Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Yaani balaa, mfuko wa haya madafu kuingia ni mmoja ila inapokuja swala la kutoka, mfuko una milango mingi sana. Hadi inakera.......
 
no acheni tuolewe kwanza ndo mlete hizi mada zenu hapa!!
Umeona ehee kwa vile wao waliishachangisha watu sasa hivi ndio wanaona kero, halafu cha kushangaza zaidi kuna wengine humu humu unawasikia wanasema michango ya harusi inakera kweli lakini bado wanaenda kuchanga
 
Wabongo bana yaani ni kulalamika tu na unafiki kibao wewe uletewe kadi mchango ushindwe kumwambia aliekuletea kwamba huwezi kuchangia kwa sabubu hizi na hizi. Unashindwa kusema unakuja kuongelea JF hapa, Mchango ni hiari wala sio lazima, Kila siku tunaambiana hapa "do wat you believe is right" sasa unashindwa kusimamia uamuzi wako mnakuja kulialia hapa. Eti Mtu mzima unaogopa eti mwenzioa atanunu kisa ujachanga? akinuna ndo anakulishia watoto wako? au watoto watakosa chakula? katika maisha mtu mzima lazima uwe na msimamo.! Usifanye jambo kwa kuoneana aibu. Ndo maana linch haiendelei kisa mnaoneana aibu, mtu hana kigezo cha kupewa kazi unamuonea aibu unampa then kesho unauja kulialia hapa!
 
Tatizo Watanzania wanafiki, kwani ni nani anaekulazimisha kuchangia harusi mpaka ulalamike unashindwa ku- save katika account yako! Suala ni kwamba, kama kweli michango inatukera kama tuanavyosema, na tuache kuchangia! Nawahakikishia kama tutafanya hivyo, michango ya harusi itapotea yenyewe. TUACHE KULALAMIKA KAMA KAWAIDA YETU NA TUCHUKUE HATUA! HII INAPASWA KUANZA NA WEWE!!
 
Si ndo hapo kiongozi, ni unafiki tu hakuna kingine!
 
Yani hilo ndo tatizo, inakuwa ngumu kufanya jambo lolote. Mtu unakuta upo bize na michango ya harusi, unacompromise hata na mahitaji ya msingi ya familia. na mbaya zaidi wanaweka viwango vya chini vikubwa mno!!

Ndugu JF hebu tujadili ni kwa namna gani tunaweza tukaliokoa taifa letu kutoka kwenye hiki kitanzi.

Dawa yake sisi tulioshituka tuikane hii primitive tabia mpaka jamii nzima ikubali kuwa ni ujinga kushupalia sherehe za ndoa badala ya ndoa yenyewe iliyofungwa kanisani ama kwa shehe.
 
katika kumbukumbu zangu mimi Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako... unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.

Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango.... na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga...

Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa.... watu wanakuja wanakunywa na kula.. wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie....

HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA... AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO.....

Mi nakuunga mkono
 
hata me naanza kufikiria kuja kuoa kimya kimya...wife mtarajiwa akinielewa harusi itafungwa kimya kimya
 
sipendi michango ya harusi lakini sometimes inalazimu kutoa

na ni tabia hiyohiyo ya kupenda ku-spend kwenye minuso imefanya taifa kitumie mabilioni kufanya sherehe ya miaka 50 ya uhuru kila kona
 
halafu siku hz mchango wa harusi hadi fifty @ person?
 
Tatizo Watanzania wanafiki, kwani ni nani anaekulazimisha kuchangia harusi mpaka ulalamike unashindwa ku- save katika account yako! Suala ni kwamba, kama kweli michango inatukera kama tuanavyosema, na tuache kuchangia! Nawahakikishia kama tutafanya hivyo, michango ya harusi itapotea yenyewe. TUACHE KULALAMIKA KAMA KAWAIDA YETU NA TUCHUKUE HATUA! HII INAPASWA KUANZA NA WEWE!!

mimi binafsi nilishaacha siku nyingi kuchangia harusi, vipaimara ndio kabisa, wala usinisogelee. sioni kwa nini ufanye harusi kubwa ya kifahari wakati huna uwezo halafu uanze kuomba michango kwa watu. wengi wameshajinijua kua sichangi and it works kwa sababu napewa kadi ya mwaliko na ninakwenda bila wasiwasi. ni bora watanzania tuamke tuchangiane kwenye elimu kuliko harusi, ni bora mara 100. harusi hupangi kwa siku moja, unaweza kupanga hata kwa miaka, kwa nini usi save ukafanya harusi unayoitaka? kwa nini ukamue watu kwa sababu ya mke au mume wako mwenyewe. huu ni ushamba! mbona nchi nyingine wenzetu wanafanya harusi za kifahari kwa pesa zao wenyewe? Sote tuna ndugu wa karibu, iweje ukamue hadi mtu wa mbali kisa unaoa au unaolewa, asipokuchangia na mwaliko hapati, maana hicho ndio kiingilio chake. kuna viwango, kwa bahati mtu akichanga chini ya kiwango, maana ndio uwezo wake, kadi hapewi. huu ni unyanyasaji kwa kweli. naomba muache hii michango muwe kama mimi. Naishi kwa amani, asonijua akinipa kadi yake wala siangalii nani anaoa au kuolewa straight namwambie, sorry hapa ni wrong number, sichangi michango ya harusi, niletee msiba na ugonjwa nitakusaidia, full stop...!!!
 
