Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Ulimbukeni umejikita ndani ya jamii ya kitanzania na sasa umeota mizizi. Haiwezekani watu kuchangishwa kila kukicha pesa kwa ajili ya kuziteketeza. Mtu kama anaoa harusi na hana nguvu ya kuwapa watu chakula, ya nini sasa kufanyiwa hivyo na watu wengine? Viongozi ni lazima watoe muongozo namna ya watu wanavyotakiwa kuenenda na ni nini vipaumbele katika maisha. Tena suala hili la harusi linawahusu zaidi viongozi wa dini na kwa kweli ndio wamechangia zaidi ya wowote kuyachinjia baharini maadili ya wanajamii kwa kufumbia macho mambo ya adili na kuendekeza anasa.
Nawaomba watanzania wenzangu tuwekeze kwenye masuala ya msingi na kuachana na anasa na umaarufu usioakisi kile tulicho.
.
 
Fanyeni maamuzi magumu. Mimi huwa nawachunia huwa nasema sasa basi nawanyamazia wote. Ila uangalie umuhimu kama umeoa angalia waliokuchangia uwachangie na kama hujaoa angali ambao unadhani watakuja kukuchangia uwachangie. Na kama umeoa na anayeoa hakukuchangia usipate homa kula jiwe tu tunza wanao.
 
Halafu ukipatiwa kadi ya mchango tena yenye kiasi cha mchango
(Double sh .... na single sh......)
utakuta unatumiwa sms ya kukumbushwa, utadhani ni deni lazima ulipe.
hiyo sms imeandikwa maneno ya kuvutia kutoa mchango
Unajitahidi unachangia, huko arusini unaweza usipate
hata maji ya kunywa.
kweli inakera sana.
 
utakuta li message limeandikwa ''ukiwa kama ndugu yangu wa karibu nakusisitiza kuwa zimebaki siku chache sana kabla ya ndoa kufungu hivyo unakumbushwa kutoa mchango wako. Mungu akubariki sana''! agrrrrrrrrrrrr, mtu mwenyewe alishakuchunia miaka miiiiiiingi iliyopita ila kwa kuwa amepanga kufunga ndoa basi anarudisha urafiki kwa fujo!!!!!!!!! me nimepanga kuwa mstari wa mbele katika kuchangia mazishi au gharama za matibabu sio harusi.
 
This is what is happening to my life now - nimechoka kabisa kuamka asubuhi
sana only to find out that my salary ends kwenye michango ya watu!

MICHANGO! Ah Mungu wangu weee... Nchi gani hii kila ukiamka, kila ukiwa
njiani, ofisini au ukilala ni kusakamwa na michango tu?

Michangooo, michangooo, michangoo tu! Twatolewa weeeee mpaka tumepata
pancha.

Hapana jamani. Hakikyanani tena sasa mmezidi.
Amka asubuhi utasikia hodi, ukifungua kuna mtoto wa jirani na kikadi
kilichoburuzwa kwenye kompyuta kikiomba mchango wa "Kipaimara." Toba!
Unamwambia utawasiliana na baba yake anaondoka.

Upo kwenye daladala unawahi Pugu rodi kazini, kufika kazini unaombwa samahani na mfanyakazi
mwenzako... akidai alikuwa na barua yako na anakupatia bila hiana. Mtumeee! Unafungua
unakuta ni kakadi kengine ka mchango. Safari hii ni ka "chicken party I mean Kitchen party na
kameonyesha kiwango kabisaa. Kwa fasheni ya sasa ni 20,000/-.
Huyu ni wa aibu, hivyo unampa dala ukidai zingine siku nyingine.

Unatoka kazini hujala chochote kwa vile 5,OOO/= ulitoa kwenye"chicken party" ... Kitchen party
ambayo hata maana ya neno lenyewe hujui. Unakuta kengine nyumbani. Hako ni
ka mchango wa "send off'. Jamani mwanitakani lakiniiii?

Unaoga, ghafla aja mtu na kadi, tena safari hii ni mchango wa harusi ya
shemejiyo. unajikamua kamua ili usiadhirike ukweni. Unampatia kiasi
kilichokuwa ada ya mtoto shuleni.

