jogoo mweupe
Member
- Jun 29, 2018
- 10
- 13
Tuoneane huruma sisi kwa sisi jamani hali ni ngumu sana kitaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Brother' yaani ni hatari kweli kweli, leo nafika home napewa kadi na vijana eti kuna mwalimu mtaa wa pili ana send off. Na akasisitiza kuwa anatufahamu ndo maana ameleta na kwa kumbukumbu na ubize wetu hakuna MTU wa hivyo .Ndoa za mwendokasi zimekuwa ni nyingi sana skuizi, vijana wamekuwa wanamuamko wa ajabu kuowa bila kujiandaa mwishowe wanakuja kusumbua watu, Alafu unapewa kadi ya mchango yenye kiwango cha mwisho kabisa cha mchango yaani unaambiwa usitoe chini ya 100,000.
Nimeshawachangia mabest zangu wengi nilisoma nao miaka ya nyuma, nakumbuka nishawachangia mabest zangu kama 40 hivi na kati ya hao 15 ndoa zao zimeshavunjika tena ndani ya mda mfupi tu tokea wafunge ndoa
Na wengine wamekuwa ni matapeli kama yule mzee Kokobanga wa kule Instagram, wanaomba michango ukishawachangia wanaingia mitini na ndoa hamna hela wanakula, ifike mahali sasa kila mtu apambane na hali yake, ukitaka kuowa nenda kanisani au msikitini na mpenzi wako kimya kimya fungeni ndoa yenu na maisha yaendelee, mambo ya michango michango yamekuwa mengi alafu ndoa zenyewe hazidumu mnachezea hela za watu tu
[emoji23][emoji23]Brother' yaani ni hatari kweli kweli, leo nafika home napewa kadi na vijana eti kuna mwalimu mtaa wa pili ana send off. Na akasisitiza kuwa anatufahamu ndo maana ameleta na kwa kumbukumbu na ubize wetu hakuna MTU wa hivyo .
Hivi jamani unapata wapi ujasiri wa kupeleka kadi ya michango kwa MTU ambaye hata hamna mazoea au ukaribu? Kwa ukata huu wa sasa ni heri lawama ebooo?
Msalimie Deborababa debora nilimkataza kuchangisha kwenye harusi yetu. nikamwambia kama hawezi kukomaa mwenyewe kugharamia shuguli basi ndoa IFE. Mbona alikomaa na ubwabwa tukala. Tuna maisha yetu mazuri tu, Debora mzuri.
Mkuu Kuna watu wanapenda sherehe kama nini.Bora hata huo wa harusi Mimi Nina kadi za kuwaaga wastaafu na mchango ni jiwe (100,000/) hakuna cha double wala single kumuaga mstaafu jamani ndio kwa style hiii...??? Yeye anaenda kula pensheni cc tunaumia
Hahahahahahaha AmiinLaki moja mara 40 = 4,000,000! Hii ni sawa na gharama ya kununua tofali elfu nne za block. Kama umechanga pesa hii yote ihali bado unakaa kwenye nyumba ya kupanga, basi nakuombea rehema kwa Mwenyezi Mungu. Siku ukifa uingie Peponi moja kwa moja...
Hiyo ipo ofisini kwetu. Boss wetu aliteuliwa kuongoza taasisi fulani kama General Director kutoka kwenye taasisi ambayo nafanyia kazi yaani huwezi amini tangu ateuliwe March 2018 kuna watu wakaunda kamati ya sherehe ya kumuaga. Huwezi amini inasogezwa mpaka leo pesa haijawahi kupatikana.Mkuu Kuna watu wanapenda sherehe kama nini.
Kuna mkoa idara ya afya walipohamishiwa wizarani walilazimishwa kufanya sherehe ya kuwaaga wanaobaki tamisemi.
Yaani ni aibu Mambo tunayoyafanya.
Wengine wanafanya sherehe ya kumuaga mtu anayehama.
Ni upuuzi mtupu. Kisa alikuwa boss.
[emoji23][emoji23]watu wanaoana ili wakakulane wenyewe hlf wanakuja omba michango sa kama hawana pesa za harusi c ndoa za mikeka ipo
[emoji23][emoji23]Hiyo ipo ofisini kwetu. Boss wetu aliteuliwa kuongoza taasisi fulani kama General Director kutoka kwenye taasisi ambayo nafanyia kazi yaani huwezi amini tangu ateuliwe March 2018 kuna watu wakaunda kamati ya sherehe ya kumuaga. Huwezi amini inasogezwa mpaka leo pesa haijawahi kupatikana.
Yani kama mbwai na iwe hivyo, kila mtu apambane na hali yakeHii ishakua kero kubwa sana mi nna kadi kama 6 na mbili mchango ni kuanzia laki,nimesema sichangi bora lawama kuliko fedheha sitaki kufedheheka kwa kulala njaa kisa kutoa mchango wa harusi
Kuna Jamaa alitufanyia hivo..... ila yeye akasepa na michango India, kaenda kupiga shule! Nilimuelewa sana yule Jamaa!Nikitaka Mtaji natafuta tapeli mwenzangu wa kike nakusanya michango ya harusi kisha naenda Njombe kulima Maparachichi.
Hahahaha anaendelea vyema na masomo kweli?Kuna Jamaa alitufanyia hivo..... ila yeye akasepa na michango India, kaenda kupiga shule! Nilimuelewa sana yule Jamaa!