Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

sichangi wala sitaki kuchangiwa,,nachangia misiba tuu harusi na mashereh mengine big no!
 
Mm nina daftari la walionichangia kwenye harusi yangu na nimelifanyia lumination kabisaaa..ninao wachangia ni wale walio nichangia..na nikimchangia ambaye hakunichangia (kama sio ndugu) basi ujue nina hamu na ubwabwa wa harusini
 
Mimi ninazo 11 na sichangii hapo yenyekima cha chini ni elfu 50. Zaidi ya laki 8 eti. Sina muda huo.
 
eti wakenya,hizi mambo za kuchangiashana kwa ajili ya harusi kwenu ipo?
 
Karibuni uislamu, hatuna hayo mambo.
Mimi ni muislamu, nataka nikwambie kuwa haya mambo si suala la dini bali ni suala la mtu binafsi. Kwa wakristo ndoa hufungwa kanisani yanayobaki yote ni mbwembwe na si lazima. Kwa waislam ndoa ni watu watano tu ambao ni;
1. Muoaji
2. Muolewaji
3. Baba/mjomba wa muolewaji
4. Shahidi wa kwanza
5. Shahidi wa pili.
Mambo mengine yoyote zaidi ya hapo ni mbwembwe tu sio lazima.
 
Ukweli ni kwamba mimi kwa ujumla si muumini wa michango ya harusi na kitchen party au sherehe kwa ujumla. Mm huwa napata shida sana kuchangia harusi wakati kuna jirani yangu analala njaa kwa kukosa pesa kidogo tu ya chakula. Huwa napata taabu sana kutoa alfu hamsini kwaajili ya harusi wakati kuna watanzania wanateseka kwa maradhi kwa kukosa alfu 30 tu ya dawa. Kwangu mimi ni bora nikaenda muhimbili wodi ya watoto nikaona japo watoto wawili kila mmoja nikampa alfu 50kuliko kuchangia harusi watu wakastarehe.

Kwa kifupi sina interest kabisa na mambo ya sherehe.
Sifa yangu mimi ni kuwachangia wenye shida si kuchangia sherehe. Aidha, zawadi za harusi nina uhuru wa kupeleke hata yenye thamani ya 5,000 au hata laki tano kwa kadiri nitakavoona inafaa.

Mimi si muhudhuriaji wa harusi, mara nyingi hupenda kushiriki harusi za ndugu zangu wa karibu na jamaa zangu wa karibu sana na family friends tu. Lakini hupenda kusaidia wenye shida bila kujali udugu, kabila wala dini. Ndivyo nilivyo. Watu wengi hunisema lakini mimi naishi nitakavyo. Ninayo mengi ambayo nimeamua kuishi kinyume na watu wanavolazimisha watu waishi, mfano, mimi hata siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei, hata ya mke wangu na hata ya mwanangu, wala hata neno happy birdhday huwa silitamki. Napenda kutumia masiku haya kwa kuwasapoti wenye shida. Sioni sababu ya mimi kutumia laki eti kusherehekea birthday ya mwanangu wakati kuna watoto chungu nzima wana malnutrition wamekosa hela kidogo kwa ajili ya kuimarisha lishe zao. Laiti, ukitafakari vzuri utatambua nini nasema na kwanini sichangii sherehe. Haya ni maisha yangu niliyoyachagua kuishi hapa duniani. Sitaki sifa kwa mtu, mimi natimiza lengo la kuumbwa kwangu na Mwenyezi MUNGU hapa duniani. I have dedicated my life to support the most in need. I know that i cant finish their problems but i will fullfill my part to the level that i can afford.
Maneno mazito na ya hekima sana. Kuna amani ya ajabu pale unapomsaidia mtu mwenye shida ambaye hakujui na inawezekana wala usimwone tena.

Kuna kipindi huko nyuma nililazwa Bugando. Nilikuwa peke yangu mbali na home bila pesa wala ndugu lakini mzee mmoja alikuwa akifika kila Jumatano kunijulia hali na kuniletea sabuni, matunda na vihela kidogo. Alikuwa anapita mawodini akiongea na wagonjwa na akikuona kweli una shida kabisa kabisa basi anakusaidia. Mpaka siku nafanyiwa operesheni alifika na kuniambia kuwa I was going to be OK. Nakaribia kuagwa nikamuomba anifahamishe jina lake na anakaa wapi akagoma. Aliniambia haina haja bali tu nikatende wema kwa wengine huko niendako. Mpaka leo huwa nalia nikimkumbuka na sijapata kumwona tena na sijui kama yungali hai kwani alikuwa mzee sana na miaka imepita 10+.