Hapo bado kuhudhuria vikao vya shemejio vya harusi. Nako kuna ka mchango ka
kila mkutanapo kanaitwa uchache au chakaza.Shemeji mtu tena si ni lazima
wakukamue kamasi mwanangu?

Haiishii hapo. Unakuja ujumbe kuwa dada yake dada wa mama yako mzazi kafia
Muhimbii yuko mochwari. Hapo achilia mbali bakuli la mchango utakalokuta
linakungoja. Patakuwepo pia kitabu cha kujiorodhesha wanandugu na kiasi
mtakachotoa.

Yallah! Michango haitoshi. sasa yabidi wale wa karibu yake mjazie ili
iwezekane kukodisha "Fuso" ya kumpleka kwao Mbagala. Na huko nako ni lazima
mkamuliwe tena hela ya kununulia mboga.

Unasema walau sasa napumua. Mara inatoka barua kwa wajomba zako kuwa ile
arobaini ya babu ni mwezi ujao. Na unatakiwa mchango wa kununulia nyama na
mchele kwa ulaji wa siku hiyo.

Kwani utakimbia jamii yenu kwa vile imekuwa ya michango?
Haya tena. Kazini nako wameanza kukukata mshahara kwa madeni uliyo nayo
SACCOS. Mtoto wa jirani ambaye umemdhamini ubatizo naye aja akidai mchango
wa kununulia gauni la "birthday".

Ebo! Sasa mwanangu? Utasahau mdogo wenu wa mwisho aliepigwa ritrenchi na
sasa ana mtoto mchanga wa kubatiza... Utakwepa vipi usimchangie kitu kidogo
atakapowahi kwako majogoo?

Afadhali usingezaliwa Kipatimo mwanangu. Mwezi huu ni wa kuwacheza watoto.
Utawaambla nini huko kwenu wakuelewe kama hukutuma mchango wa hilo tamasha
ambapo mwezi uliopita mtaa wa pili alipochezwa Sikuzani watu walikula
wakasaza?

Bado wana wewe kaka!
Mtoto wa kaka yako anapata komunio utamkwepaje mbele ya jamii
iliyokuzunguka? Na asavali tajiri yako asingekuwa na mtoto Chuo Kikuu
anayegradueti mwisho wa mwezi na keshakuletea kadi ya mchango.
Utachangia sana graduesheni ya sekondari, chekechea hata na darasa la
saba, nini VETA...
Mtajiju ! Kwani nani aliyewatuma kuzaliwa Bongo? Asavali wanajeshi hawana
sherehe hata wapatapo usaameja.

Utadhani sasa utapumua uendapo nyumba za ibada. Toba yaillahi! Huko
Utakutana na michango ya ofisi ya paroko, mchango wa jengo na pikipiki ya
shemasi - kama sio mchango wa madrasa, mchango wa majamvi msikitini ama
mchango wa kofia ya imamu. Upo hapo?

Huko kijijini ndo usiseme. Kuna barabara, shule, maji, zahanati, ugeni wa
DC, vyote vyadai mchango na mara nyingi hakuna risiti. Si ni jamaa zako una
wasiwasi gani weye?

Umesahau mfereji wa kijiji, trekta la mshikamano, shamba la kijiji na
kadhalika - vyote navyo vyataka michango; achilia mbali mchango wa damu
Muhimbili! Ila asavali huu wa damu kwa vile hauhusu fedha.

Unafikia mahali unasema utapanchi hiyo michango. Ukiwaza hayo, mara anapita
Katibu kata mwenyewe. Huyu anadai mchango wa mapokezi ya Waziri Mkuu au ya
Mwenge utasemaje?

Unaambiwa hakuna cha huruma na mtu wala hakuna wa kutaka kujua kipato
chako kabla hajakupa kadi ya mchango.
Shuleni watatuma barua kuhusu mchango wa kumuaga mwalimu mkuu. Bado
michango ya tuisheni, uji wa saa nne, safari ya Serengeti na T-shirt za siku
ya michezo shuleni.

Hapo usisahau redio ya shule ikikosa betri wazazi shurti mchangishwe.
Mwashangaa nini, kwani hospitalini hamchangii?

Michango hii! Sasa mtatukamua mpaka damu. Ipo ya kwaya, Saidia Simba Ishinde, usafi wa
makaburi, basi la kijiji. Bado sijasema michango ya SACCOS na upatu kazini
kwenu.

