Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

tuulizie kama anatoa dawa za mapenzi/mahusiano kuna wanajf wanataabika na mwaswali yasiokuwa na majibu coa huyo ndio babu wa ukweli
 
Mhhh safari njem amwaya!!!Utuambie uponyaji ukikutembelea!!!
 
Sina wasiwasi na miujiza ya huyu Bwana , lakini nina mashaka na "mungu" anayefanya kazi kwa staili hii. Kwa ujuzi wangu mungu wa namna hii ni yulee mwenye kujipendekeza, wa biashara, mwenye lengo la kuwavuta watu kwake hadi wakamsahau yule mwingine aishie katika ukimya na ukamilifu.
Shetani ana uwezo wote wa yanayofanyika hapo na kwenye baadhi ya "makanisa" yanayojiita ya kiroho ambayo "miujiza" ndiyo chambo cha kuwavuta waumini wanaowatajirisha wajanja wanayoyaasisi!
Mmh sijui lakini hata wana wa Israel waliambiwa kutazama nyota wa shaba aliyetundikwa juu ya mti wote waliotizama walipona na wote ambao hawakutizama walikufa. Bali njia nyembaba iendayo uzimani na njia pana iendayo upotevuni.
 
inawezekana alienda kumchukulia dawa mzee, si nasikia mchungaji anatibu magonjwa yote!

huyo KJ mwenyewe ameshaenda, wabunge kibao, eti wanajidai wanaenda kushuhudia kumbe kupata doziiiiiii
 
wakuu hizi habari ni kweli kabisa no joke.....i know mtu wa karibu kaenda kule na kapona ugonjwa mmoja wapo......mganga hataki zaidi ya 500 na huo mti dawa upo kila mahali ila lazima akupe yeye hayo ndio niliosikia ila its true kabisa....uliza watu wa arushab watakuambia ongezeko la magari mjini hapo

Yoyo hiv kuongezeka kwa magari ndo ukweli wa dawa???!! nafkiri hizi ni hope tu za watu wanaoteseka kwa magonjwa. It reminds me of one chap pande za Moshi aliwahisema ametokewa na Bikira Maria ambaye alimpa uwezo wa kugeuza maji na kuyapa baraka za kuponya..we we we we, mbona ilikuwa kimbembe huko Moshi kijijini nyumbani kwa udogo, huo umati kulikuwa hakufikiki. Busara za wakatoliki ndo ziliamua mambo, walim-hold dogo kwa muda wakamchunguza kupitia system zao wakagundua hamna kitu, ilikuwa illusions tu....huyu mzee wa Loliondo tuvute mda kwanza, wataalamu wa tiba watatuambia, take my words......hana dawa, ana kitu inafanana na dawa ambacho kama kikifanyiwa research na kuwa processed kitaalamu pengine kingechangia kupatikana dawa ya maradhi flani kati ya hayo anayosema anatibu. narudia hana dawa....mtakuja kuniambia hapa hapa JF

Tatizo jingine mwafrika akiwa na uwezo natural flan hawezi kuuelezea kitaalam au kikawaida ukaeleweka, lazima aweke hapo ushirikina, mfano lazima hiyo dawa nikunyweshe mimi akikunywesha mwingine huponi, lazima unywe mara moja tu, lazima nigeme mimi hiyo dawa akigema mwingine inakuwa sumu(teh teh teh-ujanja wa kuretain copyright kwa kutumia njia mwitu will not work)
 
Mimi naomba kuuliza huyu mganga anatibu nini maana sielewi? Kuna watu wowote wametoa ushuhuda na tiba yake au ni basi watu kujipanga. Kazi ipo kweli kweli huu mwaka ni mwaka wa matukio

Pakawa ni vigumu wewe kuamini lakini yafuatayo yametokea mjini Arusha, si yakuambiwa bali nimeshuhudia..
-Kuna rafiki yangu alikuwa mgonjwa wa kisukari kwa muda mrefu baada ya kwenda loliondo na kutumia dawa sasa vipimo vinaonyesha sukari yake iko normal
-Kuna mama mmoja na mtoto wake walikuwa waathirika na walifikia kuwa kitandani, ilibidi kuchangiwa na wapangaji wenzao, mara waliporejea toka loliondo muda wa kama wiki moja na nusu mama ni mzima na sasa anaendelea na kazi zake, mtoto amebadilika anaanza kurejewa na afya yake japo hawajacheki virusi.
-Bosi wangu mimi alikuwa na uvimbe kwenye koo (mahali sauti inapotengenezwa) daktari wake alimwambia uvimbe huo unaweza kusababisha kansa na kwakweli alikuwa na kikohozi flani hivi cha kila siku, uvimbe huo chanzo chake ni aleji ya harufu mbalimbali za perfumes na vitu kama hivyo, tahgu atumie dawa sasa hana aleji wala kikohozi hakipo tena.

Sasa kwakifupi matokeo hayo yanashawishi wengi kwenda kupata tiba.
 
Kwanza jina lako linadhihilisha wewe uko hoi, pili nina hakika wewe huna imani na ulimwengu unao ishi. Ukiambiwa hiki ni kivuli chako pia utakataa!!!!!! Sasa waulize watu lukuki waliokwenda Loliondo na mpaka sasa wanakwenda je wanapona????????? Ndg yangu watu wamejaa huko si Waarabu, Wahindi, Wazungu, matajiri ndo usiseme, PM ALIKUWA HUKO, Mkuu wa Boma kaisharudi toka huko. Sijui nikwambie vipi???????? Hayo ni maajabu ya Mungu, ni imani yako tuu. Mwamini Mungu yote yawezekana !!!!!!!!

Jamani dunia ya tatu kuendelea ni ngumu sana. wakati wenzetu wanafanya majaribio ya KISANSI jinsi ya kulifikia jua(ambacho ni kitu kigumu sana kutokana na moto wake mkali) sis huku dunia ya saba...aha sori ya tatu..tunanyweshwa mifori(kinyesi-maji cha ngombe) na vitalolo(chakula flani cha wachaga chapikwa kwa mbogamboga) eti ni dawa ya kuuwa virusi wa HIV...Hiv serkali inasubiri nin kwa nini haimkati huyu jamaaa, anasababisha confusion katika jamii bure na ataua watu wengi sana kwani watu wameacha tiba wanakimbilia porini kulishwa uchafu. kama kuna watu wa dunia ya kwanza wapo huko ni ili wachukue hiyo concoction wakaifanyie testing scintifically nawala hawapo huko eti kupata dawa!!!

kuna jamaa mmoja m-tasha flan alisema waafrika wamelaaniwa watu walimjia juu lakin utasema nini pale hata mkuu wa mkoa anapoamini illussions kama hizi?? most of we africans are cursed. halafu jamani mnajua ujinga is very expensive to pay for
 
jamani kam huyo Mganga anaonekana anaweza kusaidia umma basi serikali yetu ichukue hatua haraka ya kumpa ulinzi,na apewe msaada wa hali na mali ili afanye kazi yake kwa ufanisi.
NAPENDEKEZA
apewe eneo arusha mjini, aungane na Madaktari ili wafungue matawi KCMC,BUGANDO,MBEYA na MUHIMBILI.
Serikali TUMIA fursa hii kuokoa Taifa.INAWEZEKANA TU,ENDAPO USHAURI WANGU UTAPOKELEWA NA KUFANYIWA KAZI HARAKA.
 
Back
Top Bottom