Mzee huyu ndo alinibadilisha nikawa na msimamo mkali kama wako. Mimi hata fungu la kumi kanisani sitoi bali napeleka mwenyewe moja kwa moja mahospitalini huko na kwenye majumba ya mayatima na masikini wengine. Sijui kama huwa nafanya kosa lakini moyo wangu hupata faraja ya kweli nikifanya hivyo badala ya kumpa mchungaji ambaye najua tayari ni bilionea. Na kama wewe harusi kwangu ni strictly kwa ndugu wa karibu tu basi. Na zamu yangu ikifika sitegemei kufanya harusi ya kifahari na sitegemei kumchangisha mtu.
 
Ndugu, nimebarikiwa sana na ushuhuda wako, ninaamini wengi watabarikiwa pia. Nikutie moyo tena ndugu yangu. Fungu lako la kumi peleka pale moyo unapokutuma upeleke. Mimi ni muislam lakini mafungu hayo huwa sipeleki msikitini, huwa napeleka pale moyo unaponituma nipeleke na mara nyingi huwa namshirikisha Mwenyezi MUNGU kwanza na hivyo huwa najikuta nimepeleka mahali sahihi. Katika kutoa kwangu siangalii dini wala huwa siulizi jambo hilo, ili mradi umeumbwa na Mwenyezi MUNGU na una shida basi mimi nipo tayari kumsaidia. Hebu nikushuhudie jambo moja kwa faida yako na wengine.

Siku moja mwisho wa mwaka niliamua kutoa 10% ya akiba yote niliyokuwa nayo kwenye akaunti zangu. Moyoni nilidhamiria kwenda kutoa sadaqa kwenye wadi ya watoto, nilivofika hospitali nikaachana na wazo la kwenda kwa watoto nikaelekea moja kwa moja kwenye wodi ambayo alilazwa marehemu mzee wangu wakati anaumwa japo roho iliendelea kunikataza ikinitaka nipeleke kwa watoto, nikang'angania kwenda wadi ile. Cha ajabu nilivofika pale ile nataka kuingia wodini nikakuta watu wanazuiliwa kuingia na muda wa kuzuia watu ulikuwa haujafika!! Nikawaza, nikasema huyu ni Mwenyezi MUNGU anataka nipeleke pale alipopakusudia. Nikaamua kwenda kwa watoto wachanga, kwakweli niliwakuta watoto ambao wazazi wao kwa kuwaona walikuwa ni masikini sana!!!. Nikamuomba Nesi aniruhusu niweze kuwaona na anitafutie wazazi kumi wenye hali duni. Aliwaleta wakiwa na watoto wao. Mimi nikatoa nilichonacho nikarejea home; na kwakweli siku hiyo nilitamani ningekuwa tajiri kama Bakharesa maana 10% ingekuwa ni bonge la burungutu.

Baada ya kufika home nikamshukuru Mwenyezi MUNGU na nikatubia iwapo nimefanya kosa katika kufanya jambo hilo maana wakati mwingine unaweza fanya jambo kwa nia njema lakini ukawa umekosea. Kuna kitu cha ajabu sana kilinitokea ambacho siwezi kueleza hapa na watu wakanielewa. Nilihisi msisimko wa ajabu sana mwilini mwangu, na nguvu za ajabu ziliingia mwilini mwangu kwa namna ambayo nashindwa kuieleza; sitasahau siku hii kamwe maana naamini roho wa MUNGU alishuka katika wakati ule; Ile hali haiwezi kuelezeka mtu akakuelewa. Kuna baraka kubwa katika kufanya mambo mema. Nakutia nguvu tena, peleka sadaqa yako mahala roho inakutuma hususani kwa wahitaji, mshirikishe Mwenyezi MUNGU jambo lako unalotaka kulifanya kabla ya kutoka nyumbani utaona maajabu makubwa ambayo hata wewe utashangaa.