Enheee, halafu mama watoto anacheza mchezo. wiki hii zamu yake kutoa na
mama nanihino kaja jana kukumbushia asicheleweshewe kama safari ileee...

Hujakaa sawa hodi! Wakala wa wazoa taka yuko mlangoni na kitabu chake cha
risiti mkononi. Anang'aka kwamba safari hii usipotoa atakuripoti kwa
mwenyekiti wa mtaa kwamba huna ushirikiano katika mambo ya kutunza
mazingara.

aaaaaaaaaah...! Nachoka kabisa
 
Sitaki kutoa michango ya harusi kabisa imenichosha, lakini kila nikikumbuka kwamba Harusi yangu ilifana sana kwasababu nilichangisha watu basi nakuwa mpole nakufa na tai shingoni, sijui niwasaliti watu?????????
 
naskia skuizi kuna michango ya graduation ya mtoto wa nursery....., mweeeeh!!!
 
umesahau yafuatayo:
  1. zaka kanisani kila mwaka
  2. tegemeza jimbo
  3. saidia kuhamisha tumaini media kwenda kristu mfalme
  4. sadaka kanisani kila jumapili
  5. sadaka sala za jumuia kila wiki
  6. michango ya ujenzi wa parokia
  7. ujirani mwema
  8. misiba ya wanajumuia
  9. maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa tanganyika
  10. michango wanayodai wanaofukia mashimo barabarani
 
kinachotuumiza hapa ni Culture tu hamna kingine.. nisipotoa atanionaje? n.k Lakini uhalisia unabakia pale pale. mtu anaahirisha vitu vya maana na kujinyima ili achangie harusi.ghrrrrrrrrrrrrrr
 
haya , mwanangu kaja na CLASS PARTY tsh 10000/=
iko kazi........................................................................
 
This is what is happening to my life now - nimechoka kabisa kuamka asubuhi
sana only to find out that my salary ends kwenye michango ya watu!

MICHANGO! Ah Mungu wangu weee... Nchi gani hii kila ukiamka, kila ukiwa
njiani, ofisini au ukilala ni kusakamwa na michango tu?

Michangooo, michangooo, michangoo tu! Twatolewa weeeee mpaka tumepata
pancha.

Hapana jamani. Hakikyanani tena sasa mmezidi.
Amka asubuhi utasikia hodi, ukifungua kuna mtoto wa jirani na kikadi
kilichoburuzwa kwenye kompyuta kikiomba mchango wa "Kipaimara." Toba!
Unamwambia utawasiliana na baba yake anaondoka.

Upo kwenye daladala unawahi Pugu rodi kazini, kufika kazini unaombwa samahani na mfanyakazi
mwenzako... akidai alikuwa na barua yako na anakupatia bila hiana. Mtumeee! Unafungua
unakuta ni kakadi kengine ka mchango. Safari hii ni ka "chicken party I mean Kitchen party na
kameonyesha kiwango kabisaa. Kwa fasheni ya sasa ni 20,000/-.
Huyu ni wa aibu, hivyo unampa dala ukidai zingine siku nyingine.

Unatoka kazini hujala chochote kwa vile 5,OOO/= ulitoa kwenye"chicken party" ... Kitchen party
ambayo hata maana ya neno lenyewe hujui. Unakuta kengine nyumbani. Hako ni
ka mchango wa "send off'. Jamani mwanitakani lakiniiii?

Unaoga, ghafla aja mtu na kadi, tena safari hii ni mchango wa harusi ya
shemejiyo. unajikamua kamua ili usiadhirike ukweni. Unampatia kiasi
kilichokuwa ada ya mtoto shuleni.

Hapo bado kuhudhuria vikao vya shemejio vya harusi. Nako kuna ka mchango ka
kila mkutanapo kanaitwa uchache au chakaza.Shemeji mtu tena si ni lazima
wakukamue kamasi mwanangu?

Haiishii hapo. Unakuja ujumbe kuwa dada yake dada wa mama yako mzazi kafia
Muhimbii yuko mochwari. Hapo achilia mbali bakuli la mchango utakalokuta
linakungoja. Patakuwepo pia kitabu cha kujiorodhesha wanandugu na kiasi
mtakachotoa.

