Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Ndoa za mwendokasi zimekuwa ni nyingi sana skuizi, vijana wamekuwa wanamuamko wa ajabu kuowa bila kujiandaa mwishowe wanakuja kusumbua watu, Alafu unapewa kadi ya mchango yenye kiwango cha mwisho kabisa cha mchango yaani unaambiwa usitoe chini ya 100,000.

Nimeshawachangia mabest zangu wengi nilisoma nao miaka ya nyuma, nakumbuka nishawachangia mabest zangu kama 40 hivi na kati ya hao 15 ndoa zao zimeshavunjika tena ndani ya mda mfupi tu tokea wafunge ndoa

Na wengine wamekuwa ni matapeli kama yule mzee Kokobanga wa kule Instagram, wanaomba michango ukishawachangia wanaingia mitini na ndoa hamna hela wanakula, ifike mahali sasa kila mtu apambane na hali yake, ukitaka kuowa nenda kanisani au msikitini na mpenzi wako kimya kimya fungeni ndoa yenu na maisha yaendelee, mambo ya michango michango yamekuwa mengi alafu ndoa zenyewe hazidumu mnachezea hela za watu tu
acha uvivu wewe kubwa zima unaogopa kuchanga laki utakuwa ulioa ndoa ya mkeka tu kwa mawazo haya mgando
 
Ngoja tu kutakuja kadi za michango hadi mtoto kutolewa kipaimara
Siku zaja tu
 
Kwa kwel michango ya harusi imezid...alafu sasa kuna wale anakuomba mchango hadi unakasirika mana mtu anakua kama analazimisha sasa...jaman kama nnayo ntakupa kama sina pia bas mana sio lazma....Inaboa sana
 
Sipingi kuwa sisi binadamu tunahitajiana kwa ajili ya masuala ya kijamii. Ila jambo muhimu hapa, Je ni suala lipi la kijamii unahitaji kushiriki kulingana na uwezo wako kiuchumi.?

Haiingii akilini mtu mwenye kipato cha Tshs. 450,000 kwa mwezi, halafu umtake mtu huyo kuchangia zaidi ya michango mitatu ya harusi kila mwezi yenye kuanzia Tshs. 50,000/= - 200,000/=.

Je, tunafahamu vipaumbele vyetu kimaisha kulingana na uwezo wetu kiuchumi.?

Maisha haya ya kiafrika tuliyonayo, ambayo kwa kiasi kikubwa vipato vyetu ni duni, inahitaji sana kuwa na vipaumbele katika matumizi yako ya fedha unazofanikiwa kuzipata.

Kwa maoni yangu, miongoni mwa vipaumbele muhimu ni pamoja na chakula, matibabu, mavazi na malazi.

Sasa unakuta mtu hata tu kuwa na kipato cha kumudu chakula kwa mwezi hana kisha umtake achangie michango ya harusi yenye thamani kuanzia laki moja kwa mwezi, Je, huu ni uungwana.? Achilia mbali kuhusu uwezekano wa kumudu mahitaji mengine muhimu kama mavazi, matibabu na malazi. Hapo nimeongelea chakula tu.

Najua wapo watu watasema, si uwe unaacha kuchangia kwani unalazimishwa.? Hivi utajisikiaje mtu unayefanya naye kazi ofisi moja, mwingine umesoma naye, mwingine umekutana naye katika matukio muhimu na kisha kufahamiana naye, utajisikiaje akikupa kadi ya mchango na kisha kumchunia tu bila kumchangia.?

Nini Kifanyike.?

Utamaduni wa kufunga ndoa na kufanya sherehe si utamaduni mbaya lakini uendane na kipato cha muhusika.

Kama jamii unayoishi ipo katika nafasi nzuri kiuchumi, ni jambo zuri kuishirikisha jamii hiyo ili wakuunge mkono kwa namna moja au nyingine maana jamii ya watu wenye kipato kizuri cha fedha inamanisha imeshatoka kwenye kiwango cha kumudu mahitaji muhimu na kuelekea kwenye matumizi ya ziada kama vile anasa n.k

Kama jamii unayoishi ni ile yenye kumudu matumizi ya mahitaji ya msingi kama vile chakula, malazi, matibabu na mavazi basi usiishurutishe jamii hiyo kukuchangia ilihali unafahamu kabisa hata wakichanga watachanga huku wakiumia moyoni. Katika hili tusipeane moyo kuwa kutoa ni moyo na usambe si utajiri.Moyo upi huo wa kutoa laki moja kufanikisha sherehe ya harusi ya mtu huku nyumbani kwako hakuna chakula.?

Ni vema tuwe na utamaduni wa kufanya maandalizi mapema kupitia rasilimali zako mwenyewe kama unaona ni lazima ufanye sherehe yako ya ndoa. Ili badala ya kuwachangisha watu , wewe ndiye utoe fedha zako za akiba na kuwakaribisha watu kushiriki sherehe hiyo bila kuwalazimisha kukuchangia kwanza.

Ni vema tukazingitia kuwa, kufunga ndoa si lazima ufanye sherehe. Bado utahesabika umeoa/kuolewa hata kama ulimefunga ndoa bila kufanya sherehe.

Mbaya zaidi, unatoa mchango wa harusi laki moja, mbili, au hata tano ila linapokuja suala la kumchangia mgonjwa anayehitaji matibabu unaona anastahili Sh 2000/= au 5000/=

Je, huu ni uungwana.???
 