Kulazwa kwako Bugando kulikuwa na kusudi la Mwenyezi MUNGU, Kuna jambo alitaka akufundishe. Namshukuru Mwenyezi MUNGU kwakuwa ni kweli amekufundisha na umefundishika. Baadhi ya tabia njema ulizonazo hivi sasa huenda ni matokea ya kulazaa kwako hospital. Katika kila tatizo kuna mafunzo, hivyo yakupasa kushukuru sio kulalamika. Mimi nina ushuhuda mwingi sana, safari ya mabadiliko ya kitabia na mwenendo katika maisha yangu haikuwa ya siku moja bali ni mtiririko wa matukio mbalimbali ambayo yote yamenishape hivi nilivyo leo.

N.B: Ukitaka kujua faida za kutenda wema. Sikiliza wimbo unaitwa "Wema ni Hazina" ameimba mama mmoja anaitwa kama sikosei ni "Mgendi". Hilo ni jna lake la pili. Nenda You tube search jina la wimbo utaupata. Ni wa wakristo lakini hata kama ww ni muislamu nakusihi sana nenda kasikilize maana inasemekana ni kisa cha kweli kama kilivyo.
 
Huu mfumo mbaya sana, naupinga kwa nguvu zote na ushindwe kwa mamlaka yangu!!.

Juzi jamaa yangu mmoja yupo DRC ali_post kwenye page yake kuwashukuru ndg, jamaa, marafiki na wadau kwa michango yao tena kupitia mitandao ya simu ambayo ilifanikisha mwanae kuhitimu elimu ya juu!.

Niliipenda na nikasena nitai_apply hapa bongo nione mrejesho wake!!.
 
Ndugu, nimebarikiwa sana na ushuhuda wako, ninaamini wengi watabarikiwa pia. Nikutie moyo tena ndugu yangu. Fungu lako la kumi peleka pale moyo unapokutuma upeleke. Mimi ni muislam lakini mafungu hayo huwa sipeleki msikitini, huwa napeleka pale moyo unaponituma nipeleke na mara nyingi huwa namshirikisha Mwenyezi MUNGU kwanza na hivyo huwa najikuta nimepeleka mahali sahihi. Katika kutoa kwangu siangalii dini wala huwa siulizi jambo hilo, ili mradi umeumbwa na Mwenyezi MUNGU na una shida basi mimi nipo tayari kumsaidia. Hebu nikushuhudie jambo moja kwa faida yako na wengine.
Siku moja mwisho wa mwaka niliamua kutoa 10% ya akiba yote niliyokuwa nayo kwenye akaunti zangu. Moyoni nilidhamiria kwenda kutoa sadaqa kwenye wadi ya watoto, nilivofika hospitali nikaachana na wazo la kwenda kwa watoto nikaelekea moja kwa moja kwenye wodi ambayo alilazwa marehemu mzee wangu wakati anaumwa japo roho iliendelea kunikataza ikinitaka nipeleke kwa watoto, nikang'angania kwenda wadi ile. Cha ajabu nilivofika pale ile nataka kuingia wodini nikakuta watu wanazuiliwa kuingia na muda wa kuzuia watu ulikuwa haujafika!! Nikawaza, nikasema huyu ni Mwenyezi MUNGU anataka nipeleke pale alipopakusudia. Nikaamua kwenda kwa watoto wachanga, kwakweli niliwakuta watoto ambao wazazi wao kwa kuwaona walikuwa ni masikini sana!!!. Nikamuomba Nesi aniruhusu niweze kuwaona na anitafutie wazazi kumi wenye hali duni. Aliwaleta wakiwa na watoto wao. Mimi nikatoa nilichonacho nikarejea home; na kwakweli siku hiyo nilitamani ningekuwa tajiri kama Bakharesa maana 10% ingekuwa ni bonge la burungutu. Baada ya kufika home nikamshukuru Mwenyezi MUNGU na nikatubia iwapo nimefanya kosa katika kufanya jambo hilo maana wakati mwingine unaweza fanya jambo kwa nia njema lakini ukawa umekosea. Kuna kitu cha ajabu sana kilinitokea ambacho siwezi kueleza hapa na watu wakanielewa. Nilihisi msisimko wa ajabu sana mwilini mwangu, na nguvu za ajabu ziliingia mwilini mwangu kwa namna ambayo nashindwa kuieleza; sitasahau siku hii kamwe maana naamini roho wa MUNGU alishuka katika wakati ule; Ile hali haiwezi kuelezeka mtu akakuelewa. Kuna baraka kubwa katika kufanya mambo mema. Nakutia nguvu tena, peleka sadaqa yako mahala roho inakutuma hususani kwa wahitaji, mshirikishe Mwenyezi MUNGU jambo lako unalotaka kulifanya kabla ya kutoka nyumbani utaona maajabu makubwa ambayo hata wewe utashangaa.