Yallah! Michango haitoshi. sasa yabidi wale wa karibu yake mjazie ili
iwezekane kukodisha "Fuso" ya kumpleka kwao Mbagala. Na huko nako ni lazima
mkamuliwe tena hela ya kununulia mboga.

Unasema walau sasa napumua. Mara inatoka barua kwa wajomba zako kuwa ile
arobaini ya babu ni mwezi ujao. Na unatakiwa mchango wa kununulia nyama na
mchele kwa ulaji wa siku hiyo.

Kwani utakimbia jamii yenu kwa vile imekuwa ya michango?
Haya tena. Kazini nako wameanza kukukata mshahara kwa madeni uliyo nayo
SACCOS. Mtoto wa jirani ambaye umemdhamini ubatizo naye aja akidai mchango
wa kununulia gauni la "birthday".

Ebo! Sasa mwanangu? Utasahau mdogo wenu wa mwisho aliepigwa ritrenchi na
sasa ana mtoto mchanga wa kubatiza... Utakwepa vipi usimchangie kitu kidogo
atakapowahi kwako majogoo?

Afadhali usingezaliwa Kipatimo mwanangu. Mwezi huu ni wa kuwacheza watoto.
Utawaambla nini huko kwenu wakuelewe kama hukutuma mchango wa hilo tamasha
ambapo mwezi uliopita mtaa wa pili alipochezwa Sikuzani watu walikula
wakasaza?

Bado wana wewe kaka!
Mtoto wa kaka yako anapata komunio utamkwepaje mbele ya jamii
iliyokuzunguka? Na asavali tajiri yako asingekuwa na mtoto Chuo Kikuu
anayegradueti mwisho wa mwezi na keshakuletea kadi ya mchango.
Utachangia sana graduesheni ya sekondari, chekechea hata na darasa la
saba, nini VETA...
Mtajiju ! Kwani nani aliyewatuma kuzaliwa Bongo? Asavali wanajeshi hawana
sherehe hata wapatapo usaameja.

Utadhani sasa utapumua uendapo nyumba za ibada. Toba yaillahi! Huko
Utakutana na michango ya ofisi ya paroko, mchango wa jengo na pikipiki ya
shemasi - kama sio mchango wa madrasa, mchango wa majamvi msikitini ama
mchango wa kofia ya imamu. Upo hapo?

Huko kijijini ndo usiseme. Kuna barabara, shule, maji, zahanati, ugeni wa
DC, vyote vyadai mchango na mara nyingi hakuna risiti. Si ni jamaa zako una
wasiwasi gani weye?

Umesahau mfereji wa kijiji, trekta la mshikamano, shamba la kijiji na
kadhalika - vyote navyo vyataka michango; achilia mbali mchango wa damu
Muhimbili! Ila asavali huu wa damu kwa vile hauhusu fedha.

Unafikia mahali unasema utapanchi hiyo michango. Ukiwaza hayo, mara anapita
Katibu kata mwenyewe. Huyu anadai mchango wa mapokezi ya Waziri Mkuu au ya
Mwenge utasemaje?

Unaambiwa hakuna cha huruma na mtu wala hakuna wa kutaka kujua kipato
chako kabla hajakupa kadi ya mchango.
Shuleni watatuma barua kuhusu mchango wa kumuaga mwalimu mkuu. Bado
michango ya tuisheni, uji wa saa nne, safari ya Serengeti na T-shirt za siku
ya michezo shuleni.

Hapo usisahau redio ya shule ikikosa betri wazazi shurti mchangishwe.
Mwashangaa nini, kwani hospitalini hamchangii?

Michango hii! Sasa mtatukamua mpaka damu. Ipo ya kwaya, Saidia Simba Ishinde, usafi wa
makaburi, basi la kijiji. Bado sijasema michango ya SACCOS na upatu kazini
kwenu.

Enheee, halafu mama watoto anacheza mchezo. wiki hii zamu yake kutoa na
mama nanihino kaja jana kukumbushia asicheleweshewe kama safari ileee...

