Bro wewe kama kweli ni msomi basi usomi wako huutendei haki.Nina wazo nataka kuchangia,swala la ndoa ni deni kwa mwenyezi mungu hivyo kila mtu lazima afunge ndoa,ili tuepukane na uzinifu,na swala la mtu asichangishe watu eti kisa raha atapata yeye mimi binafsi naona ni roho ya kimaskini na choyo na pia kujifanya tumeelimika sana bila kujali kuwa ni upuuzi kwa kuongea swala ambalo watu waliosoma wenzio wakilichambua wanakuona umetoa uzi wa kipuuzi,uchumi wa nchi,mifuko imetoboka,hali mbaya lazima mtu achangishe kwa wadau wake wakaribu na si lazima unaweza usitoe,kuna swala la kadi,mtu anasambaza kadi kwa watu wa karibu sana ambao ni uhakika na waliokaribu lakini sio sana sana ambao sio wa uhakika sana zinaitwa kadi za kubahatisha sasa nadhani wewe mtoa mada upo kundi la pili la watu wa kubahatishwa
Watu mnataka sifa sana na hii ndio inawapelekea kufanya huu ijinga wa harusi ambazo hamna uwezo nazo kisha unaanza kusumbua kila unaemjua.
Hakuna msomi anayeweza kusanya from 1M to any amount for months kisa akaisaga ndani ya saa halafu ukasema huyo ni msomi(huyo mwite mjinga).
Ndoa ni pale unapofungiwa kanisani /msikitini .
Mtu unatumia milioni 10 ndani ya masaa halafu kesho unaanza kusumbua watu wakukope huu ni ujinga wa kutaka sifa