Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chuki yako ni kwa pombe sio michango, hizo pombe ndo zinalipa kodi, ndio mcjango mkubwa kwa bajeti, na hayo masoda mnayokunywa kama maji ya sumu kiasi gani?Mi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu
Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
Dooh!..inabidi unisamehe tuuAisee huwa unashangaza
Mimi nimechagua kuishi maisha yangu kwa mujibu wa kipato changu na imani yangu. Ni maisha ambayo sio lazima watu wengine waish kama mimi.Chuki yako ni kwa pombe sio michango, hizo pombe ndo zinalipa kodi, ndio mcjango mkubwa kwa bajeti, na hayo masoda mnayokunywa kama maji ya sumu kiasi gani?
Aisee, ni shiidah! Hiyo noma, mi hata kisingizio singetoa ningewambia chukueni kadi yenu mkanunue wenyewe hivyo vitu kama mnaweza.Kweli kwa hali ya sasaivi kila kukicha mahitaji yanaongezeka na mishahara ipo pale pale,mimi nililetewa card ya harusi mchango laki5 au kuna list ya vitu uchague ukanunue ulete,fridge,cooker,kuweka mapazia,Sofa tena wamekwambia
ukisha chagua watakuelekeza wapi ukanunue,na hao watu hata wenyewe hawapikii gas wanapika na mkaa
nikasema wanatukomoa kila aliepewa card ya mchango wa hiyo harusi walisema mie ntakua nje ya nchi,wengine
sijui watakua makazini,nikasema ivi mtu unampa kiwango cha mchango atoe kwani ni harusi yake?
Mi nilishampiga biti wife mambo ya michango ya harusi na kitchen party zisizo na tija.Mi...amebaki wife kunielewa....dawa yake inachemka na hiyo michango yake
Kwakweli michango ni Jipu.Jipu hili inabidi JPM atusaidie kulitumbua maana Rais akisema hamna michango watu wataheshimu [emoji28]
Umesema huwezi kuchangia harusi yenye pombe badala yake hicho kiasi unaweza kukitoa kama zawadi, kama mchango ni Tsh elfu 30 na ina pombe hutoi ila utatoa zawadi ya elfu 30 tena baada ya harusi kupita, Lengo la mchango ni mtu afanikishe shughuli yake hapo unakua hujamsaidia, kwenye harusi kuna vinywaji tofauti na kila mmoja anakunywa anachoweza, watu wengi mmekariri pombe ndio dhambi ila uchafu mwingine haukemewi kama pombe,Mimi nimechagua kuishi maisha yangu kwa mujibu wa kipato changu na imani yangu. Ni maisha ambayo sio lazima watu wengine waish kama mimi.
yani wakavu,ivi unataka cooking range wakati kwanu mnapika na mkaa ..nilicheka mpaka nikikumbuka hua najiulizaAisee, ni shiidah! Hiyo noma, mi hata kisingizio singetoa ningewambia chukueni kadi yenu mkanunue wenyewe hivyo vitu kama mnaweza.
HayaDooh!..inabidi unisamehe tuu
Haaaaahaaaaa... Changa bhana ili uje kuchangiwa na wewe....hahaaahaaaa... Pole sana dear.. Just try to do what you can and leave what you can't , don't force yourself .. Do what you can handle.. After all not all marriages last forever now these days ... Thanks..Habari ya leo wadau,
Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.
Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.
Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.
Nawasilisha.
Hapo ndiyo utakapo shindwa kushangaa aise duuuuBwana harus anataka harusi ya mil 25
Halafu yeye na familia wana laki 2
Hapa hua nachoka
Ukweli ni kwamba mimi kwa ujumla si muumini wa michango ya harusi na kitchen party au sherehe kwa ujumla. Mm huwa napata shida sana kuchangia harusi wakati kuna jirani yangu analala njaa kwa kukosa pesa kidogo tu ya chakula. Huwa napata taabu sana kutoa alfu hamsini kwaajili ya harusi wakati kuna watanzania wanateseka kwa maradhi kwa kukosa alfu 30 tu ya dawa. Kwangu mimi ni bora nikaenda muhimbili wodi ya watoto nikaona japo watoto wawili kila mmoja nikampa alfu 50kuliko kuchangia harusi watu wakastarehe.Umesema huwezi kuchangia harusi yenye pombe badala yake hicho kiasi unaweza kukitoa kama zawadi, kama mchango ni Tsh elfu 30 na ina pombe hutoi ila utatoa zawadi ya elfu 30 tena baada ya harusi kupita, Lengo la mchango ni mtu afanikishe shughuli yake hapo unakua hujamsaidia, kwenye harusi kuna vinywaji tofauti na kila mmoja anakunywa anachoweza, watu wengi mmekariri pombe ndio dhambi ila uchafu mwingine haukemewi kama pombe,
Hata mtoto wako unaweza kumpa pocket money akaendea guest, unapotoa hela toa tu usifuatilie magumizi.
You really display my character. Nimependa sana. Mimi huwa nawagomea kazini kwangu, huwa hawanielewi kabisa, lakini huwa nawambia kuwa ipo siku watanielewa tu. Mi nawashangaa watu, unapanga sherehe kubwa kwa kutegemea hela za watu! Ni ajabu sana hii kitu!mimi sichangii sherehe yeyote, hilo linajulikana hata kazini kwangu. Na kuweza kufanikisha hili kwenye harusi yangu sikuchangisha mtu hata mmoja. Mimi na mumewangu(mchumba kwa kipindi kicho) tulikubaliana kufanya sherehe ya kipato chetu, ambayo kiukweli ilikuwa ni ndoa na watu wakala ubwabwa na kunywa maji baaaas!. Ila tulienda honeymoon ya hatari. Ukweli sijawahi jutia hata kidogo, mpaka leo nipo na amani sana maana wananijua mimi nachangia misiba, ugonjwa na mambo ya kielim tu! Tena nipo very open, mtu akinifata na kadi yake namwambia wala asinipe maana sintachangia. Mwanzoni waliniwekea kinyongo, ila kwa sasa ninawafuasi wakutosha ambao wameunga telaaaaa!. Hii michango inachosha na kukosanisha watu sana.