Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Wekeni taarifa za uhakika zikiambatana walau na kaushahidi hizi stori zinazidi mpaka wengine wanadiriki kusema mukulu j wa k kainekana huko!
 
Mi sisemi saana,ila nauliza huyo babu anatibu hata vidonda vya tumbo bcoz vinanitesa sana jamani.
 
Naomba kujibiwa swala hili kwa mwenye ufahamu tafadhali. Huyo babu mnasema ni mchungaji/askofu and the like. Na kuwa imani ndio inaponya. Je watu wa dini zingine eg waislamu nao wanaenda? Je wanaoenda nao wanapona wakibaki na imani ya dini zao? Msaada tafadhali
 
Naomba kujibiwa swala hili kwa mwenye ufahamu tafadhali. Huyo babu mnasema ni mchungaji/askofu and the like. Na kuwa imani ndio inaponya. Je watu wa dini zingine eg waislamu nao wanaenda? Je wanaoenda nao wanapona wakibaki na imani ya dini zao? Msaada tafadhali

mkuu ... sawa sawa .... unatumia imani yako inayokufanya umjue mungu .... yaani dini ya aina yeyote wanakwenda
 
huko hadi huduma ya dawa imekuwa tata.nimetoka huko jana na nimeshuhudia magari zaidi ya elfu mbili ya watu binafsi,mabasi makubwa na magari ya idara za serikali.Huduma za jamii kama hotel,vyoo na mawasiliano hakuna
watu mashuhuri na wengine wamekuja kwa helikopta wamefika hapo.polisi wilaya wamewasiliana na uongozi wa wilaya,mkoa na taifa kuomba msaaada zaidi wa mfumo wa kusaidia watu..tatizo ni kuwa mpaka mzee mwenyewe atoe dawa kwa mkono wake mwenyewe.
watu niliowapeleka hawakufanikiwa kupata dawa na hivi sasa tumerejea arusha
Insp gen mstaafu wa polisi ndg Mahita ni mmoja wa watu niliowaona na Choper ilikuja na kijana wa mzee Ndesamburo
 
alipooteshwa na Mungu amemwambia kuna meli mbili zinakuja na watu kutoka ulaya watakapoisha tu watu hao na dawa itaisha nguvu so watu waende kwa wingi wawahi maana meli zinakaribia kufika.Kuna habari nimezipata kuwa Mkwere alipokuwa kwenye zoezi la kufukua nyayo alipita kwa mchungaji na kupewa dawa mwenye macho haambiwi tazama na masikio haambiwi sikia na ****** haambiwi kujamba kila mwenye tatizo aende aapate tiba!
 
Huko Loliondo kuna maelfu ya watu, hakuna choo,maji,hotel, na magonjwa ya mlipuko yakitokea itakuwa janga la Taifa.

Kwa nini serikali ipo kimya ikasaidia kuweka utaratibu?

Msalaba mwekundu waende huko ili watoe huduma
 
Waambieni redcross wapeleke mahema. Mimi naenda kujenga danguro a.k.a guest house hapo jirani sasa hivi.
 
Kulingana na uwingi wa hizi posts naamini huyu mtumishi wa mungu amewezeshwa kutibu maradhi haya. Naomba aliyefika hapo atueleze prescriptions za hizi tiba.
 
Serikali iko bize kuandaa matamko mapya dhidi ya CHADEMA, kwani ulishaona wako serious na welfare za watu wake
 
Hivi wewe unauliza serikali gani? Swala la kijamii sio swala la serikali..labda wasikie watu wameshakufa ndo utawasikia wakitoa tamko..wao wapo tayari kupambana na tatizo na sio kuzuia tatizo lisitokee! Wapo busy kujibu mashambulizi ya CDM
 
Huko Loliondo kuna maelfu ya watu, hakuna choo,maji,hotel, na magonjwa ya mlipuko yakitokea itakuwa janga la Taifa.

Kwa nini serikali ipo kimya ikasaidia kuweka utaratibu?

Msalaba mwekundu waende huko ili watoe huduma

Habari iko nusunusu haieleweki, Kuna maelfu wamefanya nini?
 
Ni juzi tuu mkuu mmoja wa serikali alitangaza kua ugonjwa kama wa kisukari hauna dawa kabisa, leo gazeti la Mwananchi linatoa taarifa kua kuna mchungaji anatibu kisukari, ukimwi na magonjwa mengine sugu. Kinachishtusha sana ni kuona akili za waTanzania wengi namna gani zinaweza kukinaishwa maramoja.

Ugonjwa kama ukimwi kisukari nafikiri sio ugonjwa wa mtu kupewa kikombe kimoja cha dawa na kufika kwenye conclusion kua mtu ameshapona, tunaribu kua reasonable, hivi ni vitu vinahitaji muda kidogo ili kujua kua kweli dawa hiyo inatibu.

Upande mwingine ni ule wa mtu kudai kua ana mawasiliano na God hili nalo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kinachoshtusha zaidi ni kusikia watu ambao tunawaamini kua ndio viongozi wa taifa letu kama wabunge mawaziri wanamiminika huko na mkuu wa mkoa anaiomba serikali ifacilatate mazingira ya watu kwenda. Hii ndio Tanzania yetu. Mungu ibariki dunia, Afrika na Tanzania
 
mkuu kila mtu na roho yake wew kama huamini wengine wana amini. pole sana
 
Back
Top Bottom