Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Hii kitu Ina chosha akili people they spend too much money for nothing hizi smart married three yrs ishakua majangas na umewachangisha watu weee hao hao wanakamati ndio watakulia mkeo, auwakimuona anagegedwa hawakwambii!! That's bull shit!! Ndoa moyoni lisherehe Kubwa la ninj
 
Hili swala la michango ya harusi kila mtu analalamika lakini ikifika wakati wake anachangisha wengine. Ndio maana tabia inaendelea bila kikomo.
Naap sitachangisha mtu mimi koz sifanyi hiyo sherehe ,sana sana ntafanya katafrija kadogo sana na ndugu wachache na marafiki kama 20 tu.Sio kuchanga tu vinaanza vikao ,sipendi kama mnataka kutokomeza umasikini afrika , inakera sana
 
Michango ya harusi ni majanga, halafu wanadai utafikiri ni deni yaani ni kero.
Hapo umenena kama wanakudai vile wakati ni uamuzi wa mtu, poor africans ,utamaduni wa magharibi wa miaka 300 iliyopita tunao hadi leo
 
Tusiwe na uso wa aibu, mwambie anayekuletea kadi kuwa badget ya harusi mwaka huu huna. Na wewe ikifika zamu yako, fanya harusi ya family size unayoimudu, tena kwa muda mfupi tu mfano 2hrs- 3hrs basi. Mimi nimepunguza ushabiki wa harusi, bahati mke wangu yuko against na hii addiction, napeleka zawadi pale ambapo najisikia kufanya hivyo, otherwise salamu za pongezi.
 
Tatizo ninaloliona hapa wengi mnaochangishwa sana ni wale ambao mlichangisha kwa kila mtu hadi mliokutanishwa nao mwezi huo...mimi yangu nilipiga dinner tu,ya mdogo wangu mimi nilitaarifu watu ambao najua ni watu wangu wa karibu ambao either walishaniomba michango au najua kwa namna moja ama nyingine hao wataniomba michango..hata kama ni office mate nachoose
 
Kabla ya kuwa negative kuhusu mfumo huu wa uendeshaji harusi, ni vizuri ukajiuliza maswal yafuatayo:

1.Unataka 'harusi' ya namna gani?!
Kumbuka 'ndoa' ni yako lakn 'harusi ni ya familia, ndugu wa karb, jamaa na marafk, then kama hutak sherehe unatakiwa uwashinde hawa kwanza ... na malalamiko yote ambayo yanaweza kuwa na madhara kwenye ndoa yenu yataisha na kila kitu ktakua poa!

2.Uwezo wako kifedha upoje???
Ipo hv, kama wewe n milionea kwanini uwachangishe watu?Andaa reception mwenyewe na ualike tu watu waje kutumbua .. usiogope, hutakua mwenyewe, wapo weng wanafanya hvyo na utakua umekata ile cycle ya utamaduni wa kuchangishana!!!

3.Umeolewa ama kuoa??
Nategemea wengi walioolewa ama kuoa wasikuunge mkono, kwan majority harus zao zlfanikishwa sana na mfumo huu wa kuchangia gharama ... kama ulvyosema, endelea kuomba MUNGU harus yako ifke then ndo ujue hv vtu vnafanykaje!Ving haviend kama unavyodhan ...

4.Umelazimishwa kuchangia??
Kwa asilimia kubwa jbu n hapana, unaouamuz wa kuchanga ama la, na amini its a gamble wasio kwenye ndoa wanalazmka kuchangia kwa munajl wa kuchangiwa muda wako ukifka!!Najua waliokwenye ndoa hawawez kulalamika kwan ndoa yenyewe n 'taasis' inayojtegemea hvyo kad zszo na tija huwa wanaztupia chn ya uvungu kmya-kmya!Anza leo kutochangia utengeneze a good cycle ya kutochangia ambayo victim wa kwanza utakua wewe!!

Mwisho, let me show my interest now, mine expect to be on early october so exposure yangu kuhusu hii ishu!!!Ushaur kwa wakaka tu, creat as many g'd friend as u can ili siku hyo ikfka upate watu wa kufurah nao hata kama htawachangia ....

THX
 
Michango ya harusi inafa kwa ndugu wa karibu tu na pia inategemea unataka harusi yako iweje, lakini hii habari ya kuletewa kadi ya ndugu wa rafiki yako rafiki yake anaona hanioni ng'oo.
 
Mmmmh kweli jamani Harusi zinatia hasara tatizo nikwamba wengine wanataka kuacha gumzo la mwaka hivi mtu anakuopmba mchango anafanya kusema Yani nataka harusi yangu iweke Historia ...huo si ushamba?Ufanye harusi ya gharama ukimaliza mwaka mzima unaofuata we ni kukatwa madeni na benki mshahara unapokea nusu kisa na mkasa????
Mi nadhani kufanya harusi za gharama ni Umburula tu.....harusi simple yenye watu wachache inapendeza sio ufanye harusi kuuuubwa utake sifa ya kualika mtaa mzima kesho na kesho kutwa unaanza kuwagongea kuomba chumvi na kitunguuu akaaaa
 
yani tena mwingine unakutahumjui kabisaaaa akijua anashughuli miezi miwili mbeleni anaanza urafiki na salamau kwa saaaana jamani khaaaaaa
 
Michango ya harusi ni majanga, halafu wanadai utafikiri ni deni yaani ni kero.[/QUOTE]

ahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa_kuna mdada ananichukia kisa nilimchangia 30,000/=,...yaani ni upuuzi kuifanya sherehe yako na umpendae kero kwa wengine.
 
Hii pia inasababisha watu kukosana maana unaweza kuwa unamatatizo kibao muda huo lakin jamaa akiona hujamchangia anakuchukia....!! Tujifunze kujiandaa wenyewe.
 
Yani kero....mimi nadaiwa hapa mpaka bas.Cm ikiisha charge bas umenizimia.Ngoja nimpe leo nusu,nusu mwisho wa mwez maana kutoa pesa kwa mkupuo inauma.
 
Back
Top Bottom