Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu

Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
Chuki yako ni kwa pombe sio michango, hizo pombe ndo zinalipa kodi, ndio mcjango mkubwa kwa bajeti, na hayo masoda mnayokunywa kama maji ya sumu kiasi gani?
 
Yaani siku hizi michango imekuwa kama kukomoana, mtu ana takiwa achangie kadir ya uwezo wako, ila kama ba wewe ulilazimisha wakuchangie, asee utawalipa wotee kwenye harus zao,haiepukiki hiyo
 
Kweli kwa hali ya sasaivi kila kukicha mahitaji yanaongezeka na mishahara ipo pale pale,mimi nililetewa card ya harusi mchango laki5 au kuna list ya vitu uchague ukanunue ulete,fridge,cooker,kuweka mapazia,Sofa tena wamekwambia
ukisha chagua watakuelekeza wapi ukanunue,na hao watu hata wenyewe hawapikii gas wanapika na mkaa
nikasema wanatukomoa kila aliepewa card ya mchango wa hiyo harusi walisema mie ntakua nje ya nchi,wengine
sijui watakua makazini,nikasema ivi mtu unampa kiwango cha mchango atoe kwani ni harusi yake?
Aisee, ni shiidah! Hiyo noma, mi hata kisingizio singetoa ningewambia chukueni kadi yenu mkanunue wenyewe hivyo vitu kama mnaweza.
 
Nachangia misiba, ugonjwa na sherehe za mtu wa karibu sana. Michango ya sherehe za harusi inatufanya tushindwe kufikia malengo yetu kimaisha.

Inabidi jamii zianze utamaduni wa kusaidiana kusomesha, wagonjwa hospitalini na vijana wakianza maisha...thank goodness jamii yangu imeshaanza utamadumi huo.
 
Mimi nimechagua kuishi maisha yangu kwa mujibu wa kipato changu na imani yangu. Ni maisha ambayo sio lazima watu wengine waish kama mimi.
Umesema huwezi kuchangia harusi yenye pombe badala yake hicho kiasi unaweza kukitoa kama zawadi, kama mchango ni Tsh elfu 30 na ina pombe hutoi ila utatoa zawadi ya elfu 30 tena baada ya harusi kupita, Lengo la mchango ni mtu afanikishe shughuli yake hapo unakua hujamsaidia, kwenye harusi kuna vinywaji tofauti na kila mmoja anakunywa anachoweza, watu wengi mmekariri pombe ndio dhambi ila uchafu mwingine haukemewi kama pombe,
Hata mtoto wako unaweza kumpa pocket money akaendea guest, unapotoa hela toa tu usifuatilie magumizi.
 
Aisee, ni shiidah! Hiyo noma, mi hata kisingizio singetoa ningewambia chukueni kadi yenu mkanunue wenyewe hivyo vitu kama mnaweza.
yani wakavu,ivi unataka cooking range wakati kwanu mnapika na mkaa ..nilicheka mpaka nikikumbuka hua najiuliza
ivi walikua serious hawa watu........
 
Habari ya leo wadau,

Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.

Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.

Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.

Nawasilisha.
Haaaaahaaaaa... Changa bhana ili uje kuchangiwa na wewe....hahaaahaaaa... Pole sana dear.. Just try to do what you can and leave what you can't , don't force yourself .. Do what you can handle.. After all not all marriages last forever now these days ... Thanks..
 
mimi sichangii sherehe yeyote, hilo linajulikana hata kazini kwangu. Na kuweza kufanikisha hili kwenye harusi yangu sikuchangisha mtu hata mmoja. Mimi na mumewangu(mchumba kwa kipindi kicho) tulikubaliana kufanya sherehe ya kipato chetu, ambayo kiukweli ilikuwa ni ndoa na watu wakala ubwabwa na kunywa maji baaaas!. Ila tulienda honeymoon ya hatari. Ukweli sijawahi jutia hata kidogo, mpaka leo nipo na amani sana maana wananijua mimi nachangia misiba, ugonjwa na mambo ya kielim tu! Tena nipo very open, mtu akinifata na kadi yake namwambia wala asinipe maana sintachangia. Mwanzoni waliniwekea kinyongo, ila kwa sasa ninawafuasi wakutosha ambao wameunga telaaaaa!. Hii michango inachosha na kukosanisha watu sana.
 
