Kakole
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,094
- 1,747
Napotezea vipi naogopa kulaumiwa, wengine tupo ofisi moja mpaka ninaona aibu nikiwaona hlf nafikiria kuwachinjia bahariniPole aisee .. Potezea tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Napotezea vipi naogopa kulaumiwa, wengine tupo ofisi moja mpaka ninaona aibu nikiwaona hlf nafikiria kuwachinjia bahariniPole aisee .. Potezea tu
Upo sahihi sana mkuu, ni jambo la kumshukuru Mungu kupata jamii ya waelewaNachangia misiba, ugonjwa na sherehe za mtu wa karibu sana. Michango ya sherehe za harusi inatufanya tushindwe kufikia malengo yetu kimaisha.
Inabidi jamii zianze utamaduni wa kusaidiana kusomesha, wagonjwa hospitalini na vijana wakianza maisha...thank goodness jamii yangu imeshaanza utamadumi huo.
Kwa life style yako hii ubarikiwe mkuu na Mungu akuzidishie zaidi.Ukweli ni kwamba mimi kwa ujumla si muumini wa michango ya harusi na kitchen party au sherehe kwa ujumla. Mm huwa napata shida sana kuchangia harusi wakati kuna jirani yangu analala njaa kwa kukosa pesa kidogo tu ya chakula. Huwa napata taabu sana kutoa alfu hamsini kwaajili ya harusi wakati kuna watanzania wanateseka kwa maradhi kwa kukosa alfu 30 tu ya dawa. Kwangu mimi ni bora nikaenda muhimbili wodi ya watoto nikaona japo watoto wawili kila mmoja nikampa alfu 50kuliko kuchangia harusi watu wakastarehe.
Kwa kifupi sina interest kabisa na mambo ya sherehe.
Sifa yangu mimi ni kuwachangia wenye shida si kuchangia sherehe. Aidha, zawadi za harusi nina uhuru wa kupeleke hata yenye thamani ya 5,000 au hata laki tano kwa kadiri nitakavoona inafaa.
Mimi si muhudhuriaji wa harusi, mara nyingi hupenda kushiriki harusi za ndugu zangu wa karibu na jamaa zangu wa karibu sana na family friends tu. Lakini hupenda kusaidia wenye shida bila kujali udugu, kabila wala dini. Ndivyo nilivyo. Watu wengi hunisema lakini mimi naishi nitakavyo. Ninayo mengi ambayo nimeamua kuishi kinyume na watu wanavolazimisha watu waishi, mfano, mimi hata siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei, hata ya mke wangu na hata ya mwanangu, wala hata neno happy birdhday huwa silitamki. Napenda kutumia masiku haya kwa kuwasapoti wenye shida. Sioni sababu ya mimi kutumia laki eti kusherehekea birthday ya mwanangu wakati kuna watoto chungu nzima wana malnutrition wamekosa hela kidogo kwa ajili ya kuimarisha lishe zao. Laiti, ukitafakari vzuri utatambua nini nasema na kwanini sichangii sherehe. Haya ni maisha yangu niliyoyachagua kuishi hapa duniani. Sitaki sifa kwa mtu, mimi natimiza lengo la kuumbwa kwangu na Mwenyezi MUNGU hapa duniani. I have dedicated my life to support the most in need. I know that i cant finish their problems but i will fullfill my part to the level that i can afford.
Hahahaha.........hata ukienda kudai sina uhakika kuwa utarudishiwa, jukumu letu ni kuwaelimisha watu wafunge ndoa yao kanisani/msikitini na kuelekea zao hotelini kwenda kula honeymoon fulstopsasa mbona tumeshachangia sana na bado hatujaolewa, mnatushaurije tukawadai au
Duuuuuh! basi ww ni mwanamke wa tofauti sana maana mara nyingi wanawake ni wako mstari wa mbele ktk kuchangia sherehe mbali mbali, hongera kwa maamuzi mazuri.Wala usijipe presha ya kuomba michango kwa harusi yako. Yani ile uliochangia haitatambulika hata chembe, ni pale tu utakapo omba michango ya harusi yako ndio utaona kasheshe lake. Kama kweli unataka kuwa huru na michango ni muhim sana kutokuchangisha ya kwako. Hata mimi na baba watoto tulishachangia sana tu (kila mtu kwa wakati wake kabla hatujakutana) ila tulipochumbiana nilimuomba sana tufanye kitu kidogo kwa uwezo wetu ili tukate chain ya michango. Mwanzoni hakunielewa kabisa, ila nilimwelimisha kwa kila mfano juu ya umuhim huu nae akanielewa vyema kabisaaa. Tulichoamua ni kwenda honeymoon mahala pazuri sana kiasi cha kutuachia kumbukumbu isiofutika. Na mpaka leo huwa ananishukuru sana juu ya hili swala kwani anauhuru wa kuamua kuchanga au kutokuchanga pindi anapoletewa kadi na hata kiwango cha kuchangia pia halazimishwi na mtu. Ila kwa upande wangu ndio sichangii hata sumni, kwa hili najulikana na watu wanaonizunguka. Ila kiukweli nipo mrahisi sana, na wala huwa sifikirii mara mbili kwenye maswala ya maradhi, mazishi, elim na yanayoendana na hayo. Namshukuru Mungu sana kwa kunifungua macho mapema!
