Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

...non sense stuff, from clue-less padre, for the sleeping masses.
 
Mimi jamaa yangu ana ngoma ameenda kwa Babu akanywa dawa baada ya wiki ambayo ni jana amepima bado hajapona hivyo tunasubiri muda zaidi tukiwa na imani
 

mh Macho! huenda una point!
 
kama ni kwa jina la Yesu angewahubiria watu waokoke sio tu kupewa kikombe cha dawa na kuondoka bila wokovu.pole uliyedanganyika. Yesu wetu anataka watu wote waokoke na waijue kweli bwana.

Mbona hatujasikia mahubiri yoyote pale! PALE YESU HAYUKO .IKO MIZIMU YA KWAO NDIYO INAYOTIBU!
 
Dah!!! Mungu wabariki watumishi wako!!! Ushukuriwe Mungu kwa kuwa shauri lako tu ndilo linalosimama. Na mambo yote tunayakabidhi mikononi mwako, ukweli wa mambo haya unaujua wewe Mungu. Utupe neema yako ili tusije tungaamia kwa kukosa maarifa. Ni wewe Mungu uliyetuumba kwa sura na mfano wako, na ni wewe pia unayetulinda na kutuponya nafsi zetu na magonjwa na hila mbaya za shetani.

Ninachokiamini kwako wewe ni wa huruma na Neema huwezi kutuacha tungaamia kwa kutojua ee Mungu. Tulinde sisi na wagonjwa tulio nao uwape afya na nguvu. Utakapofika wakati ulio uamuru wewe mwenyewe uhukumu hukumu ya haki juu ya haya mambo, utupe kuujua ukweli ili huo ukweli utuweke huru.

Amen!!!!
 

Miss, hata wakati wa Yesu watu walikimbilia miujiza na wakati mwingine mikate na vipande vya samaki. cha msingi ni wewe mwenyewe kulijua, kuliishi na kulitenda Neno.
 
Tanzania mambo ya mmpito ni mengi mmno,
miaka ya 80-90's kulikuwa na imani ya kakakuona ,kuwa anatabiri mambo makuu na muhimu,viongozi wa serikali walishiriki ktk hilo zoezi,wanaanchi tukaaminishwa juu ya umuhimu wa kaka kuona na utabiri wa Mvua,Njaa etc
Then ilikuja product moja inaitwa OKO ,inaziba pancha ya gari likiwa in motion,kwamba ukiweka oko ktk gari lako hupati pancha tena,nayo hii ikapita,so kwa babu ni moja ya mozonge ya Tanzania na upeo wetu mmdogo kitaifa wa kupambanua mambo.
 
Nijuavyo mimi furaha ya mgonjwa uwa kubwa apatapo uponyaji, sasa ni vipi hadi sasa kuwe kimya? Naamini ni zaidi ya waTZ milioni sasa wamefika kwa babu na BABU kaweka wazi kisukari upona kwa siku 7 ukimwi siku 21 sasa mbona wagonjwa husika hawasimami kutoa USHUHUDA wa kupona kwao? Naona magazeti tu ndio yana nukuu taarifa za watu kupona au kutopona, jamani kuna tbc,itv na star tv nendeni mkatoe ushuhuda wa kupona kwenu ili wasio amini tiba ya babu waamini hata magazetini basi hata picha za wahusika ziwekwe. kuna mgonjwa wa kisukari yupo hoi kcmc ICU wakati amepiga kikombe cha BABU sasa mtu kama mimi kuniaminisha kupitia magazeti inakuwa ngumu, waliopona wajitokeze ili imani yetu kwa BABU iongezeke.
 

Hilo ndio jibu nililoona linamfaa kwa mtizamo wangu.
Kwani watu wengi wamekuwa wa siri na magonjwa yao. Yeye kwa kuwa anataka kupata scientific result aende yeye aje atuwekee matokeo
 
Kwani tatizo nini,hata kama siyo Yesu yeye na Imani yake Itatosha na kama watu wanapona mim sioni shida yyote.kama imani yako haipo hulazimishwi kuamini
 

Mizimu bomba hii inatibu magonjwa sugu . Mungu aizidishie marifa mizimu ya mwasapile iweze kutibu na matatizo mengine ya wa Tanzania
 
yetu macho, na kila mtu awe na msimamo wake,, una imani ya babu nenda kapate kikombe, huna endelea na maisha yako!!!!
 

Ndugu umenikumbusha mbaaaaali miaka ileeeeeee!! OKO!! Kulikuwa na tangazo lake redio!! Kweli sikumbuki ilienda wapi nailiishaishaje!! Sasa na huyu babu sijui ila kauli yangu: Mwisho wa babu mbaya
 
Hilo ndio jibu nililoona linamfaa kwa mtizamo wangu.
Kwani watu wengi wamekuwa wa siri na magonjwa yao. Yeye kwa kuwa anataka kupata scientific result aende yeye aje atuwekee matokeo

Na kama haumwi aende tu kupata kinga au? Babu amepiga marufuku watu wanaoenda kupata kinga sasa jamaa afanyeje? Ugumu wa watu kutoa ushahidi uko wapi. Wakitoa ushahidi itasaidia sana
 

Am blessed by your prayer. Thanx
 
Miss, hata wakati wa Yesu watu walikimbilia miujiza na wakati mwingine mikate na vipande vya samaki. cha msingi ni wewe mwenyewe kulijua, kuliishi na kulitenda Neno.

mkuu, kumbuka kuwa wakati wa Yesu kulikuwa hakuna wakristo. ukristo umezaliwa wakati wa mitume (apostolic era). zingatia sana hili please.

glory to God
 
mkuu, kumbuka kuwa wakati wa Yesu kulikuwa hakuna wakristo. ukristo umezaliwa wakati wa mitume (apostolic era). zingatia sana hili please.

glory to God

did I mentioned wakristo anywhere? nimesema watu sikusema Wakristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…