Mi nadhani unapofunga ndoa ni kwa wewe,mkeo,washenga na wazazi na watu wako wa karibu(wanaweza wasizidi 30kwa upande wako na 30kwa binti jumla ya watu wote kwenye tafrija) ndo wa muhimu kuwepo.ambao unaweza kabisa kumudu kugaramia iyo tafrija...lakini sasa,sisi tumejiwekea kuwa ukifunga ndo unaita kilaaaaaaaaa mtu unayemjua,matokeo jumla kuu unapata watu 400.sasa tatizo linakuja kuwa huwezi kumudu kuwagaramikia katika tafrija.hivyo inabidi wachangie garama za tafrja....hapa ndo kero.kwani lazima nije kwenye harusi yako?kwa iyo usinichangishe.na mi siji.
 
That the worse part of Tz mind.
hii kitu nimekuwa nikiifikiri, the way we generate wedding industry, its too shame to speak and i think we need to change our mindset.
just imagine how much we spend for wedding, its a lots . eneogh is eneough
i attended a certain wedding having almost 40 people at beach club in Dar, roughly it cost not more than 2 ml,
ilikuwa buffee, tables for us, and few drinks not for extreme drinking
Hapo hapakuwa na pesa ya ukumbi,MC,mapambo,wala keki ya laki 5,magari ya kifahari,
In short watanzania tubadilike jamani, Angalau itaumiza wale ambao ndo wanategemea hii industry mpya lakini italeta nafuu kwa maelfu ya watanzania wanaotumia kipato chao kikubwa kwenye harusi.
 
katika kumbukumbu zangu mimi Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako... unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.

Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango.... na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga...

Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa.... watu wanakuja wanakunywa na kula.. wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie....

HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA... AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO.....

Yaan mi nakuunga mkono 100% huu ni upuuzi tu. Mtu anataka kufanya sherehe kwa mishahara ya wenzie.
Mi nimeanzisha utaratibu wa kuhudhuria mahali ndoa inapofungwa, natoa zawadi ya kuwapongeza then mambo yanaishia hapo. Kadi zao za Michango yao sizitaki tena nowdays.
 
Inatia uchungu kuona mamlaka huisika zinazo hangaika kutaka kujua
pato la mtanzania wanatumia vigezo vya kinagharia huku wakifumbia macho uhalisia
wa hali halisi.t.r.a wakusanye pato hilo tuone kama hatuta kuwa na maisha bora wote.
 
Vyote hivi vimeanzia kwetu huku uchagani,ukijidai una fedha zako ukagoma kuwachangisha basi unasusiwa harusi.
Inashangaza mzaramo alipokuwa anatepembea kwa mdundiko alionekana mshamba wakati leo hii kuna matarumbeta yanayopiga style ile ile.
Mimi huwa sichangi na kwenye harusi yangu sitachangisha.
Naunga mkono hoja.

Harusi yangu nilifanya mie na mke wangu, best man wangu alikuwa rafiki yangu ambaye alijigharamia mavazi yake yy na mke wake. Hakukuwa na mchango wowote, niliwaalika wanafamilia na marafiki wachache. Harusi ilipendeza sana, walikula na kunywa kwa nafasi na vinywaji walibeba. Washkaji zangu na baadhi ya ndungu zangu eti walinilaumu, kwa nn sijawahusisha, niliwaambia pesa za michango wakawasaidie wasio jiweza. Nilifanya maandalizi kwa muda wa siku saba tu, hakukuwa ata na vikao. Tatizo vijana wa kibongo wanapenda vitu vya bure tu. Yaani kitanda cha kulala ww na mkeo, unataka watu wakuchangie!!
 
jaribu uwachangishe watu ati umepunguwa ada ya shule
utatukanwa mpaka basi. hata akina kayumba tunakufa kimyakimya tu
jamani siyo siri tusipobadilika tutajuta
 
Tatizo Watanzania wanafiki, kwani ni nani anaekulazimisha kuchangia harusi mpaka ulalamike unashindwa ku- save katika account yako! Suala ni kwamba, kama kweli michango inatukera kama tuanavyosema, na tuache kuchangia! Nawahakikishia kama tutafanya hivyo, michango ya harusi itapotea yenyewe. TUACHE KULALAMIKA KAMA KAWAIDA YETU NA TUCHUKUE HATUA! HII INAPASWA KUANZA NA WEWE!!
Mura umeisoma vizuri hiyo post unayojaribu kujibu hapa??? Amesema utakuta hana uwezo wa kuweka laki kwenye account yake lkn akishindwa kuchangia analaumiwa! Sasa wewe jiulize ni sahihi kumlaumu mtu anayeshindwa kuchanga kwa sababu ya kipato chake kidogo? Huna hata laki kwenye account halafu kadi inakudai elfu hamsini. Soma vizuri usijibu kama umurisya!!
 
Kuna harusi inafanyika leo mimi sijaenda kwa sababu sikuchangia! Na hii siyo ya kwanza, ukiniletea kadi kama tunafahamiana sana ninakuuliza 'kulikoni mpendane huko halafu uje kunipiga fine mimi?' kama sikujui nitakukwepa kwa namna yoyote hadi hayo maonyesho yako yapite. Na hii sijaanza leo, ni msimamo wangu wa siku zote.
 
Back
Top Bottom