Kulazwa kwako Bugando kulikuwa na kusudi la Mwenyezi MUNGU, Kuna jambo alitaka akufundishe. Namshukuru Mwenyezi MUNGU kwakuwa ni kweli amekufundisha na umefundishika. Baadhi ya tabia njema ulizonazo hivi sasa huenda ni matokea ya kulazaa kwako hospital. Katika kila tatizo kuna mafunzo, hivyo yakupasa kushukuru sio kulalamika. Mimi nina ushuhuda mwingi sana, safari ya mabadiliko ya kitabia na mwenendo katika maisha yangu haikuwa ya siku moja bali ni mtiririko wa matukio mbalimbali ambayo yote yamenishape hivi nilivyo leo.

N.B: Ukitaka kujua faida za kutenda wema. Sikiliza wimbo unaitwa "Wema ni Hazina" ameimba mama mmoja anaitwa kama sikosei ni "Mgendi". Hilo ni jna lake la pili. Nenda You tube search jina la wimbo utaupata. Ni wa wakristo lakini hata kama ww ni muislamu nakusihi sana nenda kasikilize maana inasemekana ni kisa cha kweli kama kilivyo.
Asante sana mkuu. Wewe ni mtu wa pekee uliyejaa ubinadamu halisi. Imagine 10% ya mapato yako yote kwenda kuwapa masikini!

Historia yangu ni ngumu kidogo na kweli mabadiliko niliyopitia mpaka kufika hapa nilipo na kuwa hivi nilivyo ni ya polepole ila ule mkasa wa Bugando ulinifungua macho sana. Kwa mara ya kwanza nilianza kumtazama binadamu kwa jicho jipya, jicho lililojaa matumaini. Ndiyo! Nitaanza kumshirikisha Mungu katika sadaka zangu ili zikaweze kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa na kupunguza mizigo ya binadamu wenzetu hawa wanaoteseka, japo kwa muda tu.

Mwaka juzi nilikutana na kijana mmoja aliyekuwa ametelekezwa na familia yake pale Muhimbili. Matundu yake ya pua yalikuwa yameota nyama na kuziba kabisa na alikuwa anapumua kwa shida sana. Alikuwa amedhoofika.

Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kwa maombi na kila nililoweza kufanya lakini ikashindikana. Mpaka siku Mungu Anamuita alikuwa akinishukuru na kuniambia kuwa nimempa amani ya kweli mimi mtu baki asiyemfahamu wakati ndugu zake walikuja kumtupa hapo na kumuacha. Niliguswa sana na kijana huyo masikini mpaka nikahisi kuwa nimekua kiroho na kuanza kuyatazama mambo kwa mtazamo mwingine kabisa. Alipofariki nilimtafuta kiongozi wake mmoja wa kiserikali tukapeleka maiti huko kijijini kwao tukamlaza. Nilichogundua ni kwamba kumbe hata ndugu zake hawakumtelekeza kwa hiari yao bali ni kwa sababu ya umasikini uliopindukia kimo. Jambo la ajabu ni kwamba kupitia kwa kijana huyu masikini nimepata bahati ya kufahamiana na watu wengi ambao baadhi yao wamegeuka na kuwa watu muhimu kwangu kiasi kwamba hata nikiwa uwanja wa ndege nikipiga simu naweza kuletewa gari na walinzi kunipeleka huko niendako. Mungu Ana mambo ya ajabu sana!

Asante sana ndugu yangu. Hapa ni mtandaoni hatujuani lakini naona kama vile huu nao ni muujiza. Asante sana kwa ushuhuda wako huu. Nahisi imani yangu imechochewa upya, wito mpya umeitishwa na moto wa ubinadamu unawaka upya. Asante sana na Molla Aendelee kukubariki!
 
Nilichoka juzi girlfriend wangu kaniletea card ya mchango wa harusi ya rafiki yake
Nikamkatalia akaanza kusema ooooh unajua huyu ni rafiki yangu sa nisipomchangia na yeye hatonichangia nikiolewa
Hahahaa sasa kichwani nikawaza "huyu demu mwehu nini! Yaani keshapigia mstari kwamba nitamuoa kheeeee!"
 
