Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Pengine niseme sasa wa tz tubadilike,tuanze fikiria sasa bajeti ndogondo za sherehe na hata kumbi na idadi ya wageni iwe ya chini ili tusiumizane kwenye michango!hali ni ngumu jamani,hali ni ngmu!!Kuna Kodi za nyumba,Ada,matumizi ya kawaida na mipango mingine ya kimaendeleo vyote vyataka pesa!
sasa ukitoa mchango harusi moja na nyingine baada ya wiki 2 mwwingine anaeta kadi...eeh ukiacha lawama mwaka unaenda mambo yako yanazotota!..jamani tuhurumiane..vyuma vimekaza mno!!
 
wanaanzia wapi kukupa kadi kama ukiwaambia kwamba hali yako sio nzuri...

mimi akinipa tu.. pale pale namwambia nina hali mbaya sana
 
Huwa nasema wazi harusi au sherehe yoyote sichangii ila ugonjwa au mtoto Shule utapata kwangu hata teni hukosi
 
Huwa nachangia kwa wale waliochanga kipindi naoa.
Uzuri karibu asilimia 90 ni ndugu wa ukoo mmoja.
Watu mpaka leo bado wanawaza bajeti za kushindana kwenye harusi!!
Huwa nawashauri vijana wenzangu ambao tunatoka halmashauri huko, usitafute umaarufu wa kuwa umefanyia sherehe jijini ukateseka kutafuta michango.
Huko waliko wazazi ni cheap na sherehe inakuwa nzuri sana tu.
 
wanaanzia wapi kukupa kadi kama ukiwaambia kwamba hali yako sio nzuri...

mimi akinipa tu.. pale pale namwambia nina hali mbaya sana
Mie kuna dada kabila langu ni mwalimu wa shule ya msingi, alinipa kadi ya send off ya mwanae ilikuwa mwaka 2015 nikamwambia niko vibaya, AMENINUNIA HADI NINAVYOTUMA HII COMMENT
 
Nitachanga kwa watu wangu wa muhimu tu.tena usiniwekee kima cha chini nitachanga ninachoweza kutoa na sio lazima unipe kadi ya mwaliko kwanza sio mpenzi wa masherehe yasiyokuwa na kichwa wala mguu,sherehe zenyewe zote zinafanana.na pia sina mpango wa kumchangisha mtu nitakapoamua kuoa.nitafunga ndoa masjid asubuhi sana,mchana inaandaliwa karamu isiyokuwa na kadi ya mwaliko free for all.jioni nasepa zangu na mamsap kuelekea honeymoon kokote nitakokuwa na uwezo nako iwe zanzibar au Bahamas.mambo ya kitchen party na send off hayapo kwenye ratiba zangu,mwali atafundwa na mashangazi kwenye semina elekezi.
 
Send off na kitchen party havikuhusu na wala huna maamuzi navyo ni vya upande wa mwanamke.

Wazazi wake wakiamuwa kumuanfalia sherehe ya kumuaga huna ubavu wa uhalali wa kuzuia, wewe utaalikwa tu kuhudhuria sherehe na some delegation yako.
 
Mkuu ndo maana nkasema hayapo kwenye ratiba yangu,siwezi kulazimisha zisifanyike,lakini sina wajibu nazo na zisipokuwepo itakuwa poa zaidi.
 
Mhubiri wa "Hatimaye maisha"yanayorushwa mubashara kutoka Mbeya alisikika akizungumzia kidogo suala la kujiepusha na gharama za arusi na kuangalia suala la elimu zaidi.
Nampongeza kama kiongozi wa kiroho kuzungumzia hilo,lakini alisema kidogo sana kuhusu aina hiyo ya "ujinga" ambao umekuwa ugonjwa wa wa Tanzania hasa wa imani ya kikristo.
Arusi zimekuwa ni kitu cha kuoneshana ufahari na mashindano ya matumizi makubwa ya pesa kwa ulevi na fahari za muda tofauti kabisa na uhalisia wa maisha ya walio wengi wanaoshiriki arusi hizi.

Ujinga unakuwa mkubwa zaidi pale mtu anapokuwa tayari kuchangia zaidi ya laki saba hadi milioni kwa mwaka kwa ajili ya arusi halafu anakataa kuchangia matibabu ama elimu kwa watoto wenye uhitaji.

Nawapongeza wakenya tangu enzi zile za mwl.Nyerere utasikia matangazo radioni "mbunge wa nyeri anaalika harambee ya kuchangia wanafunzi siku ya jumamosi"...

Matangazo hayo nikikumbuka japo nilikuwa mdogo,yanaonesha umakini wa wakenya katika suala la elimu.

Nilipokuwa mdogo nikisikia salamu katika vipindi vya watoto walikuwa na msemo " na maziwaa..ya watoto wa nyayo"

Viongozi waliona umuhimu wa lishe kwa watoto ili wawe makini na elimu.

Vipi suala la gharama hizi za arusi lisijadiliwe kwa kina na kubadilisha mind set za wa Tanzania kutoka kuchangia arusi na kufikiria kusaidia katika suala la elimu.

Bahati mbaya baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wanahimiza matumizi mabovu ya arusi za kifahari na wakati huo ndoa zinazofungwa nyingine hazidumu.

Imefika wakati wa kila mmoja wetu aanze kuangalia upya iwapo tunahitaji arusi za kifahari wakati tunakabikiwa na umaskini na ujinga ambao hatuungani kuutokomeza kama tunavyoungana wakati wa arusi.
 
Ifike mahali kila mtu agharamie harusi yake au ya ndugu yake bila kushirikisha watu wengi kama ilivyosasa.

Kwa kweli tuige mfano wa wenzetu kenya maharusi wanagharamia shughuli yao kwa msaada wa ndugu na marafiki wakaribu,lakini pia sherere za mchana zinapunguza mambo mengi jioni kila mtu kwake hakuna habari ya kukesha, mnapata chakula cha mchana na vinywaji laini visivyo na pombe, Maharusi kama wana uwezo basi watafanya tafrija fupi usiku ya watu wachache.

Hapa bongo usipo mchangia mtu unashangaa anakununia kabisa kwa kweli inabidi tubadilike

Ukienda kuomba msaada wa kuchangiwa ada hakuna ambaye atakusaidia ila peleka kadi ya mchango wa harusi watachanga hata kama wengine hawamjui muhusika.
 
E. Africa Tz inachukua no one kwa michango ya arusi na ya mwisho katika michango ya maendeleo hasa elimu. Utasikia fulani alitumia million kadhaa katika harusi, beer na chakula watu waliacha. Tuachane na ufahari uchwara tujikite kwenye elimu na mambo yenye tija
 
Ndugu wanajuwa huwa nachangia shule, ugonjwa na kifo otherwise no eti send nini ndo nitoe hela subuuutuuuuu.
 
Waache wenye uwezo wa kifedha waendelee kuchangiana,wewe kama huna shauri yako,binadamu hawafanani usiwasemee watu,usisema twafa sema nafa,mtu anaeingiza sh mil 3 kwa mwezi simi kama ni tatizo kwake kuchangia harusi kiwango chochote,tatizo letu tu wavivu na waoga wakuchangamkia fursa,kazi kubwa ni kubet mda wote.
 
Back
Top Bottom