Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mimi nimebahatika kuhudhuria harusi ya rafiki yangu ambayo ilikuwa simple tena mkristo tulikuwa watu tusiozidi 30 kilinunuliwa chakula hotelini na vinywaji watu wakanywa tukasambaa na ndoa mpaka leo mwendo mdundo!
Sijui watu nani kawavisha miwani ya mbao wanashindwa kabisa kujua huu si wakati wa kufanya ujinga huu wewe kama huna huna tu! Kwangu mimi ukija na kadi yako naiweka kado na bahati nzuri mimi pia kwenye harusi sikumchangisha mtu
 
Habari wana Jf
Aisee me kuna swal linanitatiza sana hiv kwa nini watu kwenye mambo ya sherehe watu wanachanga sana hata milion 30 na zaidi lakin kwenye mambo ya kuinuana uchumi mtu hata ukiomba elfu ishirin atakwambia cna
Kwa mfano graduate akiomba msaada wa kuchangiwa japo kidogo ajiendeleze kiuchumi hawez kupewa lakin akisema tu labda anataka kuoa hapo watu watatoa pesa balaa
 
mambo mengine ya kijinga sana unaoa wewe unaenda kugegeda wewe mi nikuchangie sitoi
 
Wakati mwingine inakera.Kuna msichana nimemaliza naye chuo ni zaidi ya miaka mitano imepita hata alikua sio rafiki yangu wa karibu cha kuahngaza leo sijui kapata namba yangu wapi kaniunga whatsup kaanza kujitambulisha sikumkumbuka hadi nikaamua kumpigia ili anieleweshe zaidi ndo nikamkumbuka baada ya hapo akaanza kuniuliza nafanya wapi kazi nikamficha. Mara nikasikia eti nataka mchango was send off yangu aisee nikaishiwa pozi, sijakaa sawa nikasikia "una pledge(ahidi) shngapi'', du nikachoka kabisa nikamwambia mbona haraka hivyo nikamuaga nikakata sim.
 
Binafsi sina mpango wa kufanya watu wakose usingizi kwa sababu ya harusi Huyo mtarajiwa atakayekuja ashuhulikie gharama za mahari ( Send off siku hiyo hiyo ya kutoa mahari na kuvisha Pete ya uchumba ) , vitu vya harusi( vyangu na vyake), kanisani , na honeymoon Kwisha kazi. Atakayetaka sherehe zaidi ya hii aifanye kwa gharama zake mwenyewe . kuna mambo mengi ya kufanya baada harusi , kujenga na kujali familia kwa baadae . Muhimu ni upendo wa kweli tuu
 
Nadhani haya mambo yametibua urafiki wa watu wengi sana ktk jamii.. mm kuna jamaa angu like two years ago aliniomba mchango ila mambo yakawa tight sikufanikisha, anyway harusi ilifanyika ila after that akanijia na bonge moja la msg, nilikaa tu kimya yapite kimyakimya.. ipo haja ya elimu ya michango ya hiari ili wana jamii waelewe aisee
 
Habari za muda huu wana jf
Takribani miongo kadhaa imepita watu wa jamii tofauti tofauti tumekuwa na mazoea ya kila MTU akitaka kufunga ndoa basi lazima aandae kadi kwa ajili ya kupitisha kwa watu apate mchango kwa ajili ya kufanya sherehe kubwa ya harusi.

Natambua ni kweli watu tofauti tofauti hali ya uchumi sio nzuri lakini kwa upande mwingine naona ni vema Muhusika na mwenza wake waandae sherehe ndogo itakayoendana na hali yao ya kiuchumi kuliko kuanza kusumbua watu na hizi kadi za michango.

Imefika wakati MTU kwa mwaka unapokea kadi za michango zaidi ya 40, sasa kwa hali hii kweli si kurudishana kwenye umasikini!!

Nawasilisha....
 
Kama huna hela ya kuwachangia huna ulazima wa kujisumbua, maana michango huwa ni hiari tu.

Mwanadamu ana safari tatu za muhimu hapa duniani..

1. kuzaliwa
2. kuoa / kuolewa
3. kufariki
 
Kiukweli kwa sasa wamezidi mtu kila ukirudi nyumbani card za michango ya harusi zamani utachangia ulichonacho cku izi na kiasi wanaandika wao kama wameweka mfukoni kwako.
 
Habari za muda huu wana jf
Takribani.....miongo...kadhaa imepita..watu wa jamii tofauti tofauti tumekuwa na mazoea ya kila MTU akitaka kufunga ndoa basi lazima aandae kadi kwa ajili ya kupitisha kwa watu apate mchango..kwa ajili ya kufanya sherehe kubwa ya harusi...natambua ni kweli watu tofaut tofaut hali ya uchumi sio nzur lakini...kwa upande mwingine naona ni vema Muhusika na mwenz wake waandae sherehe ndogo itakayo endana na hali yao ya kiuchumi kuliko kuanza kusumbua watu na hizi kadi za michango...imefika wakati MTU kwa mwaka unapokea kadi za michango zaidi ya 40 ....sasa kwa hali hii kwel c kurudishana kwenye umasikini...
Nawasilisha....
 
Kiukweli kwa sasa wamezidi mtu kila ukirudi nyumbani card za michango ya harusi zamani utachangia ulichonacho cku izi na kiasi wanaandika wao kama wameweka mfukoni kwako.
Hicho ndo kinacho niudhi kupangiwa kiwango...hapo ndo sitoi kabisa huwezi juwa uwezo wangu. Sisi waafrica tunapenda harusi kubwa nawaonea wazungu raha wanafanya harusi kwa uwezo wao
 
Kuna jamaa mmoja Dar anahusika na biashara za kufunga mizingi na rims kwenye magari, huju jamaa alifanya kitu SAFI SANA alikusanya michango kama 30mil baada ya hapo akasambaza kadi za harusi, siku moja kabda ya harusi akatuma taarifa kuwa harusi inafungwa kama kawaida lakini sherehe ya harusi imesimamishwa ghafla kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake na kuwa angewajulisha ni lini sherehe itafanyika....huu ni mwaka nne kinywa hakuna sherehe na 30mil kamalizia nyumba yake mbezi.....hii safi sana...wabongo mkome kutoa michango
ha ha ha ha ha ha ha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
ha ha ha ha ha ha ha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Haaaaa wakome wanaochanga mi sipo kuchangia watu nisio wajuwa au watu wa mbali mimi nachanga misiba number 1.harusi mpk nikujuwe sana vinginevyo bye bye haaaaaa
 
Back
Top Bottom