Ndoa za mwendokasi zimekuwa ni nyingi sana skuizi, vijana wamekuwa wanamuamko wa ajabu kuowa bila kujiandaa mwishowe wanakuja kusumbua watu, Alafu unapewa kadi ya mchango yenye kiwango cha mwisho kabisa cha mchango yaani unaambiwa usitoe chini ya 100,000.
Nimeshawachangia mabest zangu wengi nilisoma nao miaka ya nyuma, nakumbuka nishawachangia mabest zangu kama 40 hivi na kati ya hao 15 ndoa zao zimeshavunjika tena ndani ya mda mfupi tu tokea wafunge ndoa
Na wengine wamekuwa ni matapeli kama yule mzee Kokobanga wa kule Instagram, wanaomba michango ukishawachangia wanaingia mitini na ndoa hamna hela wanakula, ifike mahali sasa kila mtu apambane na hali yake, ukitaka kuowa nenda kanisani au msikitini na mpenzi wako kimya kimya fungeni ndoa yenu na maisha yaendelee, mambo ya michango michango yamekuwa mengi alafu ndoa zenyewe hazidumu mnachezea hela za watu tu