Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Ndoa za mwendokasi zimekuwa ni nyingi sana skuizi, vijana wamekuwa wanamuamko wa ajabu kuowa bila kujiandaa mwishowe wanakuja kusumbua watu, Alafu unapewa kadi ya mchango yenye kiwango cha mwisho kabisa cha mchango yaani unaambiwa usitoe chini ya 100,000.

Nimeshawachangia mabest zangu wengi nilisoma nao miaka ya nyuma, nakumbuka nishawachangia mabest zangu kama 40 hivi na kati ya hao 15 ndoa zao zimeshavunjika tena ndani ya mda mfupi tu tokea wafunge ndoa

Na wengine wamekuwa ni matapeli kama yule mzee Kokobanga wa kule Instagram, wanaomba michango ukishawachangia wanaingia mitini na ndoa hamna hela wanakula, ifike mahali sasa kila mtu apambane na hali yake, ukitaka kuowa nenda kanisani au msikitini na mpenzi wako kimya kimya fungeni ndoa yenu na maisha yaendelee, mambo ya michango michango yamekuwa mengi alafu ndoa zenyewe hazidumu mnachezea hela za watu tu
Brother' yaani ni hatari kweli kweli, leo nafika home napewa kadi na vijana eti kuna mwalimu mtaa wa pili ana send off. Na akasisitiza kuwa anatufahamu ndo maana ameleta na kwa kumbukumbu na ubize wetu hakuna MTU wa hivyo .

Hivi jamani unapata wapi ujasiri wa kupeleka kadi ya michango kwa MTU ambaye hata hamna mazoea au ukaribu? Kwa ukata huu wa sasa ni heri lawama ebooo?
 
Najiulizaga mara mbilimbili kweli...

Nitoe laki ya kwenda kukesha na kulishana mavyakula usiku wa manane au niende kwa wakala fasta nikalipie wanangu transport fee.

The conscious part part of my brain choose the latter...

Ifike mahala kila mtu apambane na hali yake.
 
Brother' yaani ni hatari kweli kweli, leo nafika home napewa kadi na vijana eti kuna mwalimu mtaa wa pili ana send off. Na akasisitiza kuwa anatufahamu ndo maana ameleta na kwa kumbukumbu na ubize wetu hakuna MTU wa hivyo .

Hivi jamani unapata wapi ujasiri wa kupeleka kadi ya michango kwa MTU ambaye hata hamna mazoea au ukaribu? Kwa ukata huu wa sasa ni heri lawama ebooo?
[emoji23][emoji23]
 
Bora hata huo wa harusi Mimi Nina kadi za kuwaaga wastaafu na mchango ni jiwe (100,000/) hakuna cha double wala single kumuaga mstaafu jamani ndio kwa style hiii...??? Yeye anaenda kula pensheni cc tunaumia
Mkuu Kuna watu wanapenda sherehe kama nini.
Kuna mkoa idara ya afya walipohamishiwa wizarani walilazimishwa kufanya sherehe ya kuwaaga wanaobaki tamisemi.
Yaani ni aibu Mambo tunayoyafanya.

Wengine wanafanya sherehe ya kumuaga mtu anayehama.
Ni upuuzi mtupu. Kisa alikuwa boss.
 
Mimi haya mambo nilishajikomboa nayo long time. Meseji za michango na makundi ya whatssap niliyounganishwa bila taarifa huwa naangalia kama sioni. Kama ni mtu wa ofsin au MTU wa karibu nikitoa 25 ya kupunguza ndo nitolee. Ni ushenzi kwasababu mtu akitaka kujenga anakopa, gari anakopa mke wake anayelala nae uchi kila siku tunasumbuana kisa ana namba yako ya simu. Mimi hacha niwe anti social kwa hili. Ukitaka kuoa kama hujajipanga subiri au nenda benki kakope ufanya utapanyaji vzr.
 
watu wanaoana ili wakakulane wenyewe hlf wanakuja omba michango sa kama hawana pesa za harusi c ndoa za mikeka ipo
 
Mkuu Kuna watu wanapenda sherehe kama nini.
Kuna mkoa idara ya afya walipohamishiwa wizarani walilazimishwa kufanya sherehe ya kuwaaga wanaobaki tamisemi.
Yaani ni aibu Mambo tunayoyafanya.

Wengine wanafanya sherehe ya kumuaga mtu anayehama.
Ni upuuzi mtupu. Kisa alikuwa boss.
Hiyo ipo ofisini kwetu. Boss wetu aliteuliwa kuongoza taasisi fulani kama General Director kutoka kwenye taasisi ambayo nafanyia kazi yaani huwezi amini tangu ateuliwe March 2018 kuna watu wakaunda kamati ya sherehe ya kumuaga. Huwezi amini inasogezwa mpaka leo pesa haijawahi kupatikana.
 
Hii ishakua kero kubwa sana mi nna kadi kama 6 na mbili mchango ni kuanzia laki,nimesema sichangi bora lawama kuliko fedheha sitaki kufedheheka kwa kulala njaa kisa kutoa mchango wa harusi
 
Yani kama mbwai na iwe hivyo, kila mtu apambane na hali yake
 
Hapa nashindwa kufanya maamuzi , nina kadi 5, Majirani zangu 2,Bosi wangu wa Zamani,Mjumbe mwezangu wa Bodi, Mwanafunzi wangu.
Harusi zote mwezi wa Kumi. Nataka kuchanga kwa watu wawili tu sijui nimchangie nani nimwache nani?
 
Naunga mkono hoja. Sio lazima kufanya sherehe. Oa/olewa kanisani/msikitini kisha mshukuru Mungu endelea kutafuta maisha.

Unaletewa kadi eti kima cha chini 60,000 sijui. Hiyo hela uliweka wewe mfukoni mwangu??

Kila mtu apambane na hali yake.
 
Back
Top Bottom