Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

biashara imehamia JF,ziunganisheni zote basi maana ni mtu mmoja huyu anaepost hii kitu:hand:
 
mkuu huyu jamaa atasababisha watu waache dawa muhimu za haya magonjwa sugu wakiamini mauzauza ya huyu mganga.hii itapelekea watu kuharibu mwenendo wa tiba zao za kawaida.

Sasa we unaona kipi bora waendelee na dozi huku wakifa taratibu, au aamini apone kabisa na kuendelea na enjoyment ya muda wa maisha yao uliobaki? hata kwenye biashara risk averse remain poor na risk takers wanachance ya kubwa ya kuuaga umskini milele..So my friend let them choose what they want; au nawewe unaogopa utakosa wateja wa kuja kukupa consultancy fee na pesa za dose?
 
Mi nachohofia wanasiasa muda si mrefu wataanza kumsumbua huyu BABU
 
Sina wasiwasi na miujiza ya huyu Bwana , lakini nina mashaka na "mungu" anayefanya kazi kwa staili hii. Kwa ujuzi wangu mungu wa namna hii ni yulee mwenye kujipendekeza, wa biashara, mwenye lengo la kuwavuta watu kwake hadi wakamsahau yule mwingine aishie katika ukimya na ukamilifu.
Shetani ana uwezo wote wa yanayofanyika hapo na kwenye baadhi ya "makanisa" yanayojiita ya kiroho ambayo "miujiza" ndiyo chambo cha kuwavuta waumini wanaowatajirisha wajanja wanayoyaasisi!
 
mie nasubiria hao wana JF walioenda warudi na ushuhuda humu.:A S 13::A S 13:
 
Kweli ukiwa desperate utaamini kitu chochote.
 
PJ penye wengi hapakosi mengi. Juzi alhamisi gari moja lilikuwa linarudi nyuma na kumgonga mtoto mdogo na kufa papo hapo. Jana ijumaa mgonjwa mmoja aliyekuwa amezidiwa sana alikufa kabla ya kuonana na Mchungaji. Penye neema kuna maafa pia.

mweh basi waweke utaratibu wale waliozidiwa sana ndio wamuone kwanza huyo mchungaji
 
kwani huyo mganga amegoma kuhamishwa? Rai yangu kama hajagoma siwamlete A Town, then watu anaowaamini ndio wawe wanaifata hiyo dawa kule loliondo kumletea hapo Town. Hata mitume hawakupata kumuona mungu je iweje yeye aseme mungu kamuonesha shilingi mia tano, na je ni noti ipi aliyomuonesha mia tano mpya au ya zamani. point ni kwamba wenye uwezo wa kufika wafike na kama ulikuwa muathirika ukipona ndo ukomee hapo zinaa na utubu ukweli wa kutubu
 

Nakubaliana na wewe kwa namna nyingi lakini pia judgement tumwachie Mungu kama nila shetani litakuja backfire very soon kwani God is still alive and in full control...Cha msingi kila karama ya Mungu haina masharti na matunda yake yanadumu..Nikweli kuwa shetani anaweza kujigeuza kuwa malaika wa nuru na ndipo hapo neno la Mungu linatuasa tuzipime roho kwanza kabla ya kuzikubali kazi zake maana amelaaniwa mtu amwaminie mwanadamu na kumfanya kuwa tumaini lake na huku moyoni amemwacha Mungu.

Swali na doubt yangu kubwa kwa huyu bwana ni kwanini emphasis yake ni kwenye uponyaji wa mwili na huku kwenye roho anapaacha bila tiba? A true God's healing miracle healeth both spirit and body but always the emphasis is the spiritual healing ambayo hatimaye inaingiza a total transformation na kinga kamili kwa mwanadamu (recreation) and through that there would be a vitalization to the attacked body in the future case...which is not the case for this bwana kwani watu wanaponywa sukari alafu wanarudia matendo yale yale yaliyosababisha sukari kuingia mwilini....Ina maana kuna latent factor ambayo hiyo healing imeshindwa kuiondoa na hiyo ni kama for example kiu ya kunywa pombe...For a truly healed person hiyo kiu inaondoka kwani ndani yake kunaushuhuda/dhamira inayomfanya aichukie na siyo kujizuia like kama ambavyo mtu hawezi kula kinyesi siyo kwamba anajizuia bali there is a force which prevent that person not to na hiyo inakuwa controled na mind..

Lakini pia siwezi kumjudge kihivyo na kuhukumu kuwa ni nabii wa uwongo maana simjui and Mungu ananjia nyingi ya kupanda mbegu ya imani ndani ya mtu yaweza kuwa through that healing in later years wengi wakaja kutambua kuwa huo ulikuwa uponyaji wa Mungu na kumpokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yao hivyo sifa na utukufu kumrudia Mungu na siyo huyo Mchungaji kwani Mungu naye anamjua vizuri mchungaji kuliko sisi na amegawa karama mbali mbali kwa different indiviual each playing a particular and a specific task Holly spirit akiwa ndiye mwenye nguvu na mamlaka yote ya hayo kutendeka jinsi apendavyo; thats why I am emphsizing to take a precaution before being involved lakini pia bila kuwa judgemental na mtu akishuhudiwa moyoni mwake akapate hiyo tiba for me its a hundred percent acceptable because its all about faith and not science!
 
