Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu huyu jamaa atasababisha watu waache dawa muhimu za haya magonjwa sugu wakiamini mauzauza ya huyu mganga.hii itapelekea watu kuharibu mwenendo wa tiba zao za kawaida.
Sina wasiwasi na miujiza ya huyu Bwana , lakini nina mashaka na "mungu" anayefanya kazi kwa staili hii. Kwa ujuzi wangu mungu wa namna hii ni yulee mwenye kujipendekeza, wa biashara, mwenye lengo la kuwavuta watu kwake hadi wakamsahau yule mwingine aishie katika ukimya na ukamilifu.Mie nimestaajabia sanaa miujiza hii ya huyo mzee, Mungu ambariki na kumzidishia pumzi ya uhai atibu wengi kama sio kazi ya kishetani......sasa hofu yangu ni usalama wa hao watu na huyo mzee, maana katika taarifa ya habari ya jana TBC1 watu ni wengi sanaa ukilinganisha na hutuma za kijamii zinazopatikana eneo hilo.....
PJ penye wengi hapakosi mengi. Juzi alhamisi gari moja lilikuwa linarudi nyuma na kumgonga mtoto mdogo na kufa papo hapo. Jana ijumaa mgonjwa mmoja aliyekuwa amezidiwa sana alikufa kabla ya kuonana na Mchungaji. Penye neema kuna maafa pia.
jamani, kipindupindu ana hoja nzito!, kuna mtu alishajifanya nabii kule mkuranga lakini eti wakati akipokea ufunuo simu ikiita ufunuo unapotea ghafla!.. kuna mtu anajifanya nabii kule Tabata, anawaambia baadhi ya kina dada alale nao ndo wapone!.
Wengine kati ya hawa wanaojiita "Waponyaji "ukiachilia ugonjwa wa akili, wanakumbwa na mapepo, yanawadanganya, yanawaambia wao ni manabii n.k, lengo ikiwa ni kuwadanganya watu ili wayatumikie na kuyaabudu, yanawapa matumaini ya kuponya maradhi kama vile ukimwi, uzazi n.k... lakini at the end of the day yanawapeleka kusiko kabisa, unaweza kujikuta umegeuka kuwa mchawi bila kujijua, kwa kufuata mambo haya ya waganga!
Tuweni makini wanadamu, Shetani ni laghai mbaya kabisa
Mi nachohofia wanasiasa muda si mrefu wataanza kumsumbua huyu BABU
kwani huyo mganga amegoma kuhamishwa? Rai yangu kama hajagoma siwamlete A Town, then watu anaowaamini ndio wawe wanaifata hiyo dawa kule loliondo kumletea hapo Town. Hata mitume hawakupata kumuona mungu je iweje yeye aseme mungu kamuonesha shilingi mia tano, na je ni noti ipi aliyomuonesha mia tano mpya au ya zamani. point ni kwamba wenye uwezo wa kufika wafike na kama ulikuwa muathirika ukipona ndo ukomee hapo zinaa na utubu ukweli wa kutubu
Ni kawaida ya binaadamu kudharau kitu na kusema kila aina ya maneno ya dharau juu ya kitu hicho na hasa ikiwa si yeye anayekihitaji. Nasema hivyo kwa sababu kama ni wewe ndio ungekuwa unaumwa na moja ya magonjwa hayo yaani Kisukari, Presha, Kansa, na hata HIV, naumekuwa ukitumia kila aina ya dawa zinazojulikana leo hii katika fani ya Tiba (Hospital na Kienyeji) lakini zote hizo bado hujapata nafuu, sidhani kama ukisikia dawa kama hii hutaacha kwenda kujaribu, kwa kuwa tu ati ushatumia dawa nyingi na hujapona. Waswahili husema uongo wa mganga nafuu kwa mgonjwa. Mi nafikiri it worth to try, in case haitibu basi utakuwa hujijutii zaidi na iwapo itakuwa inatibu basi utakuwa umepona. Baada ya kusikia habari za mganga huyu nilijaribu kufuatilia kwanza kupata ukweli juu ya huyu mtu kama kweli yupo na je kweli anatibu. Katika jitihada hizo nilimpigia simu jamaa yangu aliyepo A town, na yeye akasema anasikia habari hizo na ili kuwa na uhakika akawasiliana na Rafiki yake ambaye anafanya kazi halmashauri ya Loliondo, na yule bwana alienda hadi pale kwa huyo bwana na akakuta kweli kuna watu wengi na wanapata tiba. Yeye hakwenda tibiwa ila dereva wake alikuwa akisumbuliwa na kisukari na akapatiwa dawa hiyo. Na toka amepata hiyo dawa ni wiki sasa imepita na hali yake anasema ni nzuri na sukari iko normal. Pia kuna jamaa wanafanya kazi hapa Dar, CBA Banki hapa Dar. Hawa jamaa walikuwa wanasumbuliwa na sukari, lakini nao wanasema hali yao ni nzuri na wanakula kila aina ya chakula walichokatazwa kama soda, mafuta, sukari nk na pamoja na hayo hali zao ni bomba. Sasa mi nafikiri tuache watu wajaribu may be watafanikiwa.
Jamani!! Mbona kuna wanaJF wamekwenda huko na wakaahidi tutapata kila kinachojiri na mpk ss ha2oni?Wandugu huku kwa huyu mganga anayetibu magonjwa sugu kama vile,ukimwi,kisukari,presha,kifafa nk. Ni mbaya kwani watu ni wengi maelfu kwa maelfu huku huduma muhimu kama chakula,malazi,mahali pa kujisaidia, mawasiliamo ya simu hakuna. Kupata huduma siku izi inachukua adi siku tatu.
Wandugu huku kwa huyu mganga anayetibu magonjwa sugu kama vile,ukimwi,kisukari,presha,kifafa nk. Ni mbaya kwani watu ni wengi maelfu kwa maelfu huku huduma muhimu kama chakula,malazi,mahali pa kujisaidia, mawasiliamo ya simu hakuna. Kupata huduma siku izi inachukua adi siku tatu.
Ukweli ni kwamba anatoa dawa na imani ya wenye taabu wanapona!hakika Mungu anaipenda Tanzania sana mnaobeza wote ni CCM.