vlazarowosky
Senior Member
- Nov 9, 2014
- 173
- 285
Kwenye harusi unaambiwa bajeti isipungue mil 20 alafu ndoa zingine unaona kabisa zinaenda kuwa matatani.Ukichukua michango ya harusi iliyotolewa hapa nchini Tanzania kwa mwaka huu unaoishia unaweza kukuta kama taifa tukanunua Bombadier nyingine 2 au 3. Kupanga ni kuchagua.
Na ni wakumbushaji wazuri sana wa tarehe ya mwisho.Siku hizi akina mama wanalazimishana kuchangia mpaka sherehe za watoto wao kuhitimu vyuo vikuu!! Sherehe tu sijawahi kusikia wanachangia kwa mgonjwa amvaye hana uwezo wa kulipia matibabu au wanafunzi ambao ni yatima au wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia karo - akili zote zipo kwenye sherehe, tofauti kabisa na wenzetu wa Kenya.
Uamumuzi ni wako kuweka vipaumbele katika maisha yako, hata hivyo namna ulivyo ji-brand kwa jamii yako ndo inakufanya uwe hivyo. Binafsi, sitoi kipaumbele kwenye michango ya harusi, na ukinipa kadi andika maumivu, mara nyingi sitoi kabisa au natoa kiasi kidogo sana kama 10000 hivi, maana sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako, na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usiyo yaweza. Lakini upande mwingine, huwa nazingatia sana swala la matatizo, kama ajari, ugonjwa, vifo, na shida zingine ambazo mtu hajitakii mwenyewe na zinakuja bila kujali hali zetu za kiuchumi.Neema iwe kwenu.
Michango ya harusi inanirudisha nyuma kimaendeleo. Nina kibarua mahali na ninalipwa hela ndogo tu wala haizidi laki 8, sasa kila nikiibajeti kufanya mambo yangu nakutana na kadi ya mchango wa harusi (kitchen party, send off etc). Halafu cha kushangaza ni kwamba hizi kadi za michango zinatoka nyingi kwa wanawake ambao ni ndugu, jamaa na marafiki. Katika kadi za mchango tano naweza pata labda moja tu toka kwa mwanaume.
Hapa kwa kweli nikiangalia na kutafakari kutusua itakuwa ngumu sana, niko social hivyo wigo wangu ndugu, jamaa na marafiki ni mkubwa na hawasiti kunipa kadi.
Wenzangu mlio katika hali kama yangu mnafanyaje?
Kwenye harusi unaambiwa bajeti isipungue mil 20 alafu ndoa zingine unaona kabisa zinaenda kuwa matatani.
Mkuu hakuna point uliyoacha hapo...naomba nikunukuu; "sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako,na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usio yaweza."mwisho wa kunukuu.Uamumuzi ni wako kuweka vipaumbele katika maisha yako, hata hivyo namna ulivyo ji-brand kwa jamii yako ndo inakufanya uwe hivyo. Binafsi, sitoi kipaumbele kwenye michango ya harusi, na ukinipa kadi andika maumivu, mara nyingi sitoi kabisa au natoa kiasi kidogo sana kama 10000 hivi, maana sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako, na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usiyo yaweza. Lakini upande mwingine, huwa nazingatia sana swala la matatizo, kama ajari, ugonjwa, vifo, na shida zingine ambazo mtu hajitakii mwenyewe na zinakuja bila kujali hali zetu za kiuchumi.
Word!mkuu kuwa kama mimi tu sitaki kadi niambie unaoa au unaolewa niamue mwenyewe kuchangia au lah.. usinipe mkadi wako ukanitia stress na watu wengi wanaelewa hivyo huwa wananifanyia hivyo so sina kadi .... me sitachangisha mtu kwenye sherehe yoyote.. tukutane kwenye michango muhimu ya kufiwa, maradhi na nk nitachangia