Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

MSIISHIE KUSEMA MICHANGO NI MWIBA, FANYENI UAMUZI. MKIBAKI NA MENTALITY ZA KI TZ MNAOZA.MSIONE AIBU KUMWAMBIA MTU SINA PESA YA MCHANGO.
mimi nikikutana na m tz nje ya nchi kudadeki namkwepa..... kuaibishana tu. wote tu masaburi sisi wa tz. inakera kila siku tunajijadili kama wapumbavu
 
Naungana na mdau kupinga vikali michango ya harusi, ni kutaka ufahari usiokuwa na tija na kupoteza wakatai bila faida yoyote. Siku moja rafiki yangu alikuwa akimuonyesha rafiki yake mzungu picha alizopiga alipokuwa anafunga harusi yake, yule mzungu alishangaa kuwa sisi watanzania ni maskini allshindwa kuamini kuwa sisi ndiyo wale tunaojitangaza ulimwenguni kuwa ni maskini. Hivyo wadau tunahitaji kbadili mwelekeo wetu kuhusu kuchangia harusi.
 
Ukweli ni kwamba, Mimi binafsi ni mtu wa daraja la kati, uwezo wa kufanya sherehe ya mil 6, 7 mimi mwenyewe ninao. Ila nilitaka kufikisha ujumbe huu kwa jamii, mimi nilienda kanisani na mke mchumba wangu (sasa mke wangu) jumamosi moja miaka mitano iliyopita, nikafunga ndoa na baada ya hapo tukarudi nyumbani. Sikumchangisha mtu na wala mimi mwenyewe sikutumia hela yoyote zaidi ya shela , suti na pete. Mimi na mke wangu tunaishi kwa amani, nina watoto watatu,

Safi sana mkuu, haya mambo awali hayakuwepo ila baada ya vijana wengi kumaliza elimu za juu siku hizi imekuwa fasheni, zamani harusi zilikuwa zikifanyika kwa michango ya ndugu tu wafamilia, lakini siku hizi kwanza tangazo ktk mitandao ya kijamii, tunakutana ktk kumbi au baa maarufu tunapanga mipango ya harusi ktk vikao sio chini ya 30.
 
Sasa ni mwiko kuchangia harusi mana mnatuingiza katika matatizo tunatopoteza pesa nyingi sana katika halusi mana unakuta watu wanafunga leo kesho wameachana inakuwa haileti mana kabisa.ushauli wng ni
1.tufanye michango kwa jili ya kuwaongezea mtaji kusudi waweze kujikimu na haya maisha.mana tutakuwa tumewasaidia kuliko kuangamiza mamilion ya pesa alafu kesho utasikia wana lala njaa
2.kama mtu atahitaji kufunga halusi basi ajue ghalama ni zake hatutamchangia mana kuna watu wengi wanahitaji misaada
3.siku hizi makanisani kuna mfumo huu kuwa bibi anatoka kwao na bwana anatoka kwao wanafungishwa wanasema.
4.ina mana gani mtu anafunga halusi huku ni mjamzito jamani tuache utani na nyie viöngoz wa dini hili hamlioni huku si kutiana aibu jamani bada ya mwez unasikia kajifungua ebu tuache utani tu muogope Mungu hizi ni laa na.NAUNGA HOJA ASILIA MIA
 
Ukweli ni kwamba, Mimi binafsi ni mtu wa daraja la kati, uwezo wa kufanya sherehe ya mil 6, 7 mimi mwenyewe ninao. Ila nilitaka kufikisha ujumbe huu kwa jamii, mimi nilienda kanisani na mke mchumba wangu (sasa mke wangu) jumamosi moja miaka mitano iliyopita, nikafunga ndoa na baada ya hapo tukarudi nyumbani. Sikumchangisha mtu na wala mimi mwenyewe sikutumia hela yoyote zaidi ya shela , suti na pete. Mimi na mke wangu tunaishi kwa amani, nina watoto watatu,
umeharibu hapo. why advertise your potential in public? kuwa mpole bwana
 
nimesoma hiz posts nimejisikia faraja sana!hii kitu inakera acha kabisa!nipo safarin,huko kijjn hakuna network,ile simu inawaka tu,napata sms,naozesha binti yangu naomba mchango wako,min.elfu 50!wakati kjjn nimewaacha hali mbaya!can you imagine inavyotia hadira.
 
umesema kweli ndugu. its totally rubbish, uncouth and barbaric behavior which should stop with immediate effect. harusi ya mamilioni huku watanazania wanakufa kwa njaa itasaidia nini? watoto wa maskini wanashindwa kwenda shule huku tunapoteza mabilion kwa harusi kuendekeza upuuzi usio na msingi. hivi jamani watanzania wenzangu tutajikomboa lini kwa utumwa wa psychology? ni lini tutafikiria beyond the box?
juzi nilikua kwa club, mtu akasema tanguia asubuhi hiyo bia alikua akinywa ni ya kumi na tano. just imagine? sijui aliona fahari kusema hivyo au vp? i mean my dear friends tunapoteza muda mwingi sana pamoja na raslimali ambazo zingetuweka katika mojawapo za nchi zilizoendelea. huu umaskini unatokana na sisi wenyewe, tujilaumu.
kuna njia nyingi sana za kufanya harusi bila extreme expenses. inasikitisha sana unakuta tunaridhika kuchanga elfu 50 kila mtu kwa ajili ya harusi lakini huyu mtu ukimualika kwa mchango wa elimu haji au anatuma 1000 au analeta vigezo vingi visivyo na maana. wadau wenzangu nafikiri ni wakati mwafaka wa kuijadili mambo kama haya ni hili jukwaa liwe njia moja ya kutujenga katika misingi ya kujua mema na mabaya.
 
