Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Safi sana. Bora ndoa simple miaka hii.maana mnagaramia halafu siku mbili.mnaachana au michepuko inakuwa deal. Ya nini ndoa za eti budget 50 or 100m halafu kesho yake aibu? Think twice before you decide.
 
Na kwawasio sali kanisani vipi?

tena hao ndo simple balaaa... ndoa inafungwa na mashehe baada ya hapo watu wanakunywa maji kila mtu kwake... then muoaji anaruhusiwa kwenda kuoa kwingine kama inawezekana siku hiyo hiyo.
 
Mi kiukweli wazazi wangu washachanga sn ila nikaona sio issue.
Ctaki kumchangisha mtu!

Ht mwanaume wangu Nitamwambia na tukubaliane no kamati, ndugu wa karibu tu tunawapa plan yetu tunataka iweje basi.
Tunafanya kutokana na uwezo uliopo
Na ikitokea imechangwa pesa kwa watakaotaka kuchanga bajeti ni ile ile hyo nyingine bora tufanyie mambo ya muhimu. ...
Mambo ya kufanya sherehe kubwa baada ya sherehe mnaanza kuhangaika maisha magumu ctaki kabisa.
Mungu akubariki na kukusaidia ubaki na msimamo huu na wala usiyumbishwe na mtu yeyote
 
Kuwa na msimamo mmoja tu wa kutochangia. MIMI nilichaacha hayo makitu kitambo na ndugu zangu na marafiki huwa hawajisumbui kunipa kadi za mchango, sababu wote wanajua msimamo wangu. Kama kuna tatizo jingine sina tatizo. Ndoa ufunge wewe fedha tukuchangie sisi kwa starehe zako. Big NO.

Itabidi nijifunze huu msimamo wako.

Harusi za mwezi huu tu, imeni cost laki tano. Kuna send off inanukia next month!

Ni bora kuonana wabaya!
 
Hii michango ni ni majanga .Arusi mchango ,ubarikio mchango .komunyoo mchango ,kipaimara mchango ,send off mchango ,misiba mchango kuhusu misiba Sina tatizo la kuchangia maana ukipaata matatizo wanasema ngoja akazike mwenyewe .

Umesahau na basidei
 
Nachangia msiba tu tena bila kuambiwa hizo zingine naipulia sufuria jikoni
 
Mtoa hoja usijinasibishe nao hyo nd njia rahisi na pekee na usiwe mnafiki ktk Maisha
Wew jipambanue ktk Maisha km mm kwamba sichangii aina yoyote ya sherehe' hakuna atakaekuletea kadi na hata km wakileta unawaambia kbsa m sichangii haruc km una shida, matatizo, Majanga njoo at usiku wa manane niamshe km nna uwezo ntakusaidia' Asa we rafk angu kadi unaletewa unaipokea alf unkuja ap kuomba simpathy yetu, unatakaje xx wakikupa kadi uskumbushwe??! Ukipokea kadi maan ake imeingia kwenye bajeti kk! Jipambanue na jamii yko kaka! Au nd vile Maisha hayaendi bila unafiki...!!!
 
Bora michango hiyo ingekua KUMSOMESHA fulani, lakini kula na kunywa kwenye harusi tu....
SIPENDI.....

Hata mimi sipendi, huwa nazikwepa sana maana nimegundua ni kujiongezea umaskini. Kuna umuhimu wa kutafuta mbadala wa hili.
 
BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;
“Ndugu, rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika”, baada ya wiki meseji huwa kali zaidi;“Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu.”

Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.

Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.

Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele!

Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta.”

Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja na kinywaji round moja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi?

Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.

Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, “Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.

“Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.

“Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

“Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama waliopika sambusa hizi tulizokula kwa kweli zilikuwa tamu sana, kwa kweli leo ni furaha tupu. “MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali kuwa mc wa shughuli hii kwakweli upo vizuri, aksante sanaaaaa!

Yaani inamaanisha ela zetu za mchango sijui zilinunua nini maana kila kitu almost kilikuwa bure.. mnaoowa karibuni poleni msinihesabu.
 
hyo harusi au birthday? au usikute walioana watani wewe hujui tu! hahahhahaha
 
Hahahahha sasa kwanini unalipa faini au unamakosa gani??
 
hakuna haja ya kuchangishana these day......pumb....fu zao....
 
Pole sana ndugu kwa yote ambayo yalikukumba siku hiyo ya harusi. Lakini pia naomba nichangie machache kutokana na uzoefu wa watanzania wengi hasa wanapotoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha tukio fulani hasa sherehe (harusi). Kiasi kikubwa cha wachangiaji huwa na lengo la kuja kutumia pesa walizochangia na si kufurahia pamoja na maharusi na kuwatakia maisha mema na yenye furaha katika ndoa. Sasa wanapokutana na hali kama hii huwa wanaumia na kulalamika sana. Najua kila mtu ana madhaifu yake, na katika sherehe uwezi kumfurahisha kila mtu, cha msingi Ni kumezea tu unapoona mapungufu kama haya.
 
mkuu unapo nichangisha elfu hamsini single double elfu sabini nategemea bia nne na plate ya chakula yenye nyama nyingi na soda na maji na zawadi juu kama nilikuwa mwanakamati .. acha kabisa wanasumbua mpaka basi
 
Juzi kuna jamaa yangu hatukuwasiliana toka tumalize o level kanipigia simu.Nashangaa leo asubuhi kaniandikia msg ananialika kwenye kikao cha ufunguzi cha harusi yake.
 
Back
Top Bottom