Ndugu wana JF, hili suala la michango ya harusi naona hivi sasa inashika kasi kwa kasi ya ajabu, nikifikiria kwa makini kabisa naona ni kitu ambacho hakina tija hata kidogo, kwana mwisho wa siku zinapatikana pesa nyingi sana ambazo zinaenda kuteketezwa kwa anasa ya siku moja tu. Wakati huohuo unakuta mtu unamichango lukuki kwa mwezi, mpaka unatoa michango karibu nusu ya mshahara wako, hivyo tunajikuta tunafanya kazi ili kuziendeleza hizi anasa zisizokuwa na maana.
Mimi napendekeza, kama mtu unataka kuoa hakikisha umekusanya pesa za kutosha kulingana na aina ya sherehe unayoitaka. Mtu unataka kufanya harusi ya Mil 30 halafu wewe mwenyewe una laki tano, huku ni kuwapa stress watu wengine tu. MKE NI WAKO, KUOA UMEAMUA WEWE MWENYEWE,KULALA UTALALA NAE PEKE YAKO, HALAFU MIMI NISIPOKUCHANGIA HELA UNANINUNIA.
kUANZIA LEO, MIMI NITAPOKEA KADI ZA MICHANGO YA VITU VIFUATAVYO:
1. Kuchangia Ada mtu aliyepungukiwa
2. Mgonjwa anayehitaji huduma ya dharura ambayo ni ghali
3. Misiba
4. Na vitu kama hivyo
Hii ni kwa sababu, mengi ya mambo haya yanakuja bila ya muhusika kujiandaa kifedha na masuala mengine, na yasipotatuliwa basi tunampoteza mwenzetu in case ya ugonjwa, au mtoto atashindwa kwenda shule. Lakini Harusi, watu wanakuwa wameshafanya uzinzi weeee, wakinogewa basi wanapanga tufunge ndoa mwezi ujao. Hili ni suala ambalo mnatakiwa mjiandae wenyewe, na ufanye kulingana na uwezo wako!!!
WATANZANIA MICHANGO YA HARUSI NI KERO SANAAAAAAAA!!!!!!