Sipingi kuwa sisi binadamu tunahitajiana kwa ajili ya masuala ya kijamii. Ila jambo muhimu hapa, Je ni suala lipi la kijamii unahitaji kushiriki kulingana na uwezo wako kiuchumi.?

Haiingii akilini mtu analipwa Tshs. 450,000 kama mshahara wake kwa mwezi, halafu umtake mtu huyo kuchangia zaidi ya michango mitatu ya harusi kila mwezi yenye kuanzia Tshs. 50,000/= - 200,000/=.

Je, tunafahamu vipaumbele vyetu kimaisha kulingana na uwezo wetu kiuchumi.?

Maisha haya ya kiafrika tuliyonayo, ambayo kwa kiasi kikubwa vipato vyetu ni duni, inahitaji sana kuwa na vipaumbele katika matumizi yako ya fedha unazofanikiwa kuzipata.

Kwa maoni yangu, miongoni mwa vipaumbele muhimu ni pamoja na chakula, matibabu, mavazi na malazi.

Sasa unakuta mtu hata tu kuwa na kipato cha kumudu chakula kwa mwezi hana kisha umtake achangie michango ya harusi yenye thamani kuanzia laki moja kwa mwezi, Je, huu ni uungwana.? Achilia mbali kuhusu uwezekano wa kumudu mahitaji mengine muhimu kama mavazi, matibabu na malazi. Hapo nimeongelea chakula tu.

Najua wapo watu watasema, si uwe unaacha kuchangia kwani unalazimishwa.? Hivi utajisikiaje mtu unayefanya naye kazi ofisi moja, mwingine umesoma naye, mwingine umekutana naye katika matukio muhimu na kisha kufahamiana naye, utajisikiaje akikupa kadi ya mchango na kisha kumchunia tu bila kumchangia.?

Nini Kifanyike.?

Utamaduni wa kufunga ndoa na kufanya sherehe si utamaduni mbaya lakini uendane na kipato cha muhusika.

Kama jamii unayoishi ipo katika nafasi nzuri kiuchumi, ni jambo zuri kuishirikisha jamii hiyo ili wakuunge mkono kwa namna moja au nyingine maana jamii ya watu wenye kipato kizuri cha fedha inamanisha imeshatoka kwenye kiwango cha kumudu mahitaji muhimu na kuelekea kwenye matumizi ya ziada kama vile anasa n.k

Kama jamii unayoishi ni ile yenye kumudu matumizi ya mahitaji ya msingi kama vile chakula, malazi, matibabu na mavazi basi usiishurutishe jamii hiyo kukuchangia ilihali unafahamu kabisa hata wakichanga watachanga huku wakiumia moyoni. Katika hili tusipeane moyo kuwa kutoa ni moyo na usambe si utajiri.Moyo upi huo wa kutoa laki moja kufanikisha sherehe ya harusi ya mtu huku nyumbani kwako hakuna chakula.?

Ni vema tuwe na utamaduni wa kufanya maandalizi mapema kupitia rasilimali zako mwenyewe kama unaona ni lazima ufanye sherehe yako ya ndoa. Ili badala ya kuwachangisha watu kisha wewe ndiye utoe fedha zako za akiba na kuwakaribisha watu kushitriki sherehe hiyo bila kuwalazimisha kukuchangia kwanza.

Ni vema tukazingitia kuwa, kufunga ndoa si lazima ufanye sherehe. Bado utahesabika umeoa/kuolewa hata kama ulimefunga ndoa bila kufanya sherehe.

Mbaya zaidi, unatoa mchango wa harusi laki moja, mbili, au hata tano ila linapokuja suala la kumchangia mgonjwa anayehitaji matibabu unaona anastahili Sh 2000/= au 5000/=

Je, huu ni uungwana.???

Nakubaliana nawe, ila subiri uchangie kwangu kwanza
 
nliacha baada ya kujikuta nna kadi5 mikoa 3tofauti af mi mwenyewe npo mkoa mwingine so 350k zkawa zmepotea bure
ila asaiv nachangia harusi ntayoweza kuudhuria!! tena watu nnaowafahamu tuu
 
Unakuta mtu anataka harusi ya millions 21 na yeye hana hata million 2, inachekesha sana,,

Unakuta mtu kiguu na njia kufuata michango, ikifika siku ya tukio kachoka Kapauka mpaka bas,

Mhimu kujikubali na kuishi mazingira uliyo nayo,,,
 
Nani aliwahi shikiwa fimbo achange kama umeona mtu sio wa muhimu kwako usichangeee sio LAZIMA acheni kutupigia kelele humu kila siku[emoji21][emoji41]
 
Unakuta mtu anataka harusi ya millions 21 na yeye hana hata million 2, inachekesha sana,,

Unakuta mtu kiguu na njia kufuata michango, ikifika siku ya tukio kachoka Kapauka mpaka bas,

Mhimu kujikubali na kuishi mazingira uliyo nayo,,,
Dah harusi ni stress
 
...wanao uaaa bendi ni wale wanaokusanya michangoo Mjiniii....kisha anaenda fanyia sherehe kijijiniii...big up kwaoooo wakirudi mujini wanawekeza etc
 
Back
Top Bottom