Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Neema iwe kwenu.
Michango ya harusi inanirudisha nyuma kimaendeleo. Nina kibarua mahali na ninalipwa hela ndogo tu wala haizidi laki 8, sasa kila nikiibajeti kufanya mambo yangu nakutana na kadi ya mchango wa harusi (kitchen party, send off etc). Halafu cha kushangaza ni kwamba hizi kadi za michango zinatoka nyingi kwa wanawake ambao ni ndugu, jamaa na marafiki. Katika kadi za mchango tano naweza pata labda moja tu toka kwa mwanaume.

Hapa kwa kweli nikiangalia na kutafakari kutusua itakuwa ngumu sana, niko social hivyo wigo wangu ndugu, jamaa na marafiki ni mkubwa na hawasiti kunipa kadi.

Wenzangu mlio katika hali kama yangu mnafanyaje?
 
Ukichukua michango ya harusi iliyotolewa hapa nchini Tanzania kwa mwaka huu unaoishia unaweza kukuta kama taifa tukanunua Bombadier nyingine 2 au 3. Kupanga ni kuchagua.
 
Siku hizi akina mama wanalazimishana kuchangia mpaka sherehe za watoto wao kuhitimu vyuo vikuu!! Sherehe tu sijawahi kusikia wanachangia kwa mgonjwa amvaye hana uwezo wa kulipia matibabu au wanafunzi ambao ni yatima au wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia karo - akili zote zipo kwenye sherehe, tofauti kabisa na wenzetu wa Kenya.
 
Kwenye harusi unaambiwa bajeti isipungue mil 20 alafu ndoa zingine unaona kabisa zinaenda kuwa matatani.
 
Na ni wakumbushaji wazuri sana wa tarehe ya mwisho.
 
Neema iwe kwenu.
Michango ya harusi inanirudisha nyuma kimaendeleo. Nina kibarua mahali na ninalipwa hela ndogo tu wala haizidi laki 8, sasa kila nikiibajeti kufanya mambo yangu nakutana na kadi ya mchango wa harusi (kitchen party, send off etc). Halafu cha kushangaza ni kwamba hizi kadi za michango zinatoka nyingi kwa wanawake ambao ni ndugu, jamaa na marafiki. Katika kadi za mchango tano naweza pata labda moja tu toka kwa mwanaume.

Hapa kwa kweli nikiangalia na kutafakari kutusua itakuwa ngumu sana, niko social hivyo wigo wangu ndugu, jamaa na marafiki ni mkubwa na hawasiti kunipa kadi.

Wenzangu mlio katika hali kama yangu mnafanyaje?
Uamumuzi ni wako kuweka vipaumbele katika maisha yako, hata hivyo namna ulivyo ji-brand kwa jamii yako ndo inakufanya uwe hivyo. Binafsi, sitoi kipaumbele kwenye michango ya harusi, na ukinipa kadi andika maumivu, mara nyingi sitoi kabisa au natoa kiasi kidogo sana kama 10000 hivi, maana sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako, na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usiyo yaweza. Lakini upande mwingine, huwa nazingatia sana swala la matatizo, kama ajari, ugonjwa, vifo, na shida zingine ambazo mtu hajitakii mwenyewe na zinakuja bila kujali hali zetu za kiuchumi.
 
Kwenye harusi unaambiwa bajeti isipungue mil 20 alafu ndoa zingine unaona kabisa zinaenda kuwa matatani.

Ambacho unishangaza zaidi ni pale wanapo toa mashariti kwamba michango hisiwe chini ya elfu hamsini - michango ya hiari inakuwa na mashariti tena.
 
Sio mchezo ndoa zinatisha...
Ila hamna namna watu lazima waoane...

[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#BringBaCkBenAlive[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PumzikaKwaAmaniDenaAmsi[/HASHTAG]
 
Hilo ni tatizo kwa watanzania, kwakuwa uwezo wao wengi wa kufikiri haufanani na elimu zao wanajikuta wakipenda sifa sana.
Starehe yako wewe why usumbufu kwa wengine?.
Katu sihitaji michango kwenye hharusi yangu, itafanyika sawa na uwezo wangu. Mwenye kitu ataleta kama zawadi
 
mkuu kuwa kama mimi tu sitaki kadi niambie unaoa au unaolewa niamue mwenyewe kuchangia au lah.. usinipe mkadi wako ukanitia stress na watu wengi wanaelewa hivyo huwa wananifanyia hivyo so sina kadi .... me sitachangisha mtu kwenye sherehe yoyote.. tukutane kwenye michango muhimu ya kufiwa, maradhi na nk nitachangia
 
kila anaeomba mchango anaona yeye ndiye ameomba,

kwa mantiki hiyo, kila atakaenyimwa atajiona yeye ndiye amenyimwa, hawashirikiani kuleta kadi.

achana na hizo habari kila anaeleta kadi mkache, hata demu akijirahisi huitwa malaya, we usione aibu, michango yenyewe mtu hakukabi hapo hapo!

akikupa kadi mwambie " hii kadi umeipoteza bure"

usipompa hakuna kinacho...
 
Uamumuzi ni wako kuweka vipaumbele katika maisha yako, hata hivyo namna ulivyo ji-brand kwa jamii yako ndo inakufanya uwe hivyo. Binafsi, sitoi kipaumbele kwenye michango ya harusi, na ukinipa kadi andika maumivu, mara nyingi sitoi kabisa au natoa kiasi kidogo sana kama 10000 hivi, maana sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako, na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usiyo yaweza. Lakini upande mwingine, huwa nazingatia sana swala la matatizo, kama ajari, ugonjwa, vifo, na shida zingine ambazo mtu hajitakii mwenyewe na zinakuja bila kujali hali zetu za kiuchumi.
Mkuu hakuna point uliyoacha hapo...naomba nikunukuu; "sherehe ni jambo la kupanga na ni vyema kupanga sherehe kulingana na uwezo wako,na sio kusumbua wengine kwa kutaka mambo makubwa usio yaweza."mwisho wa kunukuu.
 
Swali ulishaoa au kuolewa je ulichangiwa? kama ulichangiwa kwanini usichangie wenzako
 
Hakuna anayekulazimisha uchange......

Kwani ukiwambia huna hela utabadilika rangi???????
 
kuna jamaa alikusanya michango ya harusi akaingia mitini kuanzisha mtaji wa biashara,ndoa akaenda kufungia bomani kusikokuwa na gharama kubwa
 
mkuu kuwa kama mimi tu sitaki kadi niambie unaoa au unaolewa niamue mwenyewe kuchangia au lah.. usinipe mkadi wako ukanitia stress na watu wengi wanaelewa hivyo huwa wananifanyia hivyo so sina kadi .... me sitachangisha mtu kwenye sherehe yoyote.. tukutane kwenye michango muhimu ya kufiwa, maradhi na nk nitachangia
Word!
 
Siku zote fanya kile ambacho moyo wako umependa kufanya hata kama mwingine aje akuchukie poa tu.
 
Back
Top Bottom