labda uhamie Ulaya ndio utafanikiwa,maana naskia huko kila mtu na lwake
 
sasa wana Jf hebu tushauriane,tufanyeje?kupiga ban hii kitu!kuwe na campaign,au elimu kwa umma,au hadi waje wazungu watuelimishe?
 
sasa wana Jf hebu tushauriane,tufanyeje?kupiga ban hii kitu!kuwe na campaign,au elimu kwa umma,au hadi waje wazungu watuelimishe?
Mkuu hii comment yako kiboko. Ngoja greti thinkazz walete maaidia hapa.
 
Naunga mkono hoja,kwakweli tumefikia pabaya na tunakoelekea sijui itakuaje. We need to do something kutoka kwenye hili JANGA maana ni kweli usipotoa mchango unatengwa,na maneno mengi yanasemwa mara ooh anajitenga sijui nini wakati hali yangu naijua mwenyewe nimetoa michango harusi tatu mwezi mmoja na zote unaambiwa sio chini ya laki moja(heri yenu mnaambiwa elfu 50),na ni watu wa karibu hapo hapo eti bado send off na kparty kweli tutafika jamani??????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Card nyingine mbili nikaweka pembeni maana mfuko wangu haukuruhusu sasa ndio yanakuja maneno,sio vizuri ndugu tuwe wastaarabu kwenye kudai michango.

Mbaya zaidi unampelekea card mtu ambae hana kazi(means hajaajiriwa wala kujiajri)sasa akaibe ndio akupe mchango??!!!!!!inatia hasira sanaaaa.

Tukomeshe hii tabia,vipi ndio tuumize vichwa kujua solution sio tubaki kuongea tu.
 
Unajua hizi pesa tunazopoteza kwa kuchangishana kwenye vitu hivi visivyo vya msingi kama tungezielekeza kwenye miradi ya maji, vitabu mashuleni,vifaa vya maabara, kwa watoto yatima n.k, matatizo mengi madogo madogo yanayotukabili kama jamii yangeshakuwa historia kitambo...

Hii kitu inakera sana, suala la kuoa/kuolewa ni jambo binafsi, na ni heshima kwa mtu kuligharamia mwenyewe...
 
Mimi naona wote kama jamii tunachangia hii hali,utakuta mtu akipewa kadi ya mwaliko bila kuchangia analalamika,anaweza hata asije kwenye shughuli yenu,anaona kama hajashirikishwa,atakwambia yaani mimi ndio wa kupewa tu kadi ya mwaliko?
 
Ukweli ni kwamba, Mimi binafsi ni mtu wa daraja la kati, uwezo wa kufanya sherehe ya mil 6, 7 mimi mwenyewe ninao. Ila nilitaka kufikisha ujumbe huu kwa jamii, mimi nilienda kanisani na mke mchumba wangu (sasa mke wangu) jumamosi moja miaka mitano iliyopita, nikafunga ndoa na baada ya hapo tukarudi nyumbani. Sikumchangisha mtu na wala mimi mwenyewe sikutumia hela yoyote zaidi ya shela , suti na pete. Mimi na mke wangu tunaishi kwa amani, nina watoto watatu,

Hiki ulichokifanya mimi nilikifanya miaka takriban kumi na moja iliyopita pale kwenye viwanja vya Jangwani. Siku hiyo zilifungwa harusi zaidi ya themanini kwa mpigo na baadaye ikawa utawala binafsi kila mtu akaenda kivyake. Jumatatu yake nilitoa taarifa ofisini kuwa nimefunga ndoa na watu hawakuamini na waliona kama vile ni mambo ya kusadikika. Kwa ufupi haya mambo ni uamuzi tu wa wahusika hasa bwana na bibi arusi. Mnagawana majukumu tu: bibi arusi anamshawishi mama mkwe na wewe unamshawishi mama yako mzazi. Hawa kina mama ndio huwa wana mind sana mambo ya kumeremeta.
 
Mbaya zaidi kwa sasa (kwa walio wengi) ni kama fashion vile, ni uhuni kwa kwenda mbele!
 
Unajua hizi pesa tunazopoteza kwa kuchangishana kwenye vitu hivi visivyo vya msingi kama tungezielekeza kwenye miradi ya maji, vitabu mashuleni,vifaa vya maabara, kwa watoto yatima n.k, matatizo mengi madogo madogo yanayotukabili kama jamii yangeshakuwa historia kitambo...Hii kitu inakera sana, suala la kuoa/kuolewa ni jambo binafsi, na ni heshima kwa mtu kuligharamia mwenyewe...
kila pesa inamatumizi yake! pesa ipo ili itumike,pesa ya kupoteza ni ile uloweka mfukoni ukashtuka ukakuta haipo.
 
Back
Top Bottom