Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

badikeni tangazo ofisini kwenu kama mimi

SICHANGII HARUSI, SEND OFF,KIPAIMARA,UBARIKIO WALA UBATIZO.
nasaidia michango ya elimu pekee ukiwa na uthibitisho maalumu.
MTU AKIINGIA NA KADI YAKE AKISHALIONA TANGAZO HUGHAIRI
harusi yangu ilikuwa simple sana,sikuweka vikao walionipa michango hawakufika 30.
bora lawama kuliko kubali maskini kisa michango ya harusi kila kukicha.
 
Hi!

Enzi za mababu zetu mtu akiolewa ng'ombe anachinjwa ndugu, jamaa na marafiki wanaalikwa tunamuaga bibi harusi na upande wa bwana harusi nao wanafanya hivyo na wanampokea mke wao mchezo unaishia hapo.Mpaka sasa vijijini watu bado wanaendelea na utaratibu huu na harusi zinafanywa bila hata kutumia gharama kubwa.

Jitu lina uwezo wa laki sita linaamua kuweka budget ya milioni 20 wakati hata kiwanja halina.Basi linaanza kuombaomba utafikiri omba omba wa mjini.Jifunzeni kujitegemea kama babu zetu.Cha ajabu zaidi wengi wanaoendekeza utamaduni huu ni wasomi badala ya kuchangia shughuli za maendeleo na kusomesha watoto wao wamekalia kuchangishana michango ya harusi kama mazezeta.Jamii inatarajia kujifunza kutoka kwa wasomi sasa kama wasomi ndiyo wanaibuka na haka kautamaduni ka kishamba nchi yetu kuendelea ni ndoto.

Ndoa ni makubaliano ya watu wawili hata kama mtafanya harusi ya kifahali namna gani haibadilishi kitu badilikeni tuendeleze familia zetu,jamii na nchi yetu kwa ujumla.
 
Mambo ya kuiga na yanakeraaa!!!!!!!

Yaani michango kila kona!

Arusi, kipaimara, graduation, ubatizo, misiba!!!!!!!!!!!!

Yaani badala ya kuchangia elimu tunachangia tu sherehe!!!

Je inatusaidia nini????
 
well said ndio maana mi nitachangisha kutoka kwa watu wote niliowachangia then nafanyia kijijini harusi na naweza tumia kama laki 8 tu zingine nanunua kiwanja fullstop.
 
Mkuu ndani ya wiki hizi mbili za June, tayari ni kadi 3 za harusi na send off, moja 25000, nyingine 40000 na nyingine 50000! Ndani sina hata seti ya sofa! Huu ni use.N.G.Ele!
 
Ni dili, hujawahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi...binafsi nimekuwa mara 2 nimenunua baiskeli
 
Kumbe tuko wengi sipendi mimi mambo ya michango na maharusi ni use...ge
 
Bnafsi hii kitu huwa inanifikirisha sna na sijajua tatizo ni nn maana nichain ya watu wngi wafanyao hvyo, yan unakuta mtu kipato chake cha mwako n 5m tshs, lkn anataka afanye harusi yenye bajet ya 10mlns tshs wkt hana hta kiwanja wala bajaji!!!!
 
Kuna jamaa kila mwezi anaweka kibindoni kama milioni 3 hivi kama mshahara, lakini cha ajabu bwana huyo wakati anakaribia kuoa pasipo hata huruma akawa anasmbaza kadi za mchango hadi kwa watu wenye kipato cha chini kabisa.

Kwa kweli sikuweza kumkalia kimya bwana yule...mtu mwenye mshahara mkubwa kama huyo wala hatakiwi kuchangisha bali anachotakiwa ni kualika watu wakampe support kwenye hiyo sherehe yake.
 
Halafu sasa hao wachangishaji ni wasumbufu...kila siku lazima akuendee hewani kukumbushia...utadhani aliwekeza

Mkuu ndani ya wiki hizi mbili za June, tayari ni kadi 3 za harusi na send off, moja 25000, nyingine 40000 na nyingine 50000! Ndani sina hata seti ya sofa! Huu ni use.N.G.Ele!
 
Uzuri wa michango ya harusi hulazimishwi kama huna hela mtu akikuletea kadi mwambie ukweli wakati mwingine tunatoa ahadi wenyewe na kwa kiasi kikubwa yanakuwa kama mashindano ya nani kaahidi nini. Kuna watu wana hela zao kuchangia elfu 50 au laki moja na yeye pamoja na mpenzi wake kwenda kufurahi ni jambo la kawaida maana angeweza kutumia kiasi hicho kwenye kumbi za starehe kama si kwenda harusini.
Ninachopinga mimi ni kuomba michango hata kwa mtu ambaye unajua hataweza kuhudhuria mfano uko Arusha unaomba mchango mtu wa Mbeya hii imekaaje? Labda kama huyo mtu uliwahi kumchangia au ni ndugu yako vinginevyo kama ni rafiki ni kiasi cha kumpa taarifa si kumuomba mchango.
 
Back
Top Bottom