Umesema huwezi kuchangia harusi yenye pombe badala yake hicho kiasi unaweza kukitoa kama zawadi, kama mchango ni Tsh elfu 30 na ina pombe hutoi ila utatoa zawadi ya elfu 30 tena baada ya harusi kupita, Lengo la mchango ni mtu afanikishe shughuli yake hapo unakua hujamsaidia, kwenye harusi kuna vinywaji tofauti na kila mmoja anakunywa anachoweza, watu wengi mmekariri pombe ndio dhambi ila uchafu mwingine haukemewi kama pombe,
Hata mtoto wako unaweza kumpa pocket money akaendea guest, unapotoa hela toa tu usifuatilie magumizi.
Ukweli ni kwamba mimi kwa ujumla si muumini wa michango ya harusi na kitchen party au sherehe kwa ujumla. Mm huwa napata shida sana kuchangia harusi wakati kuna jirani yangu analala njaa kwa kukosa pesa kidogo tu ya chakula. Huwa napata taabu sana kutoa alfu hamsini kwaajili ya harusi wakati kuna watanzania wanateseka kwa maradhi kwa kukosa alfu 30 tu ya dawa. Kwangu mimi ni bora nikaenda muhimbili wodi ya watoto nikaona japo watoto wawili kila mmoja nikampa alfu 50kuliko kuchangia harusi watu wakastarehe.

Kwa kifupi sina interest kabisa na mambo ya sherehe.
Sifa yangu mimi ni kuwachangia wenye shida si kuchangia sherehe. Aidha, zawadi za harusi nina uhuru wa kupeleke hata yenye thamani ya 5,000 au hata laki tano kwa kadiri nitakavoona inafaa.

Mimi si muhudhuriaji wa harusi, mara nyingi hupenda kushiriki harusi za ndugu zangu wa karibu na jamaa zangu wa karibu sana na family friends tu. Lakini hupenda kusaidia wenye shida bila kujali udugu, kabila wala dini. Ndivyo nilivyo. Watu wengi hunisema lakini mimi naishi nitakavyo. Ninayo mengi ambayo nimeamua kuishi kinyume na watu wanavolazimisha watu waishi, mfano, mimi hata siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei, hata ya mke wangu na hata ya mwanangu, wala hata neno happy birdhday huwa silitamki. Napenda kutumia masiku haya kwa kuwasapoti wenye shida. Sioni sababu ya mimi kutumia laki eti kusherehekea birthday ya mwanangu wakati kuna watoto chungu nzima wana malnutrition (utapiamlo) wamekosa hela kidogo kwa ajili ya kuimarisha lishe zao. Laiti, ukitafakari vzuri utatambua nini nasema na kwanini sichangii sherehe. Haya ni maisha yangu niliyoyachagua kuishi hapa duniani. Sitaki sifa kwa mtu, mimi natimiza lengo la kuumbwa kwangu na Mwenyezi MUNGU hapa duniani. I have dedicated my life to support the most in need. I know that i cant finish their problems but i will fullfill my part to the level that i can afford.
 
Hivi harusi ni lazima au mbwembwe tu,ndoa ikishafungwa inatosha mungu ameshawatambua basi sasa maisha yaanze unataka ndoa ya millions afu mke mwenyewe unamfumania kesho kutwa em mjifunze kutoka kwa warusi wale wengi wao akisha oa kanisani anaenda kupiga kaharusi ka watu kama saba hivi wanafamilia na marafiki wa Karibu wanakunywa vodka wakimaliza wengine wanasepa afu anabaki mke na mume apo honeymoon inaanza hadi siku inaisha na kesho mtu anaenda kazini kama kawa ,acheni mbwembwe ndoa ndio inayohitajika hayo nadudu mengine kula kwenu
 
mimi sichangii sherehe yeyote, hilo linajulikana hata kazini kwangu. Na kuweza kufanikisha hili kwenye harusi yangu sikuchangisha mtu hata mmoja. Mimi na mumewangu(mchumba kwa kipindi kicho) tulikubaliana kufanya sherehe ya kipato chetu, ambayo kiukweli ilikuwa ni ndoa na watu wakala ubwabwa na kunywa maji baaaas!. Ila tulienda honeymoon ya hatari. Ukweli sijawahi jutia hata kidogo, mpaka leo nipo na amani sana maana wananijua mimi nachangia misiba, ugonjwa na mambo ya kielim tu! Tena nipo very open, mtu akinifata na kadi yake namwambia wala asinipe maana sintachangia. Mwanzoni waliniwekea kinyongo, ila kwa sasa ninawafuasi wakutosha ambao wameunga telaaaaa!. Hii michango inachosha na kukosanisha watu sana.
You really display my character. Nimependa sana. Mimi huwa nawagomea kazini kwangu, huwa hawanielewi kabisa, lakini huwa nawambia kuwa ipo siku watanielewa tu. Mi nawashangaa watu, unapanga sherehe kubwa kwa kutegemea hela za watu! Ni ajabu sana hii kitu!
 
Alafu mbaya ukishachangiwa baba jua ni denii
Kama ni watu 100 una madeni kivipi
Kwa wale ambao hawajaoa jua lazima ulipe na waliooa jua kuna ndugu yake au mtoto yake weeee;!!! Deniii

Hiii kweli inanipaga mawazo kuhusu kuoa msichana anakuambia mama yangu anataka harusi duh!
 
Back
Top Bottom