Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Harusi sio lazima iwe jumamosi mkuu, inaweza siku yoyote mnayopanga ninyi

Kwa sababu mfumo ambao ni default ni ule wa Kikatoliki, harusi inachukuliwa kufungwa Jumamosi. Wengine wanalazimika kufuata hivyo, vinginevyo inaonekana kama sio harusi
 
Jambo zuri hili naamini sio wote wanaotoa michango ya harusi wanaifurahia,
wengi wanaogopa kutengwa na jamii.
Hii michango ipigwe marufuku kwani ni matumizi mabaya ya fedha.
Michango ya harusi ni biashara kwa baadhi ya watu pia.
Unakuta mtu ana magari ya kukodishia maharusi na mtu huyohuyo yuko mstari wa mbele kuwa mwenyekiti au mwanakamati ktk harusi nyingi. Mke wa mtu huyohuyo nae anafanya shughuli za mapambo na catering, na mengineo.

Wajinga ndio waliwao.
 
mkuu, umeongea jambo la msingi sana.

ngongeza:

pamoja na upigwaji marufuku wa michango pia matumizi ya watoto kwenye sherehe hizi za kipuuzi yapigwe marufuku. kuna sherehe moja nimehudhuria juzi kati nikaona watoto wadogo wanavzoteswa mpaka saa 9 alfajiri na kunyimwa haki yao ya msingi ya kupata usingizi. hili suala halikubaliki hata kidogo.
 
Umenena ndugu, yaani hatupumui kila siku ni kadi za harusi. Tumechoka jamani raisi tuondolee balaa hili umaskini unatunyemelea kwani tusipochangia tunatengwa na marafiki

ni kweli kabisa mkuu. haya masherehe ya ajabuajabu yapigwe marufuku au yawekewe utaratibu wa kisheria. kila kukicha hawa wapenda sherehe wanazidi kubuni sherehe. siku hz kuna sherehe za kuzaliwa watoto, engagement party, separation party, divorce party, graduation party na upuuzi mwingine kibao tu. tumechoka na hii misherehe ya kipuuzi...na mtu usipochangia unanuniwa utadhani umeua. tumechoka bhana.
 
Harusi huwa ni jumamosi unaamkia kazini na uchovu jumapili???

Cha muhimu hapo ni hiyo michango kwa watu masikini iangaliwe namna ya kupunguzwa kbs.

umesoma na kuelewa mada au unakurupuka tu? hebu rudia kusoma tena.
 
Hata malezi ya watoto serikali iwalazimishe?
Mzazi anayeruhusu mtoto kwenye sherehe mpaka saa 9 usiku...... akapime akili



 
Anayewashirikisha mifukoni na kitandani anawaonjesha kidogo au Mali yake binafsi?
Hapo hapo kwenye hariusi hela zetu zinarudi. Hvi unadhani nikitoa sh. 50,000 na mwenye harusi akatoa milioni tatu, nikala nikanywa, nikacheza na kuja kuvunja kamati, nani amepoteza? yeye aendelee kufaidi kitandani lakini cha moto amekiona!
 
Kama hamtaki kuchangia si mnakausha tu na kuendelea na maisha yenu, sidhani kama kuna anayesema usipotoa tutakuitia polisi au tutakufunga.
 
Tena wachaga wapigwe marufuku kugawa zawadi za kadi za chadema kwenye harusi
 
Habari ya leo wadau,

Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.

Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.

Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.

Nawasilisha.
 
Mi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu

Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
 
Hao jamaa hata usipokuwa nchini, watatafuta namna tu wakutoe kiasi. Hawana aibu wala pride hata kidogo linapofika suala la kuzidai hizo. Mi ikifika zamu yangu, nta-demand from my old folks tu, wengine njooni na zawadi. Please return the favor.
 
Kweli kwa hali ya sasaivi kila kukicha mahitaji yanaongezeka na mishahara ipo pale pale,mimi nililetewa card ya harusi mchango laki5 au kuna list ya vitu uchague ukanunue ulete,fridge,cooker,kuweka mapazia,Sofa tena wamekwambia
ukisha chagua watakuelekeza wapi ukanunue,na hao watu hata wenyewe hawapikii gas wanapika na mkaa
nikasema wanatukomoa kila aliepewa card ya mchango wa hiyo harusi walisema mie ntakua nje ya nchi,wengine
sijui watakua makazini,nikasema ivi mtu unampa kiwango cha mchango atoe kwani ni harusi yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…