Uchoyo unawasumbua kuna ubaya gani kumchangia rafiki yako wa karibu mchango kutoa ni moyo tu ka hutaki unaacha haulazimishwi sijui mwadai msiba nao si mchango Mara mwingine elimu magu sianatoa elimu bora mfyuuuuu mijitu michoyo bana na maskini wakutaftia sehemu ya matatizo yao kusingizia harusi mbona mibia mwaichikichia
 
Asante sana mkuu. Wewe ni mtu wa pekee uliyejaa ubinadamu halisi. Imagine 10% ya mapato yako yote kwenda kuwapa masikini!

Historia yangu ni ngumu kidogo na kweli mabadiliko niliyopitia mpaka kufika hapa nilipo na kuwa hivi nilivyo ni ya polepole ila ule mkasa wa Bugando ulinifungua macho sana. Kwa mara ya kwanza nilianza kumtazama binadamu kwa jicho jipya, jicho lililojaa matumaini. Ndiyo! Nitaanza kumshirikisha Mungu katika sadaka zangu ili zikaweze kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa na kupunguza mizigo ya binadamu wenzetu hawa wanaoteseka, japo kwa muda tu.

Mwaka juzi nilikutana na kijana mmoja aliyekuwa ametelekezwa na familia yake pale Muhimbili. Matundu yake ya pua yalikuwa yameota nyama na kuziba kabisa na alikuwa anapumua kwa shida sana. Alikuwa amedhoofika.

Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kwa maombi na kila nililoweza kufanya lakini ikashindikana. Mpaka siku Mungu Anamuita alikuwa akinishukuru na kuniambia kuwa nimempa amani ya kweli mimi mtu baki asiyemfahamu wakati ndugu zake walikuja kumtupa hapo na kumuacha. Niliguswa sana na kijana huyo masikini mpaka nikahisi kuwa nimekua kiroho na kuanza kuyatazama mambo kwa mtazamo mwingine kabisa. Alipofariki nilimtafuta kiongozi wake mmoja wa kiserikali tukapeleka maiti huko kijijini kwao tukamlaza. Nilichogundua ni kwamba kumbe hata ndugu zake hawakumtelekeza kwa hiari yao bali ni kwa sababu ya umasikini uliopindukia kimo. Jambo la ajabu ni kwamba kupitia kwa kijana huyu masikini nimepata bahati ya kufahamiana na watu wengi ambao baadhi yao wamegeuka na kuwa watu muhimu kwangu kiasi kwamba hata nikiwa uwanja wa ndege nikipiga simu naweza kuletewa gari na walinzi kunipeleka huko niendako. Mungu Ana mambo ya ajabu sana!

Asante sana ndugu yangu. Hapa ni mtandaoni hatujuani lakini naona kama vile huu nao ni muujiza. Asante sana kwa ushuhuda wako huu. Nahisi imani yangu imechochewa upya, wito mpya umeitishwa na moto wa ubinadamu unawaka upya. Asante sana na Molla Aendelee kukubariki!
Aamin, Aamin, Aamin. Niseme kweli, kama ilivyo kwako; kwangu pia nuru mpya imeng'ara katika maisha yangu kwa hayo uliyoeleza hapa nimepata nguvu mpya na afya mpya kiroho.

Mimi huwa nawashangaa sana watu wakikaa vijiweni na kusema "binadamu wabaya" mara utasikia "ooh Dunia hii hakuna wa kukusaidia zaidi ya ndugu yako" n.k n.k mimi huwa nawasikiliza tu na kusema; Hakika atakayekufaa kesho humjui kwasababu mimi mwenyewe nimewasapoti watu ambao siwajui na hata nikionana nao kesho hawatanikumbuka wala sitawakumbuka.

Kitu kikubwa pia nilichojifunza maishani mwangu ni kuwa tenda wema na usisubiri shukurani. Malipo ya wema wa aina hii hulipwa na Mwenyezi MUNGU mwenyewe kwako mwenyewe au hata kwa kizazi chako. Maajabu ya wema ulioufanya utaanza kuyaona ukiwa na shida, utashangaa watu wa kukusaidia wanajitokeza tu bila hata kujua wametokea wapi tena huwajui na cha ajabu zaidi hawahitaji malipo kutoka kwako!!! Kanuni ya wema ni ya ajabu sana sana sana.