Hujakaa sawa hodi! Wakala wa wazoa taka yuko mlangoni na kitabu chake cha
risiti mkononi. Anang'aka kwamba safari hii usipotoa atakuripoti kwa
mwenyekiti wa mtaa kwamba huna ushirikiano katika mambo ya kutunza
mazingara.

aaaaaaaaaah...! Nachoka kabisa

umeniacha hoi mkuu
 
Haya yote ya kuchangiana Michango yanatokana na mfumo wa Maisha ya Kijamaa yani "Socialism" tuliyotumia baada ya kupata Uhuru kwa nia ya Kuwaleta watu wawe wamoja katika Jamii, lakini katika nchi zilizoendelea huwezi kuona mambo kama haya, huko ni kila mtu na Maisha yake peke yake na familia yake.
 
wakuu kwa kweili hili linasikitisha sana, na si ijanja hata kidogo

- watanzania tuko radhi kuchangia harusi lakini si elimu, kwenye swala la elimu hata ndugu wakalibu hawako tiyali kuchangia, but waambie maswala ya harusi watachangia sana.

- kwa kweli mimi maswala ya kuchangia harusi ni meisha samehe na na waambia sitaki mtu aje anichangie kwenye harusi yangu na nitafanya kwa uwezo nilio nao, hata kama ni ya elfu 50,000.

- niko huku arusha, huku ndo kuna mambo ya ajabu kweli. Siku hizi c michango ya harusi pekee, kuna hiii.

1, send off
2. Harusi
3. Kipa imara- romani katoriki
4. Komunyo- romani katorik
5. Ubarikio- hii ni kwa lutherani
6. Mchango wa kumpongeza mtoto kuhitimu sekondary, chuo, elimu ya msingi na kazalika,

- inaniuma sana kuona mtoto anabarikiwa na kufanyiwa shrehe ya hadi milioni 4, hebu fikilia,na huyo mtoto whena akaja hata kukosa ada ya chuo kikukuu.

- watanzania tuna mambo ya ajabu sana, wakenya wanachangiana kwenye elimu cc tunachangiana kwenye harusi, na mtu anachanga kisa akale wali na pilau. Chakula kitu gani wakuu? Na haya mambo tunayaendekeza c c wenyewe, na bado mtu achange na bado aende tena na zawadi kwenye harusi haya ni mambo ya ki nge se nge se sana,

- hatuwezi endelea kwa mambo haya ya ki nge senge se, kwa nini mtu asifanye harusi kulingana na uwezo wake?
- mbona wazungu walioanzisha kufunga ndoa hawafanyi haya mambo?

- utakuta mtu anaishi kwenye nyumba ya kupanga lakini amefanya harusi ya milioni 10, huu nu unge senge se tu,

- utakuta mtu hana hata basikeli lakini siku ya harusi yake alikodisha gari la six door, huu nao ni ujinga wa hali ya juu na c ujanja hata kidogo

na washangaa sana hata watu wanoa jiita wasomi na wamesoma wana degree ndo wanao ongoza kwa kuondekeza u.fa.la kama huu.

Na harusi nyingi za namna hii za kutafuta sifa ndo hazidumu hata kidogo, mbona kuna watu wanakutana barabarani na wanachukuana wanaishi pamoja na wana watoto na wanaishi kwa amani tu?
 
Ukiona una "mood" ya kuchangia harusi hujue una mawili either unaishi kwa kuogopa ndugu zako na jamii au unazo hela ambazo hujui utatumiaje...

Kama Huna hela wazo la kuchangia halipo hata kama itabidi undugu na ukoo uvunjike!
 
Kwa kweli hii michango inatuumiza sana, hapa suluhisho ni kuichunia tu. Ofisini kwetu kuna sherehe ya kuwaaga wastaafu, wameona hakuna wa kuchangia wameamua kutoa tangazo eti ni LAZIMA watu wote wachangie na ikiwezekana wakatwe kwenye mishahara.
 
jamani michango inakera sana. Halafu mi kinahoniudhi ni jinsi watu wengine wanavyodai utadhani uliwakopa. Yaani mpaka kikao unakiona kichungu. Kali kupita yote ni pale mtu anapoomba mchango eti kwa jubilii ya miaka 25 ya ndoa yake! Navyojua mm hili analufanya mtu anapoona ana nafasi tena sio lazima. Lakini eti kunafanyika vikao kama vile watu ndo wanaoana. Huu ni ushamba wa kukemewa kabisa.
 
Back
Top Bottom