upo sahihi sn mkuu, kwa hili nakuunga mkono kwakweliKwakweli mleta mada umenigusa sana as nachukia part na maharusi yakushindana. Baada ya yote watu wanaenda kunya na pesa inakwishinea. Niutamaduni wakishamba nakimasikini watu wanafikiri kutoa 1m 5m mpaka 100m kwa ajili ya harusi ni ufahari. Nidhana yakimasiki sana mtu kupoteza ma mil kwenye harusi wakati baada ya harusi anaenda kupanga. Ujinga mkubwa sana wengine after 1 mönth ndoa inaota mbawa. Kwakweli inatia hasira na kuhuzunisha na siku iz mpaka graduation watu wanataka michango. Jaman ama kwa hakika michango itungiwe sheria ama itafutwe njia kudhibiti watu wasiumie. Eti unapangiwa toa mil au laki kadhaa huwa mim nacheka nakutupa kwenye pipa lataka nakusema i'm sorry hujuw pesa yangu naipata kwa dhiki kiasi gani. Nakama ndio anasubiri bahasha yangu yakuowa basi atapata habari nimeowa nakufunga harusi. Huu ni ujinga na umasikin mkubwa kwa watanzania.
upo sahihi sn mkuu, kwa hili nakuunga mkono kwakweli
Ni kweli kabisa wanawake ndio tunaongoza kwa kuzidhoofishafamilia kwa kuendekeza michango isiyo na tija. Ila mimi nipo huru hadi raha. Sina presha ya michango hata kidogo. Naonaga hapa ofisini watu wanavyohaha kutafuta pesa za kuchangia masherehe. Yaani hili ni janga linalohitaji hekima hasa kulitatua. Natuamai ipo siku jamii yetu itapata kuelewa ni kiasi gani kinapotea kwa michango ya sherehe.Duuuuuh! basi ww ni mwanamke wa tofauti sana maana mara nyingi wanawake ni wako mstari wa mbele ktk kuchangia sherehe mbali mbali, hongera kwa maamuzi mazuri.
Upo sahihi sana Nareem yupo ndugu yangu alikuwa akiumiza kichwa sana ataanzaje kuchangisha michango ili afanye sherehe kubwa ya harusi, lakini nilimshauri ajikusanye yeye mwenyewe atafute kiasi cha hela itayotosheleza tafrija ndogo itakayojumuisha ndugu na marafiki wachache alifanya hivyo mpaka leo ananishukuru kweli maana alifanya hivyo na shughuli yake ilifanikiwa na hana mtu yeyote anayemsumbua kwenye issue ya michango ya harusi anachangia pale atakavyojisikia.Ni kweli kabisa wanawake ndio tunaongoza kwa kuzidhoofishafamilia kwa kuendekeza michango isiyo na tija. Ila mimi nipo huru hadi raha. Sina presha ya michango hata kidogo. Naonaga hapa ofisini watu wanavyohaha kutafuta pesa za kuchangia masherehe. Yaani hili ni janga linalohitaji hekima hasa kulitatua. Natuamai ipo siku jamii yetu itapata kuelewa ni kiasi gani kinapotea kwa michango ya sherehe.
jaji mfawidhi watu wanapenda kuishi fake life kweli, basi bora afanye hivyo kwa pesa yake mwenyewe lakini sasa atataka kila mtu aumie kwa starehe yake.Thats too much,unabebwa na Gari limousine na wewe hata ka IST huna.
Watu wanywe heineken wakati wewe huwa unagongea tusker?
Kila meza iwe na keki!
Apples
Okay kama unayo usitukamue sisi,we tunakuchangia tunabyojiweza tu!
Hongera sana kwa msimao ulio nao jamani mimi na wish watu wote tuuige msimamo wako.mimi sichangii sherehe yeyote, hilo linajulikana hata kazini kwangu. Na kuweza kufanikisha hili kwenye harusi yangu sikuchangisha mtu hata mmoja. Mimi na mumewangu(mchumba kwa kipindi kicho) tulikubaliana kufanya sherehe ya kipato chetu, ambayo kiukweli ilikuwa ni ndoa na watu wakala ubwabwa na kunywa maji baaaas!. Ila tulienda honeymoon ya hatari. Ukweli sijawahi jutia hata kidogo, mpaka leo nipo na amani sana maana wananijua mimi nachangia misiba, ugonjwa na mambo ya kielim tu! Tena nipo very open, mtu akinifata na kadi yake namwambia wala asinipe maana sintachangia. Mwanzoni waliniwekea kinyongo, ila kwa sasa ninawafuasi wakutosha ambao wameunga telaaaaa!. Hii michango inachosha na kukosanisha watu sana.
Sherehe na michango ya harusi inatia sana stress. Huu msimu wa MAGU labda utatusaidia tuamke kutoka katika usingizi tulio lala.jaji mfawidhi watu wanapenda kuishi fake life kweli, basi bora afanye hivyo kwa pesa yake mwenyewe lakini sasa atataka kila mtu aumie kwa starehe yake.
Asante sana kwa mchango wako katika hili suala la harusi na michango inakera sana.Hivi wapenda heka heka za arusi kubwa, huku mnategemea kuchangiwa hamna chembe ya aibu? Mkipita thread kama hizi mjue mmekuwa kero kwa wengi.
Mishahara ikitoka kutwa kukumbushia mchango wa arusi utafikiri huyo mke au mume atakuwa mali ya umma. Fanya sherehe ndogo, shirikisha ndugu zako wa karibu tu.
Hongera sana kwa kuwa huru na utakuwa huru kweli.Ni kweli kabisa wanawake ndio tunaongoza kwa kuzidhoofishafamilia kwa kuendekeza michango isiyo na tija. Ila mimi nipo huru hadi raha. Sina presha ya michango hata kidogo. Naonaga hapa ofisini watu wanavyohaha kutafuta pesa za kuchangia masherehe. Yaani hili ni janga linalohitaji hekima hasa kulitatua. Natuamai ipo siku jamii yetu itapata kuelewa ni kiasi gani kinapotea kwa michango ya sherehe.