Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Upo sahihi sana mkuu, ni jambo la kumshukuru Mungu kupata jamii ya waelewa
 
Mimi nilishaacha kuchangia kitambo sana, harusi ni suala personal linalowaunganisha watu wawili kuwa mwili mmoja hivyo hakuna sababu ya kuchangiana hasa ukizingatia maisha ya sasa ndoa hazina furaha, talaka zimekua nyingi. Kwa experience niliyonayo, wakati tukiwa chuo mwaka wa tatu na nne na mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo, ndoa zilikua nyingi sana, ila baada ya miaka mitatu asilimia kubwa ya ndoa hizo zimeishia kwenye talaka mahakamani na hata hawajathubutu kutuomba radhi tuliowachangia wakati wa harusi zao kwa kutupotezea pesa na muda.
Mimi sasa hivi sichangi kwa yeyote yule hata awe nani, na sijawahi kukosana na rafiki yangu yeyote yule kwa kutomchangia kwenye harusi.
 
Kwa life style yako hii ubarikiwe mkuu na Mungu akuzidishie zaidi.
 
sasa mbona tumeshachangia sana na bado hatujaolewa, mnatushaurije tukawadai au
Hahahaha.........hata ukienda kudai sina uhakika kuwa utarudishiwa, jukumu letu ni kuwaelimisha watu wafunge ndoa yao kanisani/msikitini na kuelekea zao hotelini kwenda kula honeymoon fulstop
 
Kwakweli mleta mada umenigusa sana as nachukia part na maharusi yakushindana. Baada ya yote watu wanaenda kunya na pesa inakwishinea. Niutamaduni wakishamba nakimasikini watu wanafikiri kutoa 1m 5m mpaka 100m kwa ajili ya harusi ni ufahari. Nidhana yakimasiki sana mtu kupoteza ma mil kwenye harusi wakati baada ya harusi anaenda kupanga. Ujinga mkubwa sana wengine after 1 mönth ndoa inaota mbawa. Kwakweli inatia hasira na kuhuzunisha na siku iz mpaka graduation watu wanataka michango. Jaman ama kwa hakika michango itungiwe sheria ama itafutwe njia kudhibiti watu wasiumie. Eti unapangiwa toa mil au laki kadhaa huwa mim nacheka nakutupa kwenye pipa lataka nakusema i'm sorry hujuw pesa yangu naipata kwa dhiki kiasi gani. Nakama ndio anasubiri bahasha yangu yakuowa basi atapata habari nimeowa nakufunga harusi. Huu ni ujinga na umasikin mkubwa kwa watanzania.
 
Duuuuuh! basi ww ni mwanamke wa tofauti sana maana mara nyingi wanawake ni wako mstari wa mbele ktk kuchangia sherehe mbali mbali, hongera kwa maamuzi mazuri.
 
upo sahihi sn mkuu, kwa hili nakuunga mkono kwakweli
 
upo sahihi sn mkuu, kwa hili nakuunga mkono kwakweli

Thats too much,unabebwa na Gari limousine na wewe hata ka IST huna.

Watu wanywe heineken wakati wewe huwa unagongea tusker?

Kila meza iwe na keki!

Apples

Okay kama unayo usitukamue sisi,we tunakuchangia tunabyojiweza tu!
 
Duuuuuh! basi ww ni mwanamke wa tofauti sana maana mara nyingi wanawake ni wako mstari wa mbele ktk kuchangia sherehe mbali mbali, hongera kwa maamuzi mazuri.
Ni kweli kabisa wanawake ndio tunaongoza kwa kuzidhoofishafamilia kwa kuendekeza michango isiyo na tija. Ila mimi nipo huru hadi raha. Sina presha ya michango hata kidogo. Naonaga hapa ofisini watu wanavyohaha kutafuta pesa za kuchangia masherehe. Yaani hili ni janga linalohitaji hekima hasa kulitatua. Natuamai ipo siku jamii yetu itapata kuelewa ni kiasi gani kinapotea kwa michango ya sherehe.
 
Saivi mi naiangalia tu hii mialiko, ila zawadi nitatoa kadri nitakavyo jaliwa. Yangu ikifika sitataka kabisa kuwapa watu hizi stress nikitoka church tunaenda kwa familia nyumbani inakua imetoka. Memory itabaki kwa cheti na si vinginevyo
 
Upo sahihi sana Nareem yupo ndugu yangu alikuwa akiumiza kichwa sana ataanzaje kuchangisha michango ili afanye sherehe kubwa ya harusi, lakini nilimshauri ajikusanye yeye mwenyewe atafute kiasi cha hela itayotosheleza tafrija ndogo itakayojumuisha ndugu na marafiki wachache alifanya hivyo mpaka leo ananishukuru kweli maana alifanya hivyo na shughuli yake ilifanikiwa na hana mtu yeyote anayemsumbua kwenye issue ya michango ya harusi anachangia pale atakavyojisikia.
 
Thats too much,unabebwa na Gari limousine na wewe hata ka IST huna.

Watu wanywe heineken wakati wewe huwa unagongea tusker?

Kila meza iwe na keki!

Apples

Okay kama unayo usitukamue sisi,we tunakuchangia tunabyojiweza tu!
jaji mfawidhi watu wanapenda kuishi fake life kweli, basi bora afanye hivyo kwa pesa yake mwenyewe lakini sasa atataka kila mtu aumie kwa starehe yake.
 
Mleta mada, inaelekea umeshaoa na umesahau fadhila za wadau. Rudisha hela za watu. Huo ni utamaduni wetu.
 
Hongera sana kwa msimao ulio nao jamani mimi na wish watu wote tuuige msimamo wako.
 
jaji mfawidhi watu wanapenda kuishi fake life kweli, basi bora afanye hivyo kwa pesa yake mwenyewe lakini sasa atataka kila mtu aumie kwa starehe yake.
Sherehe na michango ya harusi inatia sana stress. Huu msimu wa MAGU labda utatusaidia tuamke kutoka katika usingizi tulio lala.
 
Asante sana kwa mchango wako katika hili suala la harusi na michango inakera sana.
 
Hongera sana kwa kuwa huru na utakuwa huru kweli.
 
Huku makambako kuna kamchezo Ka bwana Harusi kutaka achangiwe mahari.Aisee,michango ii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…