Mi nachohofia wanasiasa muda si mrefu wataanza kumsumbua huyu BABU

hasa chadema maana ndio wanapenda waonekane kuwa nao wapo. ivi si muda mrefu utasikia slaa na mbowe wametia timu huko
 

Vichwa vilevile,
hivi kwako muathirika ni wa ukimwi tu? Hata kama ni wa ukimwi je ni lazima awe amezini?
 

Nikweli unachosema, I once when was pregnant of my first born outside the country..Sasa nikaambiwa kuwa nitoe history ya ndugu zangu wakti wa uzazi na 50% wenye maumbile kama yangu walikuwa wamepasuliwa. Me on my side nilishajiambia sitaki kupasuliwa so ili kuondoa biase ya Dr. nikaandika hakuna hata mmoja aliyepasuliwa wote wana deliver normally. Dr. akanipima baadaye akaniambia it seams wewe hutaweza kudeliver normal...akasema itategemea your choice though ila tutaweka hii note wakati wa kujifungua ikitokea tatizo tutakupasua..Then kabla ya my time siku moja nimeenda clinic Dr. kunipima nikaona anachukua simu akaita tax nikaambiwa nisiende nyumbani moja kwa moja niende referal hosp...Nikaenda kufika kule duuh nikawekwa ma machine mengi mengi then nikauliza kwani tatizo nini wakaniambia we suspect the baby is dead...nikamwambia dr. my baby can never die! Akaona huyu mgonjwa anajipa moyo...akasema yes its good to think that way but also its gud to prepare your mind incase we find out its dead...nikamwambia tena I choose not to prepare my mind for the lose but to believe is alive for christ is also alive and have never left me alone...Dr. akaona hii argument siyo nzuri akaendelea na vipimo..So akasema I cant feel the beats and you see you can read from your side there is graph nikamwambia I dont believe the graph give me time...Basi wakaniambia okay then we will examine you after 15 min. naona alinikubalia ili asiniumize..Then after 15min they examined wakakuta mapigo kwa mbali...nikaambiwa nipumzike na nilale kwa ubavu kila baada ya 5 min wananichunguza mapigo yakapanda mpaka normal... Then wakasema wanipeleke theatre pindi ile enxiety ikiondoka nikamwambie dr. I dont want that way i will deliver normally...So dr. akaniangalia akasema please its risk for me I understand what you mean my darling na kuni pet pet kwingi..Nikamwambia I will sign and will bear all the consequences! Wakaniacha day one niko salama na mtoto mzima then wakasema kama ndivyo basi tuna initiate labour lakini kama contraction hazitakuwa nyingi then tunakupasua nikasema sawa...Wakanianziashia put the cathetor and kuniwekea maji ya uchungu huku waki monitor progress ya mtoto..and the thing went on mpaka nikapata baby boy normal bila kupasuliwa alive until todate Glory to God!

So second born at Aghakhan dr akaniambia nipeleke report ya yule wa kwanza kusoma akasema huyu ceasarian session kama kwenye excelent centre mambo yalikuwa hivi sisi hatutake risk...nikanyamamza maana dr wetu collaboration na mgonjwa unatakiwa kuwa makini they know almost everything even against your will...So was praying God to make my day of delivery before that date nakweli ikawa a week before na dr. aliyekuwepo akasema aah huyu mwacheni mbona anajifungua kawaida ila mwekeeni maji ya chungu and thats how I got my second born. Why all this kuwa chosha no but to tell you siyo kila kitu science inaweza kujibu na mjue kuwa kama ni hiyo science hata mimi naifahamu inside out lakini haijatawala maisha yangu iko applicable to a limited extent for me science without faith is empty!
 
Jamani naombeni ufafanuzi juu ya suala hili. Niko silias tafadhali kwa mwenyemapenzi mema naomba anifafanulie
 
kuna wana jf wameenda huko wanarudi kesho asubuhi kua mpole utapata news zooote
 
Huyo babu atakuwa anachoka sana.
Kasije kakafa kwa kukosa mapumziko.
 
Jamani!! Mbona kuna wanaJF wamekwenda huko na wakaahidi tutapata kila kinachojiri na mpk ss ha2oni?
 

ila imekaa sana kimatangazo tangazo vile
 
Tunasubiria kesho tupate more news kutoka kwa wana JF.......
 
Kama ni kweli basi mola atakuwa amewakumbuka waja wake na kuiteua Tz kama sehemu ya kimbilio la wagonjwa.
Serikali inabidi kuboresha miundombinu uko ili mamia ya watu wanaoenda uko wasije dhurika na ukosefu wa huduma za jamii.
Maana nasikia ni nyomi la kufa mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…