Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Nikero kubwa lakini maisha ya kiafrica ndivyoyalivyo tunachanga maana leo kwangu kesho kwako.
 
Wewe huwa unaomba michango kwa wenzako?
Kuna watu huona raha kusambaza kadi za kuomba michango lakini huona tabu kurudishiwa fadhila
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
Yaaani mda so mrefu imeingia sms ya kukumbushwa mchango
 

Kwani umelazimishwa mkuu!??
 
Habari wanajamvi,
Kuna tabia imezuka kwa wadada au wakaka wanaotarajia kuoa na kuolewa kudai michango ya sherehe zao bila hata maelezo.

Yani unakuta msg inaingia direct unaombwa mchango; hakuna salamu wala maelezo ya awali. Utakuta mtu mwingine ulisomaga nae chekechea hata hujui namba katoa wapi anaanza tu kudai mchango bila hata salamu dah.

Hii tabia inaboa sana, kuweni na hekima kidogo, salimia then elezea shida yako na hii tabia ya ndoa za kislamu kuanza kukomplicate kama wakilistu pia inaboa. Mtu anaitwa Ashura sijui Juma nae anakimbilia kuomba mchango, inahusu?

Kuoa uoe wewe hela ya sherehe nitoe mie how come? Halafu unaenda kwenye pati unakuta hakuna mvinyo ni soda na zile juisi zao. Yani huwa nawaza hela nitoe mie halafu napangiwa cha kunywa eti kisa mwenye sherehe ni mpendwa basi ungeomba mchango kwa wapendwa wenzako tu.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usichange tu. Mfano mm sitoi michango hivyo hivyo nikioa sitegemei kuomba hela hata kwa mzazi wangu wanisaidie. Show yote nitamaliza mwenyewe.
 
Hujaeleweka point yako unaelezea nn!! hupendi kuchangia harusi au hupendi kuchangia waislam?? kama unaona mtu amekutumia msg na huna pesa za kumchangia, unamwambia tu bro, hiyo sio court order lazima uitekeleze!! acha uswahili mkuu!! wenzako ambao wanacho watatoa!!
 
Ya nini kusumbua watu? ukiamua kuoa jitosheleze mwenyewe.Mbona miaka ya nyuma muoaji alijiweza peke yake? Michango ya harusi ni matumizi mabaya ya fedha.
 
Wewe ndio hujaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio hujaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Anyway hata kama sijaelewa point yako, lakini hiyo michango ya Harusi unayolalamikia, hujalazimishwa kutoa kama unacho unatoa huna unasema sina,,acha kulalamika JF, mimi binafsi nina kadi kama 5 na hua nachanga tu sioni cha ajabu, huo ni utamaduni mojawapo wa kujenga undugu na mshikamano kama ambavyo misiba coz harusi ni jambo la heri sio dhambi!!
 
si ungemwambia aliyekutumia sms kuwa humchangii kuliko kuja kulalama hapa jf aiseee hahahaaaaa
umeonaaa enheee!!! usikute yeye alichangiwa sasa wenzake wamemletea kadi anaona kero!!! hahahahha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…