Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Nimeshuhudia watu wanavyofunga safari kutoka Dar kuelekea Loliondo. Nasubiri matokeo baada ya kurudi kwao maana wengine ni marafiki zetu.
 
Jana Mwandishi wa TBC Alikwenda hoku. TBC Ilionesha kipindi kizuri sana. Mlinzi wa Jamaa wa getini alitoa maelezo nanukuu " mwanzoni yalikuwa yanakuja magari 10 kila siku, ikawa 20 ikawa 40 ikawa 70 kwa siku. Sasa hivi yanakuja magari 200 kila siku". Mwisho wa kunukuu.

Ilionekana misafara mingi sana. Watu wengi sana walionekana kupitia TBC Na kuripitiwa gharama za kufika huko ni shs. Elfu 70.

Jamaa hafichi, alimuonesha mwendishi Mti aliooneshwa na Mungu. Kaupanda nje kwake lakini mtu mwingine yeyeto awaye hawezi tumia isipokuwa Kaagizwa yeye tu. Alitoa maelezo alionekana ana umri kati ya miaka 65 na 70. Kuna kitu kinafanyika kwake. Siyo bure.
 
jamani huyo mchungaji atafutwe haraka na wizara husika kabla mambo hajawa mabaya,watu wataambukizana hapa wakifikiri kweli dawa ipo,chonde chonde wizara fuatilieni hili,kama kweli najua kwenu si habari njema kwasababu mnapata sana kupitia misaada,ila hili wekekeni huruma mbele maslahi baadaye

Waziri mdogo wa afya alihojiwa na alitoa baraka zake!!
 
nieleza kuwa huyo mwarabu wa Loliondo ni Brigedia msataafu Al Adawi! Nimeshindwa kumkatalia kwa kuwa simjie anayehusika, wadau tusaidiane
 
Kaenda kumchukulia mkwere aache kale kaugonjwa kake ka kuanguka wakati wa kampeni
 
Waziri mdogo wa afya alihojiwa na alitoa baraka zake!!
Kwa taarifa na yeye alikwisha kunywa hiyo dawa,asilimia kubwa ya viongozi wamekunywa na wameona mafanikio ingenkuwa na matatizo FFU badala kudhitbiti isitolewe sasa wanasimamia utaratibu ili kila aliyefika apate dawa.
Taarifa niliyoipata pia kila siku kuna basi kumi zinapeleka watu,mabasi hayo yanatoka Arusha na moshi,Arusha basi linaloongoza ni Coastline ambalo nasikia siku mbili zilizopita liliuza abiria wa Dodoma ili kwenda Loliondo,jumla ya basi za coastline zinazofanya safari ya huko ni tano.
 
Kama ni kweli, Serikali na taasisi husika zifanye jitihada za kiutaalamu ili dawa zake zitambuliwe na TFDA na WHO (ila WHO wanamizengwe sana). Hii itawezesha makampuni yanayotengeneza dawa kufanya naye kazi kwa mkataba ambao utamwezesha yeye kupata faida kubwa na pia itawezekana kusaidia watu wengi zaidi, kupitia mass production ya dawa hizo na huduma sehemu mbalimbali. Au zinamasharti ya kiza?
 
Mshaurini ahamishie kituo chake Dodoma katikati ya nchi ili iwe rahisi kwa watanzania kutoka kila kona ya nchi kumfikia.
 
Mshaurini ahamishie kituo chake Dodoma katikati ya nchi ili iwe rahisi kwa watanzania kutoka kila kona ya nchi kumfikia.

Kutokana na maono aliopewa na Mungu ni kwamba huduma yake inatakiwa kutolewa at source!
 
kumbe waathirika wengi anasingiziwa Liumba na Mkwere tu:hand:
 
huyu babu ukisimuliwa unaona ni utan ila ukiona watu wanavyopona ndo utaamini dunia inaenda mwisho jamani

Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Join Date : 5th March 2011
Posts : 1
Thanks 0Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0




Karibu Jamvini Kaka!!!
 
Mie nimestaajabia sanaa miujiza hii ya huyo mzee, Mungu ambariki na kumzidishia pumzi ya uhai atibu wengi kama sio kazi ya kishetani......sasa hofu yangu ni usalama wa hao watu na huyo mzee, maana katika taarifa ya habari ya jana TBC1 watu ni wengi sanaa ukilinganisha na hutuma za kijamii zinazopatikana eneo hilo.....
 
BABU AMESHAWAHAKIKISHIA WATU WALIOPO HAPO kwenye mafoleni kuwa HAKUNA ATAKAYEZIDIWA, wala kufa katika himaya yake hiyo...maana aliona wengine wakikata tamaa ya kupata dawa, na kuhofia maisha yao.

Na ukweli ni huo kuwa hakuna baya lilijiri maeneo hayo...

Wanafikishwa hapo watu ambao walikuwa wanalishwa na kuvalishwa, lakini wanaondoka wakiwa wanapiga hadithi...
 
Back
Top Bottom