Kubwa zaidi tukumbuke kuwa tunavotenda wema ni tunatimiza kusudi la Mwenyezi MUNGU. Tujifunze kuwa unapotenda wema huwenda ukawa umefanya muujiza mkubwa sana kwa yule uliyemtendea bila hata wewe kujua. Kwa wema wako huenda yule uliyemtendea akakesha usiku kucha akimshukuru Mwenyezi MUNGU kuwa amemjibu maombi yake!!! Sote Hatujui lakini huwenda mtu uliyemsaidia aliomba Mwenyezi MUNGU amsaidie jambo, nawewe ukajitokeza ukafanya lile lile kama alivoomba kwa mwenyezi MUNGU! Tazama jinsi mtu huyu atakavomshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kumjibu maombi yake. Kifupi ni kuwa kila mmoja hapa duniani katumwa na Mwenyezi MUNGU aje atimize kazi fulani alizopangiwa lakini wengi wameamua kufuata mambo yao wenyewe yanayowafurahisha wao na nafsi zao bila kujali walichotumwa na Mwenyezi MUNGU ndio maana harusi wanachangia 50,000/= lakini kwa mgonjwa na mwenye shida anatoa 500! Ni vitu vya ajabu sana vinatendeka hapa duniani hadi vinachekesha na kuhuzunisha.
Kwakweli mimi nishajisemea moyoni mwangu kuwa kwenye haya mambo ya kipuuzi ya sherehe zisizo na maana watu wanatumia milioni kumi kwa siku kwa kula na kunywa hawataniona kamwe na nipo tayari kulaumiwa na hata kutengwa maana ninajua kuwa watakaonifaa si hawa ninaowadhania bali Mwenyezi MUNGU ataniletea watu nisiowajua na hata kunizika watanizika. Napenda sana niwapate ndugu wa kiroho kama wewe wawe jirani zangu katika maisha yangu maana hata ktk nyakati za huzuni watanipa faraja ambayo pengine singeipata mahali pengine popote.
 
Dawa ya hii kitu TRA waanze kuchukua kodi kwenye kila mchango wa harusi,wanandoa lazima wataingia mitini tu.
 
Uchoyo unawasumbua kuna ubaya gani kumchangia rafiki yako wa karibu mchango kutoa ni moyo tu ka hutaki unaacha haulazimishwi sijui mwadai msiba nao si mchango Mara mwingine elimu magu sianatoa elimu bora mfyuuuuu mijitu michoyo bana na maskini wakutaftia sehemu ya matatizo yao kusingizia harusi mbona mibia mwaichikichia
Ww fanya upendavyo. Ni pesa yako na ni hiari yako kutumia utakavyo. Kila mmoja ana mtizamo wake na ana hiari ya kutumia atakavyo katka mapato yake kwa kadiri atavoona inafaa. Siku ukiumwa ni watu wachache sana waliokuchangia/uliowachangia harusi ambao watakajitokeza kuchangia matibabu. Tafakari na chukua hatua.
 
Mi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu

Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
Well said....mimi nimekaa nje miaka 18 nimerudi na mchumba nikafanyiwa harusi na wazee.nikawaambia wazee mimi napenda harusi ndogo tu watu wachache mno wakajibu sisi tilichanga harusi za watu sana sasa zamu yao.basi ilibidi niwasikilize wazazi.ila mimi binafsi kuchanga harusi sipendi na kadi itasema minimum sijui ngapi.mimi nina harusi 3 za kuchanga na zote si watu wa karibu na sitachanga.misiba tu ntakuwepo
 
Dawa ya hii kitu TRA waanze kuchukua kodi kwenye kila mchango wa harusi,wanandoa lazima wataingia mitini tu.

Well said ,TRA ni ma-robot?

Watoto wa wafanyakazi wa TRA ndo wanaongoza kwa harusi kubwa!Hujui hilo?

Wakati wewe unabania na mkono wa korosho wenzio wanachangia na wanapata baraka!

Hulazimiahwi,hata elimu kuchangia hulazimishwi!

Kupanga ni kuchagua!
 
Waendelee kuchanga kwa maisha ya sasa sitaweza changia harusinya mtu acha nitumie pesa yangu kumsomesha mwanangu mimi.mtu anataka harusi kubwa na uwezo hana.nashukuru mi si mtu wa kujichsnganya kwenye starehe.misiba twende tu
 
Back
Top Bottom