalamu swmbuse ndoa
kama mmekosa ya kuandika ni heri kupumzka tu
Kweli kabisa kuna watu hawana ustaarabu vitu vidogo wanaweka chuki.Asante ww umeeleza vzr!
Yaani kamati tu ina matumizi mpaka unashangaa!
Mi kiukweli baba angu hataki kabisa kumlazimisha mtu akuchangie, somtym mtu hana inakuwa km deni mpaka anakosa raha!
Na.kuna wengine asipochangiwa anaweka bifu kabisa utafikiri ni lzm au anajua.maisha yako!
Tufike mahali tusiwekeane chuki mtu kwa ajili ya michango
Kuchangia sio mbaya ila kunataasisi wanalazimisha sana haya mambo
Kuna sehem nilifanya kazi mkuu wa idara kidogo anifukuze kazi sababu sikuchangia harusi ya mwanae .
Kuna mambo ya msingi ya kuchangia kama magonjwa ,
Shule na matatizo mengine kwenye jamii . Nashangaa jinsi tunavojitahidi kuchangia Arusi kuliko wagonjwa wetu wanaohitaji msaada wa upasuaji
Tena huko nyuma hasa vijijini kabla hii biashara ya kamati za gharama watu walikua wanachangishana walicho nacho kama vile chakula. Yaani mtu analeta mchele au unga na sherehe inakua nzuri ,ila hawa wanakamati huwa wanampotosha bwana harusi na kumlaghai kuwa ni vema ufanye sherehe ya aina flani . Iwapo wenye harusi watakua na misimamo thabiti basi michango huwa ni midogo mno na huwezi sikia lawama. Kwa mfano hii mil 1 mbona kama ni watu 20 inatosha sana kufanya harusi.Mimi nipo tofaut kidgo.
Kwa destur yetu Watanzania ni watu wakirimu na kupenda kushirikiana. Ni jambo jema kupeana saport katika shida na raha
Tuache ubinafsi na kudopt maish ya jamii zingine
Duh..mimi ndo mtindo wangu huu,sitakagi sifa za kijinga kbs
Vibaya hivyoo
Kushrikiana kwenye furaha na hudhuni ni utamaduni wetu bahati mbaya hawa waliogeuza biashara sherehe za wenzao ndio wanao tuharibia mkuu. Unajua hata hiyo mil 1 inatosha kabisa kwa sherehe ya harusi tatizo huwa lipo kwa wanakamati.
Yaani hii tabia ipo sana huku kwetuNimecheka sana mkuu. pole sana,duuh! Yaani kidogo ufukuzwe kazi kisa hukuchangia harusi ya mtoto wa mkuu wa idara? hatari sana.
Kinachoniuhdi ni michango kua kama deni,kila mara sms ya kukumbusha,simu,yani kero tupu alafu unakuta wameweka kiwango flani bila kujali hali ya wachangiaji unakuta kingine kiko juu sana kwa baadhi ya watu ila wao wanataka ukifikishe,yani ni tabu tupu. Tubadilike kwa kweli aisee.